Kwa nini Mahakama za Tanzania zinaandika hukumu kwa Lugha ya Kigeni(Kingereza)? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Mahakama za Tanzania zinaandika hukumu kwa Lugha ya Kigeni(Kingereza)?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mwakalinga Y. R, Oct 31, 2012.

 1. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha kuwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru moja ya muhimili wa dola Mahakama inatumia lugha ya wakoloni (kingereza) kama lugha ya mawasiliano(kuandika hukumu) .Inashangaza kuona hukumu zinaandikwa kwa kingereza kwa kigezo kuwa lugha ya kisheria ni ya kitaalamu mno hivyo kuitafsiri kiswahili ni vigumu.

  Haitoshi, pale ambapo mtuhumiwa/msomewa hukumu haelewi kingereza basi Hakimu/Jaji anamwelewesha kwa kiswahili.Swali la kujiuliza Je, hayo maneno ya kumwelewesha msomewa hukumu kwa kiswahili yatoka wapi ? ama ni upotoshaji unatumika kwa makusudi kupindisha mambo?.Ama ni ufinyu wa bajeti !!?

  Mambo/maswali ya msingi ya kutafakari kwenye muhimili huu muhimu wa dola kwa miaka zaidi ya 50
  1.Mahakama zipo kuwahudumia kina nani?
  2.Wanaohudumiwa wanajua lugha gani kwa ufasaha?

  Napenda kujua zaidi ya kidogo nachojua ,hivyo naomba kueleweshwa kulingana na mada.

  Nawasilisha
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,221
  Trophy Points: 280
  madaktari wanaandika lugha gani?
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nikauliza ili nijuzwe kutokana na uwela wangu mdogo. Sasa naona na wewe unaniuliza swali tena ,Watanzania bwana!!
  Shukrani kwa mchango wako
   
 4. n

  nlambaa JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kutokana na sheria ambayo imesema kuwa hukumu kuanzia mahakama za wilaya na kuendelea ziandikwe kwa kiingereza, kwa upande wa mahakama za mwanzo hukumu zinzandikwa kwa kiswahili. Hata hivyo nafikiri ni wakati muuafaka kubadilisha sheria na iwe kama shauri limeendeshwa kwa kiswahili basi kuanzia mwenendo wake na hukumu viandikwe kwa kiswahili pia, nafikiri itakuwa bora sana maana sheria hizi tuli rithi toka kwa wakoloni na sasa hizi hatuna majaji na mahakimu ambao ni wazungu au wahindi.
   
 5. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hapo ni sawa ,naungana nawe kwa 100% . Tumekuwa watumwa wa fikra kwa muda mrefu bila kujua kipi ni sahihi kwa wakiti gani na kwa hadhira ipi.
   
Loading...