Kwa nini lowasa na rostam hawapelekwi mahakamani?

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Kama ushahidi wa kamati ya bunge unatosha kufungua kesi ya jinai kwa nini DPP asiwapeleke lowasa na wenzake mahakamani mapema ili tusiingize mafisadi ikulu? Heri jipu lipasuke sasa kuliko baada ya uchaguzi! Dr Slaa alichoeleza kinatosha kwa jinai ya matumizi mabaya ya madaraka na utapeli na kuitia serikali hasara. Kama ikulu haihusiki kigugumizi cha nini. Dowans ni mzigo usiostahili kulipwa na walipa kodi.
 
Hawatapelekwa maana wazee wa KIWIRA na Richmond wanajulikana sana hivyo amani ya nchi itavurugika.
Kwa nini Mwakyembe alificha kipande cha karatasi wakati wa kusoma habari za Richmond?
 
Mpenda Mhashamu Askofu wa jimbo langu, nakuaminia kwa uadilifu wako. Naamini wewe na Kardinali Pengo ni miongoni mwa wale maskofu wanne ambao mmemkataa kuhongwa na huyu msaka urais. Basi nakusihi sana sema neno ili sisi kondoo wako tuendelee kuimarika. La kama nawe umechukua na ulishazitumia tayari, basi tuambie tuchange tumrudishie fisadi pesa yake maana tumefedheheshwa sana.
 
Back
Top Bottom