Kwa nini kuapisha Mawaziri wa Serikali ya Rais Kikwete inakuwa sherehe ya kukata na shoka?

fundimchundo

JF-Expert Member
Jul 23, 2010
616
904
Kuwa Waziri au Naibu Waziri ni kazi ngumu inayohitaji umakini na massa mengi ya kufanya kazi.
Mtu anapoteuliwa kufanya kazi hiyo, anatakiwa ajue kuwa anatwishwa mzigo mkubwa.
Hali hiyo siyo ya kufanyia sherehe hata kidogo.
Kinyume chake, kazi ya kuwaapisha wateule wote wa Rais Kikwete imegeuzwa kuwa sherehe ya kukata na shoka kuanzia Ikulu kwenyewe ambako hupambwa kwa gharama kubwa sana na kumalizia nyumbani kwa wateule ambako ng'ombe kadhaa huchinjwa.
Maadamu uteuzi ni tukio la kula sana na kunywa sana, kwa nini tunashangazwa na ripoti za CAG za utendaji wa wateule hawa?
Wakati wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mawaziri walikuwa wanaapishwa mbele ya meza ya mbao za mninga, bila wake na watoto wa wateuliwa kuwepo.
 
Back
Top Bottom