Kwa nini makinda aliirudisha ripoti iliyokuwa ikimchunguza jairo bila kujadiliwa na w | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini makinda aliirudisha ripoti iliyokuwa ikimchunguza jairo bila kujadiliwa na w

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ciril, Apr 25, 2012.

 1. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Wadau nna wasiwasi kuwa hapa tunataka kuja kupigwa changa la macho.Sheria ya marekebusho ya kupata katiba mpya ulijadiliwa Bungeni kwa maslahi ya taifa .Hii ripoti iliyokuwa ikimchunguza ndugu Jairo kwa nini spika Makinda aliiiamulia mwenyewe kuwa aliona kasoro zinazopaswa kwenda kurekebishwa?Maswali ya kujiuliza ni mengi
  •Kama aliona pana mapungugu kwa nini asiyataje hayo
  mapungufu tukayajua?Ni siri gani inafichwa hapa?

  •Wananchi tukihisi Spika na Serikali yake wanapanga ku-
  msafisha Jairo Kama ilivyo kawaida yenu ya kulindana
  tutakuwa tunakosea kweli?
  Yapo mengi yanatutia wasiwasi jinsi makinda anavyoendesha Bunge kwa kauli zake Kama"waziri jibu kwa kifupi/Swali lako ni jipya"na mengine Kama hayo.
  Nnaomba kuwasilisha hoja
   
 2. mgashi

  mgashi JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 304
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nashwindwa kuwaelewa hawa wwabunge, huyu ndo walipaswa waanze nae kutokuwa na imani nae. Haiwezekani bunge aliendeshe kama familia yake inatia uchungu sana.
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Haiwezekani ukapeleka kesi ya nyani kuamuliwa na ngedere ukategemea kushinda. Wote ni wadau wa madudu ya Jairo na kama yangeachwa yaendelee huenda yangeibua mambo mengi zaidi na ya kuianika serikali uchi wa nyama laini. Ni busara ya Makinda kuchelewesha mambo kwa kufunika kombe shetani apite. Hiyo ndiyo formula ya boso wake pia aliyemweka kwenye kiti hicho, yaana ahakikishe mambo yao yanalindwa vilivyo ama kwa kidictetor au kwa demorasia iliyopinda.

  Makinda yupo kwa ajili ya kulinda maslahi ya wakubwa na mitandao yao na kamwe usidhani analinda maslahi ya wananchi. Kama unadhani nabisha, tafakari hoja zote nzito dhidi ya wakubwa anavyozipangua kwa jeuri ya mamlaka aliyokalia kitini na hakuna wa kumsemesha zaidi. Mbaya zaidi ukiikomalia hoja inawezekana kibao kikageuka na wadau wake wakashupalia "Kudhalilishwa kijinsia" ili kukumaliza nguvu kabisa. Never ever ague with a woman!!!!! Amewekwa pale makusudi na kimkakati. Angalia sasa anasema hagombei 2015. ameshaona hapamfai pale, hata yeye mwenyewe amekalia kile kiti na anaungua masaburi pale alipo, Sitta alipaweza na ni kidume kwelikweli kiasi cha kuwafanya wadau wasilale kuhakikisha anaondoka akiwa kazibwa midomo yote.
   
 4. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hadi sasa nashindwa kuelewa kwa nini Wabunge hawakuja juu hapa. Yaani Makinda amepewa mamlaka ya kuhakiki ripoti kwa niaba ya Wabunge? Mie nilidhani Speaker ni "facilitator" katika Bunge, sio "Chief Executive Officer - CEO" wa wabunge anayeweza kuamua jambo linalojadiliwa kwa niaba ya Wabunge na bila kuwataarifu wabunge.

  Hili ni tatizo la taasisi nyingi Tanzania - wale wenye mamlaka wanafikiri wapo pale kwa kuwa wana akili kuliko wengine wote katika hiyo taasisi. Hata taasisi ya Ikulu ina tatizo hili - raisi kufikiri kiupotovu kwamba ana akili kuliko Watanzania wote anaowaongoza. Mawaziri ndio kabisaaa, wanajiona wamechaguliwa kwa kuwa wao ni ma-genius kulinganisha na wengine!!!
   
 5. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  si ndio wale wale magamba tu hawezi kuwa na la maana anawlinda wenzie maana kama majibu ya serikali yalikuwa shallow ingeongeza hasira za wabunge nafikiri wangepanda juu ya Meza.
   
Loading...