Korea ya kaskazini imekuwa ikichukuliwa kama taifa korofi, kandamizi kwa raia wake na lisilotii sheria za kimataifa hususani zile zinazohusisha umiliki silaha na urutubishaji wa nyukilia, ambacho ndio kiini cha mgogoro unaofukuta baini yake na Marekani. Swali la msingi ni Kwa nini taifa dogo lenye idadi ya watu takribani million ishirini na tano na pato la taifa linalokadiliwa kuwa dolla za Marekani billion 40 tu liwekeze kwa kiwango kikubwa namna katika jeshi na umiliki silaha za nyukilia? Jibu ni kwamba uwepo wake unategemea na utategemea uhimara na nguvu zake za kijeshi, nguvu zinazoendana ama kukaribiana a adui wake.
Kwa kiwango kikubwa mwenendo na sera za serikali ya Korea ya Kaskazini ina akisi matukio ya kisiasa na histori katika rasi ya Korea tangu karne ya ishirini. Ikumbukwe kuwa kati ya miaka ya 1910 mpaka 1945 rasi ya Korea ilikuwa chini ya ukoloni wa Japani. Katika kipindi hiki, wakorea, haswa wale wenye kufuata itikadi za kijamaa, walikuwa wakiendesha harakati za kujikomboa dhidi ya mkoloni Japani kwa mbinu za vita ya mstituni (guerrilla war).
Mwaka 1945, Urusi ikatangaza vita dhidi ya Japani na kufanikiwa kushinda hivyo kumuondoa Japani katika rasi ya Korea. Baada ya Japani kuondoka, Uruisi na Marekani, waliokuwa washirika, katika vita kuu ya pili, wakakubaliana kuigawa Korea, kaskazini ikikawa chini ya Urusi huku kusini ikiwa chini ya Marekani.
Mwaka 1947, umoja wa mataifa ukaelekeza kufanyika uchaguzi Korea lakini Urusi ikaususia kwa kuwa waangalizi wa uchaguzi walikuwa washirika wa Marekani, ambayoilionekana kuwapa upendeleo viongozi wa Korea ambao walishirikiana na utawala wa kikoloi wa Kijapani dhidi ya Kim Il-Sung ambaye aliongoza harakati za ukombozi dhidi ya Japani kwa kuwa alifuata itikadi za kijamaa. Hatua hii ikapekea Korea kutegana moja kwa moja. Serikali mbili zikaundwa, Democratic People's Republic of Korea ikitawala sehemu ya kazikazini na Repubic of Korea ikitawala sehemu ya kusini huku serkali zote zikidai kuwa ndio watawala halali wa Korea nzima.
Mwaka 1950, mvutano baini ya serikali hizi ukapelrkea kuzuka kwa vita ya Korea baada ya majeshi ya kaskazini kuvamia kusini katika harakati ya kuunganisha nchi chini ya utawala mmoja. Marekani, katika sura ya umoja wa mataifa, akaingia kumsaidia mshirika wake, Korea ya Kusini, aliyekuwa analekea kushindwa. Kufuatia kampeni kubwa ya kijeshi na mfululizo wa mabomu, Marekani akafanikiwa kumrudisha Korea ya Kaskazini mpaka pale Uchina alipoingia upande wa Korea ya kaskazini.
1953, makubaliano ya kusitisha mapigano yakafikiwa yakizitaka serikali za Korea ya kusini, Korea ya kasikazini, Uchina na Marekani kuendelea na mazungumzo ya kutafuta amani. Haakujawa na makubaliano ya kumaliza vita na hivyo, richa ya mapigano kusitishwa, nchi hizi mbili bado ziko vitani. Baada ya kusimamishwa kwa mapigano Marekani ikazidi kujiimarisha kijeshi katika rasi ya Korea kwa kuweka vituo vya kijeshi na kupleka silaha nzito. Kwa upande wake Korea ya kaskazini, ikajiweka chini ya ulinzi wa Urusi na Uchina huku ikichukua ser sys jeshi kwanza sera amabayo inalipa jeshi kipaumbele katika mgawanyo wa raslimalimili kuimarisha jeshi lake na uwekezaji katika kutengeza silaha kujilinda dhidi ya Marekani.
Mgogoro wa sasa umejikita katika kukuwa kwa uwezo wa kivita na uwezo wa kutengeneza silaa wa Korea ya Kaskazini. Tishio linaweza lisiwe Korea ya Kaskazini kutengeneza makombora yenye uwezo kufika marekani, bali hatari ya kuungana kwa Korea kama nchi moja. Serikali zote mbili za korea zimekuwa na ajenda ya kutafuta namna ya kuunganinisha eneo lote la rasi ya Korea chini ya serikali moja. Mwaka 1972 Serikali zote mbili za Korea zilitoa tamko la pamoja la hatua zitakazo chukuliwa kufikia kuungana tena kwa amani na kufuatiwa na tamko jingingine kama hilo mwaka 2000. Hata hivyo, changamoto kubwa katika maazimio hayo imekuwa ni tofauti za kiuchumi na siasa baini ya Korea ya Kaskazini na Kusini na kwa upande mwingine, masilahi ya mataifa ya kigeni.