Kwa nini maduka yetu mjini yafungwe saa 11 au 12??

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Katika jiji kama hili la DSM nashangaa sana kuona bado hatujaweza kuwa na mfumo wa kuwa na maduka yetu kufanyakazi hadi angalau saa 4 usiku. Inakuwaje main shoping area inayojulikana sana hata kwa majirani zetu KARIAKOO maduka yafungwe mapema vile.

Ule muda wa jionina usiku ni muhimu kwa wale ambao kutwa nzima kutokana na shughuli mbalimbali hawawezi kupata muda mchana kufanya shoping. Hivyo jioni ni muda muafaka kwao. Kuna wengine wanapenda kutoka na familia zao kwenda kufanya shopping na ni muda mzuri kwa watoto pia kwani hakuna msongamano na joto.

Wengine kama mimi ule msongamano na kelele zinanipunguzia appetite ya kutafuta vitu. Tukiongeza muda wa biashara tutapunguza pia msongamano mchana kwani tutakuwa tunapishana wengine wanatoka wengine wanaingia. Mataifa mengi sehemu kama hizo ni 24 hrs.

Tuanze sasa maana hakuna sababu ya wafanyakazi kusubiri Jumamosi kufanya shopping wakati wanatokea hukohuko kila siku.
Karibu kwa mawazo, a project begins with an idea.
 
Wazo zuri isipokuwa usalama ndio janga la taifa.
Pili hao wafanyabiashara kila mtu anataka afanye kila kitu na awepo mda anaomudu yeye.
Kwani kama wangebadilishana shift sawa lakini uaminifu upo?
Kweli wanaweza ila inataka guarantee ya usalama wa wafanyabiashara kutoka serikalini au CCTV ziwepo kila mahali.
Ni wazo zuri ila inataka muangalizo mpana.
 
Katika jiji kama hili la DSM nashangaa sana kuona bado hatujaweza kuwa na mfumo wa kuwa na maduka yetu kufanyakazi hadi angalau saa 4 usiku. Inakuwaje main shoping area inayojulikana sana hata kwa majirani zetu KARIAKOO maduka yafungwe mapema vile. Ule muda wa jionina usiku ni muhimu kwa wale ambao kutwa nzima kutokana na shughuli mbalimbali hawawezi kupata muda mchana kufanya shoping. Hivyo jioni ni muda muafaka kwao. Kuna wengine wanapenda kutoka na familia zao kwenda kufanya shopping na ni muda mzuri kwa watoto pia kwani hakuna msongamano na joto.Wengine kama mimi ule msongamano na kelele zinanipunguzia appetite ya kutafuta vitu. Tukiongeza muda wa biashara tutapunguza pia msongamano mchana kwani tutakuwa tunapishana wengine wanatoka wengine wanaingia. Mataifa mengi sehemu kama hizo ni 24 hrs. Tuanze sasa maana hakuna sababu ya wafanyakazi kusubiri Jumamosi kufanya shopping wakati wanatokea hukohuko kila siku.
Karibu kwa mawazo, a project begins with an idea.
bado hatujawa wakali kiusalama mkuu
 
Siamini kama ni usalama au ndio mtindo wa maisha tuliouzoea. Ki ukweli tukiimarisha matumizi ya ki electronic katika biashara, tatizo la ujambazi wa kupora fedha utapungua sana, na tunaweza sasa kufanya biashara kwa masaa zaidi angalau kwa kuanzia mpaka saa 2 usiku.
 
sehemu nyingi za kiarabu maduka yanafunguliwa saa saba mchana mengi mpaka saa nne usiku
inakuwa watu waamerudi kazini na wamepumzika wanatoka shopping ni pangependeza sana
 
wazo zuri lakini usalama ndio tatizo maana hao askari wenyewe wa shfti za usiku hua hawalindi hutafuta sehemu na kula pozi kusubiri simu za uharifu na sio simu zote hua wanaenda!
 
hapa intakiwa tuimarishe matumizi ya malipo kielecronic au banks nazo zichelewe kufungwa
 
Umetumwa na majambazi.
Sio bure.
Pale kariakoo kuna maduka yanaingiza mpaka mil 10 kwa siku
Afunge duka SAA 4 usiku hajitaki?
 
majambazi wanashirikiana na polis,polis wetu wengi bado siobwaaminifu wanajulengesha kwa majambazi na siku utakayoibiwa a kuuwawa kabisa watafika baada ya Masaa matatu
 
Hoja nzuri sana hii mkuu, kubwa hapa tu mazoea pamoja na mfumo wa ajira ambao tumekua nao tangu enzi zile. Kwani kuongeza muda vile kuna implications kwenye posho na benefits mbalimbali za watumishi katika maduka husika. Kubwa hapa ni kwamba serikali ya jiji la dar ikiamua hakuna linaloshindikana.
 
Umetumwa na majambazi.
Sio bure.
Pale kariakoo kuna maduka yanaingiza mpaka mil 10 kwa siku
Afunge duka SAA 4 usiku hajitaki?
Technology inajibu swali lako. Pole bado uko dunia nyingine.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom