Kwa nini kodi ya leseni ni kwa madereva tu!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Kwa muda nimeliwaza hili nimeona leo niliongelee.

Binafsi huwa nashangaa serikali yetu kung'ang'ania vyanzo vilevile vya mapato miaka nenda miaka rudi. Kwa mfano utakuta kila mwaka hayo ma road toll na madudu mengine kama sigara na vileo vikiongezwa kodi kila uchao.

Kuna hili la madereva kutakiwa kulipia kodi leseni zao za udereva, pia ni la kuangaliwa. Sheria zilizopo zinamtaka raia wa TZ awe anamiliki au hamiliki gari, lazima atatakiwa alipie leseni yake ya udereva. Hebu angalia hapa, kazi ya kawaida sana ambayo haihitaji elimu hata ya chuo kikuu, mtu utatakiwa ulipie mapato leseni yake. Pesa inayopatikana kutoka vyanzo hivi si haba.

Hata hivyo huwa najiuliza: mbona kuna fani nyingi sana za maana ambazo kama serikali ingekuwa serious isingehitaji kukimbizana na raia masikini kupata mapato? Jaribu kufikiria hili: Tanzania kuna makandarasi wengi, madaktari, wanasheria, wataalamu wa mazingira, walimu, madaktari, wahasibu (CPA holders) nk. Kama kweli serikali inataka kuboresha mapato yake, haioni kuna haja ya hawa wataalamu nao wawe wanalipia kodi leseni zao wanazomiliki? Chukulia mfano, hao wote niliowataja wakiwa wanalipia professional lisence zao ni kiasi gani cha pesa serikali ingekuwa inapata kila mwaka wa fedha? Bila shaka ni pesa nyingi sana. Ungewekwa utaratibu wa ukaguzi kuhakikisha wahusika wanalipia mapato kila mwaka.

Lakini kama kawaida, kutokana na ufinyu wa kuwaza wameendelea kung'ang'ana old sources ambazo kwa kiasi kikubwa zimeshindwa kuboresha mapato ya ndani.

Hata hivyo haya ni maoni yangu tu, maana huwa naboreka kuona gharama za kuendesha nchi hii imeachwa mikononi mwa walalahoi ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wanaodharauliwa sana na watawala wachache tuliowapa madaraka ya kuiongoza nchi hii.

Ni mtazamo tu, tusijenge chuki wakuu!

CIAO!!!!!!!!!
 
Wengi wa hao uliowataja wanalipa aina fulani ya tozo kuhusiana na leseni zao. Kwamba pesa hizo zinaenda serikali kuu au zinagharamia taasisi husika za utoaji leseni/usajili hilo sina uhakika.
 
Wengi wa hao uliowataja wanalipa aina fulani ya tozo kuhusiana na leseni zao kwamba pesa hizo zinaenda serikali kuu au zinagharamia taasisi husika za utoaji leseni/usajili hilo sina uhakika.

thanx for your updates!
 
Back
Top Bottom