Kwa nini mashirika yasomeshe watoto wa Kilimanjaro nje badala ya Pwani, Lindi, na Mtwara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini mashirika yasomeshe watoto wa Kilimanjaro nje badala ya Pwani, Lindi, na Mtwara?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by AridityIndex, Apr 18, 2011.

 1. A

  AridityIndex Senior Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimetafakari kwa kina juu ya suala hili sijapata jibu, naombeni kushare na wana JF wenzangu kulikoni katika hili. Nimepata kusoma katika makala nyingi sana hapa JF na kwingineko zikisisitiza kuwa katika mikoa hii ya pwani ikiwemo Lindi, Pwani na Mtwara ni mikoa ambayo iko nyuma kielimu kuliko mikoa mingine TZ. Tena makala hizo hazikuisha kutaja mikoa ya kanda ya kaskazini ukiwemo Kilimanjaro kuwa ni the best watu wamekula nondoz huko ni balaa na kila penye waTZ 10 wenye kazi nzuri basi 3 hadi 4 wametokea kilimanjaro. Yes wamesoma tena wamesoma vizuri hili halina ubishi, kwa nini wametutangulia watz wengine katika hili nadhani kila mtu anafahamu, na hiyo siyo hoja kwa thread hii.

  Maswali .

  Ni kwanini juhudi za kuelimisha watanzania zinaendelea kuelekezwa huko zaidi ya yale maeneo yaliyopo nyuma kama Lindi, Pwani na Mtwara?.

  Je kuna uhusiano kati ya watoa maamuzi yaani wale walioshika nafasi hivi sasa na uamuzi wanaoufanya wa kuelekeza rasilimali nyingi katika maeneo yao?

  Na je kwa haya maeneo ambayo kila mmoja wetu anakiri kuwa yapo nyuma kielimu yataendelezwaje iwapo wale walioko mbele bado wanaelekeza rasilimali zinazopatikana pamoja na miradi katika maeneo yao?.

  kampuni ya bia ya Afrika Mashariki (EABL)ni mfano mmojawapo tu lakini mambo haya yako sehemu nyingi TZ

  Jamani naomba ushauri wenu, hoja za msingi zitawafikia wabunge wa eneo hilo pia.

  unaweza kupata maelezo kutoka kwa kampuni ya bia ya Afrika Mashariki (EABL) juu ya mradi wa kusomesha nje watoto wa Kilimanjaro kwenye gazete la T/daima ya leo.
  http://http://www.freemedia.co.tz/da...i.php?id=29853
   
 2. b

  beko Senior Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35


  Aliye nacho huongezewa na yule asiyenacho hunyang'anywa kile kidogo na kupewa yule aliyenacho. this is how it is sorry for that
   
 3. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Jana niliona majibu mazuri tu sasa cjui unataka nini tena???
  Hata simba akipata mzoga hapeleki kwenye kundi la fisi, ujitosheleza wao kwanza then mabaki ndio ya fisi
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa silijui hilo ila nafikiri ni kwasababu na wao hawajiweki nyuma nyuma. Hata viongozi wao nahisi wanajibidiisha katika hilo.
  Viongozi wa pwani, lindi na nyie changamkeni sio mnalala lala tu. Lol!
   
Loading...