Kwa nini Master J asiwajibishwe?

BISHOP

New Member
Feb 19, 2008
4
0
Master J ninaye muongelea ni huyu aliyekua eti Jaji wa Bongo Star Search iliyomalizika hivi karibuni na kushuhudiwa na mamia ya watanzani.Kwa bahati mbaya siku hiyo sikuweza kuhudhuria mpambano huo Live.

Baada ya siku kadhaa nilibahatika kuona marudio ya tukio hilo lililofanyika pale Ubungo Plaza ndani ya Blue Pearl Hotel.Katika mzunguuko wa mwisho wa wasanii husika nakumbuka kuna mwanadada mmoja alikua amevaa nguo yake ambayo kwa mimi binafsi ilinivutia tena sana.

Mwanadada aliimba kwa kadri ya uwezo wake wote na ikumbukwe kwamba siku hiyo ilikua fainali.Kimsingi ni kwamba shindano hili lilipitia ngazi(michujo) mbalimbali ili kupata wasanii bora.Naamini kulikua na washiriki zaidi ya miamoja lakini kutokana na mchujo mkali hatimaye walibakia washiriki watano ambao kwa hakika walistaili kuwa the best five.

Katika hao washiriki watano yumo pia huyo mwanadada ninaye mzungumzia.Naomba tukumbuke kwamba mchujo huo haukua wa siku moja bali ulikua wa safari ndefu ambapo wale tano bora wanastaili kupongezwa kwa hatua waliofikia.Majaji waliowafikisha wasanii hapo walipofikia katika TANO BORA ni hao hao akina Kitine,Salama Jabir,Master J na mama lao Rither.

Nije katika Comment za Majaji,baada ya yule mwanadada kumaliza kuimba.Comment ya master J alisema hivi,'mimi leo sijaona kitu zaidi ya mpasuo'Jamani mimi nauliza hivi Master J alikua sahihi kutoa kauli hiyo au tuite kuropoka.Kama wao ndio waliomfikisha hapo alipofikia hawaoni kama wamekula matapishi wao wenyewe?Mashindano yalilenga uimbaji na haikua shindano la mavazi,mimi nadhani kama lingekua suala la sauti au bits n.k hivi ndio vilikua vitu vya kuzingatia na sio suala la kusema fulani kavaa nini.Hapa kuna viashiria vya UMALAYA kwa jaji huyu.Huyu mama amekusea nini au kwa kuwa mlikua mmepanga matokeo.

Kitendo hiki mimi kimenikera tena sana na sidhani kama anafaa tena kuwa jaji wa mashindano haya.Basata wamfungie vinginevyo awasiliane na Lundenga.Naleta kwenu wadau sijui wenzangu mnasemaje.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom