Elections 2010 Kwa nini mikoa inayoikumbatia CCM ndiyo maskini zaidi?

RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
Jamani wadau nijibuni. Tukisema ccm ndio chanzo cha dhiki watu wanapinga. Tazama mikoa ya singida, Lindi mtwara na Tabora ambayo ndio ngome ya ccm ni ufukara kwa kwenda mbele. CCM imewasaidia nini? Niambieni jamani kwa nini hawa ndio wako maskini kuliko mikoa mingine?
 
Ni kwamba umaskini unaendana na kiwango kidogo cha elimu (ujinga). CCM wanapenda hao kwenye hiyo mikoa wabaki hivyo hivyo ili waendelee kuzoa kura huko. Lakini kwenye hiyo mikoa mijini utakuta kuna mwamko kigodo kwa wale waliosoma, wenye TV, etc. Kama kura zingekua zinapigwa mijini tu CCM wangekua out toka wakati wa mrema
 
Umaskini na ujinga wa watanzania ndiyo mtaji mkubwa wa CCM. Si kwamba wanapenda kuikumbatia CCM bali ni kutokana na kupata chochote kutoka CCM hasa chumvi, khanga, kofia na tshirt. Mtu maskini na asiye na elimu katu hawezi kuwafagilia wale wanaokuja mikono mitupu. Maana shida yake ni kumaliza matatizo yanayomkabili kwa wakati huo na si matatizo ya kesho. Kwa hiyo kwenda na sera nzuri kwa mtu maskini anaona hazimsaidii kwa kuwa yeye ana njaa leo na anahitaji kula leo. Na hapo ndipo ambapo CCM huwa inafanikiwa kwa kuwa wanatoa hizo elfu mbilimbili, na mabango ya CCM, basi wananchi wa huko maskini wanaona hawa ndiyo wenyewe.
 
Ni kutokana na ujinga wa watu wa mikoa hiyo kwa kipindi chote toka uhuru walikuwa hawajaamka, lakini sasa wameshaijua sisiem na janja yake na mambo yatabadilika baada ya oktoba 31.
 
Umesahau Ruvuma kwenye hiyo list. Nilikuwa nasoma gazeti la mwananchi katika mkoa mzima wa Ruvuma ni Mbinga mashariki tu ndiko kunaonekana kuwa na upinzani kwenye ubunge. Hii ni hatari sana. Ndugu zangu Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa yenye umasikini wa kutupwa.

Nafikiri kukumbatia CCM kama wengine walivyosema inatokana na kukosa elimu na upeo. watu wengi huko vijijini hawapati taarifa sahihi kuhusu vyama vya upinzani. Na hata tunapozungumza kuhusu Dr Slaa (Mr president) ninahakika watu wengi huko Ruvuma hata hawajaona sura yake.
Nilikuwa naongea na ndugu zangu wa Ruvuma wanaonekana kuto kuwa na mwamko kabisa. Bado kuna mawazo mgando kuwa kuchagua upinzani ni kuleta vita katika nchi hii.
Juhudi za ziada zinahitajika kuikomboa mikoa hiyo kutoka kwenye wimbi la ujinga.
 
We umetumia Kigezo ganeni kwamba hiyo mikoa ndo masikini kuliko mikoa mingine?Wacheni hizo ,Watanzania wote masiki
 
Ndio watanzania wote ni maskini lakini ukiiweka mikoa hiyo ktka maskini-meter ita-diflect zaidi to the right. Get the point.
 
shule ndo tatizo kwani huwa mikoa ya mwisho kwenye matokeo, hata wazazi hawana mwamko wa kuwapeleka shule. kwa mfano Tabora mjini, Hiace zenyewe zimeanza mwaka 2002, zilikuwa baiskeli tu pia ukitafuta mwl wa A-level kwa tuition ni shida ile mbaya. So elimu hawa watu hawana kabisa.

na wataendelea kuwa duni
 
Ujinga ni adui namba moja wa maendeleo na CCM wanapenda sana watu maskini. Ukiwatwanga bajaji moja unapata kura za kijiji kizima. Halafu watanzania nasikia siku hizi kikwete anawanunulia NET na Mashuka...Noma mwanamme kununuliwa net!!! Tafakari Chukua hatua
 
Jamani wadau nijibuni. Tukisema ccm ndio chanzo cha dhiki watu wanapinga. Tazama mikoa ya singida, Lindi mtwara na Tabora ambayo ndio ngome ya ccm ni ufukara kwa kwenda mbele. CCM imewasaidia nini? Niambieni jamani kwa nini hawa ndio wako maskini kuliko mikoa mingine?

Umesahau kuwa Kikwete amekuwa mstari wa mbele kutekeleza ajenda yake ya "mikoa iliyo pembezoni" yaani disadvantaged?
 
Jamani wadau nijibuni. Tukisema ccm ndio chanzo cha dhiki watu wanapinga. Tazama mikoa ya singida, Lindi mtwara na Tabora ambayo ndio ngome ya ccm ni ufukara kwa kwenda mbele. CCM imewasaidia nini? Niambieni jamani kwa nini hawa ndio wako maskini kuliko mikoa mingine?

Mikoa ya kusini ilikandamizwa kielimu, kibiashara yote kwa sababu ya CHUKI binafsi ya Nyerere kwa Waislamu. Mikoa ya kusini ina Waislamu wengi kitu kilichomfanya Nyerere kuwabagua. Sasa hivi mikoa ya kusini inaanza kuendelea kwa sababu Dictactor Nyerere hayupo madarakani.
 
nathani unafikiria na ****** na sio kichwa Ruvuma pia kuna Waislam wengi? na Rukwa pia? na Mkapa aliyeanza kujenga barabara huko na daraja je ni Muislam?
 
nathani unafikiria na ****** na sio kichwa Ruvuma pia kuna Waislam wengi? na Rukwa pia? na Mkapa aliyeanza kujenga barabara huko na daraja je ni Muislam?

Daraja ilibidi lijengwe kwa sababu walijua kuna mafuta yameonakana kusini. Makampuni ya Wazungu ambayo yanafanya kazi mikoa ya kusini ndiyo yalitaka daraja lijengwe ili kuwarahisishia kama mafuta yakianza kutoka.
 
Mikoa ya kusini ilikandamizwa kielimu, kibiashara yote kwa sababu ya CHUKI binafsi ya Nyerere kwa Waislamu. Mikoa ya kusini ina Waislamu wengi kitu kilichomfanya Nyerere kuwabagua. Sasa hivi mikoa ya kusini inaanza kuendelea kwa sababu Dictactor Nyerere hayupo madarakani.

Ndugu yangu umesema sawa, maana hata Kawawa alitoka mikoa ya Kaskazini na hakuwa wa dini ya Kiislamu. Ndiyo maana hakusaidia maendeleo ya mikoa ya Kusini. Pili, maendeleo yaliyoletwa na serikali ya awamu ya pili yaliharibiwa na na rais wa awamu ya tatu ambaye pamoja na kuwa alikuwa anatokea mikoa ya Kusini alikuwa na Udini na tena alioa kule mikoa ya Kaskazini. Tatu, rais wa awamu ya nne, Mh. JK, katika miaka mitano iliyopita ameleta maendelo makubwa kwa sababu yeye ni wa dini yetu na ni shemeji yetu. Nne, hata mwanzilishi wa mada hii kwamba mikoa ya kusini ni maskini si mkweli kwa sababu, watu wa mikoa hiyo sasa wana maisha bora na ndiyo maana wameikumbatia CCM.

Ukisoma maelezo haya changanya na ya kwako.
 
Watanzania wote ni maskini. Kuonekana nyuma kwa mikoa hiyo ni kutokana na tatizo la mbunge kuwa waziri hasa waziri wa fedha, waziri mkuu. Kwani DSM hakuna watu wanaoshangilia CCM baada ya kupewa khanga na sukari?
 
Over the years Dar and Mwanza have been solidly voting for CCM. Is Dar one of the poor regions? Mwanza?
I think you miss the point!
You can not deny the genuine love that the majority of Tanzanians have had on CCM.
 
Back
Top Bottom