Kwa nini maduka yetu mjini yafungwe saa 11 au 12??

Katika jiji kama hili la DSM nashangaa sana kuona bado hatujaweza kuwa na mfumo wa kuwa na maduka yetu kufanyakazi hadi angalau saa 4 usiku. Inakuwaje main shoping area inayojulikana sana hata kwa majirani zetu KARIAKOO maduka yafungwe mapema vile.

Ule muda wa jionina usiku ni muhimu kwa wale ambao kutwa nzima kutokana na shughuli mbalimbali hawawezi kupata muda mchana kufanya shoping. Hivyo jioni ni muda muafaka kwao. Kuna wengine wanapenda kutoka na familia zao kwenda kufanya shopping na ni muda mzuri kwa watoto pia kwani hakuna msongamano na joto.

Wengine kama mimi ule msongamano na kelele zinanipunguzia appetite ya kutafuta vitu. Tukiongeza muda wa biashara tutapunguza pia msongamano mchana kwani tutakuwa tunapishana wengine wanatoka wengine wanaingia. Mataifa mengi sehemu kama hizo ni 24 hrs.

Tuanze sasa maana hakuna sababu ya wafanyakazi kusubiri Jumamosi kufanya shopping wakati wanatokea hukohuko kila siku.
Karibu kwa mawazo, a project begins with an idea.[/Q
PUNGUZENI AU ACHENI KABISA WIZI MADUKA YATAKUWA WAZI MPAKA USIKU
 
Hili wazo lako liweze kutekelezeka ni ueleze mbinu itakayotumika katika kuhakikisha usalama wa wateja na wafanyabiashara kwa ujumla.

La sivyo wazo lako halitekelezeki.
 
Safety and security purposes. Ila kwa sehemu kama Mlimani city au Shamo complex au Kibo komplex Au Qulity plaza na centre inawezekana ila sahau kuhusu kko
 
Back
Top Bottom