Elections 2010 Kwa nini matokeo ya Uraisi hayakutangazwa majimboni?

Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
177,870
2,000
Mwanzoni NEC ilituahidi matokeo ya Uraisi yangelitangazwa Majimboni lakini baadaye NEC ikageuza utaratibu huo na kuamua yatumwe Dar-Es-Salaam ili wao wenyewe pale Dar ndiyo wayatangaze.........lengo lilikuwa ni nini?

Sasa NEC inatangaza Majimbo ambayo JK yadhaniwa kafanya vizuri ili kukwepa yale yaliyotokea Kenya ambayo muda wote Raila Odinga alikuwa anaongoza lakini mwishoni majimbo ya Mwai Kibaki yakaletwa mwishoni na kummaliza Raila.............

CCM wameishinikiza NEC ihakikishe ya kuwa hakuna hata wakati mmoja Dr. Slaa aonekane akimwongoza JK......

Tukio la Morogoro Mjini la kuchakachuliwa fomu ya Uraisi nalo limeleta mashaka makubwa ya kuwa huenda nchi nzima fomu za Uraisi zimechakachuliwa........haya matatizo yasingelikuwepo kama Majimboni matokeo yangelitangazwa moja kwa moja............

NEC inachofanya ni kuratibu hisia za matarajio ya wapigakura na hiyo siyo demokrasia hata kidogo.................

matokeo yangelitangazwa majimboni ya Uraisi yangeliyapa kukubalika zaidi kwa sababu ni rahisi kuhakikika na wapigakura lakini sasa kazi hiyo kufanywa na vyama vya siasa badala ya wahimili wakuu wa demokrasia ambao ni wapigakura............

Hizi ni njama za NEC kuhakikisha JK anarudi madarakani kwa kishindo........bila ya ridhaa ya mpigakura..................
 
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
352
170
Naona mwisho wa dhuruma hii ni mbaya. Siku 1 watajuta. Tusubir
 
J

joka

Member
20
0
..you have a point there.
hata kama yangetangazwa huko unakosema, bado slaa angepigwa kwani hajakubalika vijijini kama ilivyo mijini. Kwa hali hiyo hakuna cha uchakachuaji wala shangazi yake nini bali hali halisi ndo hiyo. Tusijaribu kuwaadaa watu wakati ni hivyo! Mbona pale majimbo anayoshinda au uraisi haujasema nao chadema mmechakachua matokeo. Naona hoja hiyo haina msingi kwani hapa bukoba mjini slaa kura za urais mbona kaongoza??? Jumlisha kila jimbo ulinganishe na tume ya uchaguzi utakuwa umejijibu mwenyewe. Tafadhali tuwe wakweli tofauti na kakobe kwamba kaota mrema anakuwa rais au slaa. Nawasilisha.
 

Forum statistics


Threads
1,424,514

Messages
35,065,584

Members
538,002
Top Bottom