Kwa nini Marais wa E. Africa hawakuhudhuria Maadhimisho??

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Ndugu wana JF hadi sasa sijapata sababu maarum zilizo fanya majirani zetu hasa wale waliopo katika jumuia ya Afrika Mashariki wote kushindwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
Ndugu wana JF hadi sasa sijapata sababu maarum zilizo fanya majirani zetu hasa wale waliopo katika jumuia ya Afrika Mashariki wote kushindwa kuhudhulia Maazimisho ya Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Ni ishara tosha kwamba JK hapendwi hata na Mashost zake.
 
Labda hawajaona ligic ya miaka 50 ya Tanzania badala ya Tanganyika!!!
Itabaki kuwa changamoto kwa serikali na washirika wake.
 
na hiyo serikali inasemaje kuhusu hilo?au hawajaliona?hivi msemaji wao ni nani?
 
Waliogopa kulipukiwa na ile mizinga ya kizamani. Kwani hawana habari na yaliyotokea Gongolamboto?
 
Tusiwalaumu kwani inawezekana hawajui ni nchi gani imetimiza miaka 50 kwani Tanzania bado haijafikisha na Tanzania bara siyo nchi.Huu ni usanii wa kisiasa
 
Ndugu wana JF hadi sasa sijapata sababu maarum zilizo fanya majirani zetu hasa wale waliopo katika jumuia ya Afrika Mashariki wote kushindwa kuhudhulia Maazimisho ya Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Inawezekana hawajafafanuliwa vizuri wakaelewa na hawajawahi kusikia Tanzania ilipata uhuru mwaka gani, wao wanasoma kwenye History ya kuwa Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa mwingereza 1961, na Zanzibar 1963, na katikati kuna muungano 1964 ndio maana likazaliwa jina Tanzania, sasa wanajiuliza wanasheherekea uhuru wa Tanzania au muungano wa Tanzania. Sasa tunasubiri na Zanzibar nao watimize miaka 50 nayo yatangazwe maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru Tanzania. http://www.tanzania.go.tz
 
hii ni kulipizana kisasi. wengi walisusia kwenda Burundi kwenye ule mkutano wao hivi karibuni na hiyo itakuwa mwendo mdundo kwa nchi zetu kususiana!
 
Hiyo jumuiya yenyewe isha sambaratika. Haipo tena. Thus why hata Burundi jk hakwenda.
 
Ndugu wana JF hadi sasa sijapata sababu maarum zilizo fanya majirani zetu hasa wale waliopo katika jumuia ya Afrika Mashariki wote kushindwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
Mkuu, sababu maarum ni kuwa wanafahamu kuwa hata wasipokuja kwenye hizo sherehe hakuna watakachopoteza. Tanzania imeshapoteza hadhi yake kwenye jumuiya na wenzetu wameshaona kuwa hatuna influence yoyote
 
awkwarrrrd...! walikua wanaepusha awkward situation baada ya wikileaks papers kutoka. JK alikua anawasema vibaya wenzake kwa US. alisema Museveni ni dikteta anayetaka kutawala EA na yupo tayari kutumia maguvu kufanikisha azma yake, alisema Kibaki alichangia vurugu baada ya uchaguzi Kenya.
 
aa wenzetu walikuwa wanaendeleza mipango yao kushuhulikia thamani ya pesa zao hawakuona sababu za kuja kushinda na njaa uwanjani kuangalia farasi na mbwa wa police
 
Inaonesha wazi wamesusa. Sioni ajabu kwani huyu jamaa ajitia kujua sana wakati hana lolote. Baada ya miaka yake Tanzania itabidi ianze upya mahusiano yake na nchi hizi. Huyu jamaa anaona rafiki zake ni wazungu tu, hao hathubutu kuwaudhi.
Do, how things have changed! Tanzania ilikuwa ikikohoa tu viongozi wote wamefika. Ni nchi pekee iliyowahi kuwakutanisha Mugabe, Nkomo na Sithole siku moja!
 
je mabalozi wao au wawakilishi wengine walikuwepo?

huenda tishio la al-shabaab sio hadithi na vyombo vya usalama
vikashauri mkusanyiko mkubwa wa viongozi ungeweza kuwahamasisha hao
jamaa walete balaa.

pia huenda hawakualikwa
 
Back
Top Bottom