Kwa nini Kiswahili kisitumike kwa ngazi zote za elimu

Upumbavu huo futa kichwani.

Nchi yako ingekua imevumbua teknologia hata moja ya maana unayoitumia hadi sasa ndio ungesema maneno hayo.
WaTanzania wenye vipaji vya kugundua teknolojia wapo wengi sana na kila siku wanagundua. Tatizo ni uwekezaji katika wabunifu wa ndani na pia mfumo wa elimu sio rafiki.
 
Bado hatujaendelea kufikia kiwango hicho cha kutumia lugha yetu wenyewe nazungumzia wataalamu mbali mbali hatujajitosheleza,... Vitabu na waandishi wake, pili kutumia kiswahili tutaji limit kutafuta ajira kwa nchi zinazotumia kiswahili tu... Tatu nchi yetu bado ni tegemezi kwa kiasi kikubwa angalia nchi ulizozitaja.... kama "Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Sweden, Norway, Denmark, Finland, China, Japan, Korea kusini" Hakuna hata nchi moja tunayolingana nayo......
Hatujaendelea kwa kuwa wasomi wetu wengi wanakariri. Nchi zilizokuwa na uthubutu wa kurekebisha elimu pamoja na lugha ya kufundishia ndio wameendelea. Je nchi kama Korea ya kusini , Japan na China wamefanikiwaje?

Ishu ya ajira nje ya nchi kuwa itasumbua kwa kiswahili naona sio sahihi? Je kwa sasa ajira zipo (wanasiasa wanasingizia watu wajiajiri) na ajira za nje ya nchi zipo kweli? Je wachina waliojaa Tanzania wakijenga barabara, majengo, viwanda na madaraja wanajua kiingereza?
Lugha ni muhimu ila sisi tunaidharau, cha muhimu ni kuelewa na sio kukariri.
 
Kama unasema tuanze kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia kwa ngazi zote kwa sasa inawezekana lakini inahitaji juhudi kubwa .

Pia tunahitaji kuwa na wataalamu wa fani zote ambao watafanya kazi ya kutafsiri vitabu vya fani hizo,maana fani zimekitangulia kiswahili.

Na muhimu zaidi ni wataalamu wa kiswahili chenyewe ambao watakuja na misamiati mipya ambayo itatumika katika kutafsiri vitabu hivyo.

Na hizo nchi ulizozitaja ni nchi zilizo endelea na sisi ni nchi.........

So jambo hilo linahitaji wasaa na sio kukurupuka tu,na tunamengi ya kufanya katika maendeleo makubwa zaidi ya kushughulikia kiswahili.

So endelea tu kumeza vitini.


Sent using Jamii Forums mobile app

Bado tuna shida katika lugha ya kufundishia.

Ngoja nikameze vitini tu.
 
Lugha hukua kadri inavyotumika.
Je nchi zingine zilizoendelea wanatumia lugha zipi?
Upo sawa na nchi zinazotumia Kiswahili zitakapokuwa zimejiendeleza kiteknolojia uwezekano wa kutumia Kiswahili kwenye masuala ya teknolojia utakuwa mkubwa.Nchi nyingi zinazoendelea zinatumia Kiingereza,Kifaransa, Kispaniola,Kireno nk(kutegemea mkoloni wake).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna technology
China anayo
USA anayo
Wote wanao tumia lugha zao wanayo
well sijaelewa hasa nini mausiano ya lugha na technologia let view USA before colonial Even though English is the dominant language in the United States, the first permanent English settlement came 42 years after explorers from Spain founded St. Augustine in Florida. Their primary language was Spanish. "Spanish was the first European language spoken in this country."Nov 7, 2016....Apa Tz we have a lot of graduate ambao wameielewa vizuri tu iyo lugha ya kikoloni na pia kupata GPA kubwa sana , where are they! but still we HAVE zero creativity and innovation sasa iyo technology itatoka wapi? atatungefundishwa kwa lugha za makabila yetu still tatizo litakua palepale if creativity and innovation is not our desire tutabaki kumtafutamchawi daily
 
Kuna coaz zngine kiswahil huwez tumia mfano medicine au wanaosoma mathematics
Ni kwa nini Tanzania tusingesoma kwa kiswahili kuanzia vidudu mpaka PHD?

Nipo nameza vitini hapa hata kichwani haviingi.

Hivi nchi zingine zilizoendelea kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Sweden, Norway, Denmark, Finland, China, Japan, Korea kusini wanasoma kwa lugha gani?

Naona kama tunavyosoma kwa kiingereza tunasomea mitihani tu, halafu kichwani ni chenga.

Mimi bado ni kijana mdogo sana na akili yangu ni ndogo. Natamani nifahamu hilo hasa kwa waliopanda pipa huko majuu na kulinganisha elimu na maendeleo ya nchi husika.


Ngoja niendelee kumeza vitini wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom