Kwa nini KIMEI wa CRDB anataka awe GAVANA wa Benki Kuu? ANAFAA au HAFAI?

chinga

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
312
9
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vinasema Charles Kimei halali kusaka ugavana wa benki kuu ikiwa kununua waandishi wa habari ili kila leo aonekane wakati mwingine kwenye shughuli zisizokuwa na kichwa wala miguu atahakikisha anapata coverage ya kutosha.

na amekuwa akiona JK anakwenda mahala atahakikisha kuna watu wake wa CRDB.
safari za U.K za JK za hivi karibuni huyu bwana alipeleka watu wake hakukuwa na sababu ya kuja mara mbili ila ndio jamaa yuko kwenye kampeni.

na tunawasisi na phd yake ni zile kundi la kina David Mathayo, DR.kamala,DR.Warioba wa Mzumbe University, Mary Nagu na augustino Mrema.
 
Chinga

Wellcome back Chinga, Its a long time and we value your contributions although controversial.
 
Mheshimiwa Chinga.
karibu mkuu tunaliendeleza jahazi letu. kitu hicho ulichosema kina ukweli kiasi kikubwa huyu bwana KIMEI amekuwa na pilikapilika nyingi na kuvitumia vyombo vya habari vya wana kaskazini kujitangaza sana.

na muda si mrefu alifungua tawi la CRDB kijijini KIWANGWA-Chalinze kwa muungwana JK, nadhani hiyo yote katika kujipalilia mbolea. lakini Kiwangwa kuna mahitaji mengi ya msingi ambayo angeweza kuwasaidia hasa huduma za jamii. nitaendelea kutoa data kadri muda unavyokwenda.
 
Lakini huyu jamaa ni kama amefanya kazi nzuri sana CRDB. Kama ana uwezo
na sifa kwanini iwe taabu kama anataka kuwa gavana?

Mimi simjui ila kwa TZ nachukulia ubinaifishaji wa CRDB kama mfano mzuri ambao ungeigwa kwenye mashirika mengine.

Kama ana matatizo mengine basi yamwageni.
 
knkcu

hii mada aliiongelea mswahili kule kwenye mada ya ukabila ....kuwa majina ya huyu jamaa na dau yamepelekwa kwa muungwana..na tena hata ile kashfa ya nssf na manji[magodown na majumba waliyonunua nssf kwa kama billion 80]
ni sehemu ya kupakana matope kugombea ugavana.....so mswahili akawasiliana na chinga na wengine kuleta thread ya kumchafua kimei.....]

mimi nitakuwa observer pale nitakapopata wasaa.....kateni ishu.
 
basi nadhani apangiwe assasination hili lijizi kabla halijafanikiwa !!

.......it leaves a bad taste indeed! This is blind hatred, and it must stop.

It is becoming apparent that there are dedicated 'haters' among us; as evidenced by their line of arguments not only here, but in several related discussion threads. This type of contribution of ideas will not take Tanzania any one step ahead in development.
 
Phillimon mikael.

mbona unanifuatafuata bila sababu? kama umeshindwa hoja nyamaza tu.

naomba acha uongo zee zima linakuwa kila dakika linaongopa tu.

NAOMBA NIONESHE WAPI NILIANDIKA KUWA KUNA MAJINA YAMEKWENDA KWA MUUNGWANA NIKAMTAJA KIMEI KWENYE MADA YA UKABILA? KAMA KUNA KITU HICHO UKITHIBITISHA HAPA BASI MIMI SINTOENDELEA KUSHIRIKI HUMU KWANI NITAKUWA NIMEDANGANYA.

NIMELAZIMIKA KUANDIKA KWA HERUFI KUBWA KUTOKANA NA MATATIZO YAKO YA KUTIZAMA MADA KIMAKENGEZA.

NAOMBA NIONESHE WAPI NIMEWASILIANA NA CHINGA AFUNGUE THREAD YA KIMEI?

kwanini unaishi kwa chuki na uongo kila dakika? mimi nina data za TRA huko Ikulu kwa Muungwana unazijua wewe.

naomba unikome kunizushia kila jambo baya nimekukosea nini? au Chinga kufungua thread ya kumfanananisha MBOWE NA CHIFUPA mnaona nae anachuki wachagga?

wanabodi.

mfuatilieni Phillimon Mikael ananinyanyasa bila sababu.basi lipueni na computer yangu kama mlivyochoma nyumba ya Benny LUSEGE WA TRA.
 
.......it leaves a bad taste indeed! This is blind hatred, and it must stop.

It is becoming apparent that there are dedicated 'haters' among us; as evidenced by their line of arguments not only here, but in several related discussion threads. This type of contribution of ideas will not take Tanzania any one step ahead in development.


i know i shouldnt have said assasination, but if u look at the matter closely unaweza ukaniambia ni njia gani ya kuwahukumu hii mijambazi ? au kwa kuwa wema tuliokuwa nao ndio utufanye tuwe mazezeta, viongozi wanakula halafu hapo hapo hauna means ya kuwahukumu, assasinate one of them god damn cruels and see kama watadhubuti kuendelea kula rushwa ! ndio maana tz tumekuwa wanyonge kiasi kwamba watu wengine wanadhani sie ( raia ) ni wajinga ! tunapenda sana kujitetea hasa tukiwa huku nje ya nchi kwa wengine kwamba kwetu kuna amani, viongozi wazuri just because wanapokezana madaraka lakini tukitoka hapo tunakuja JF halafu na kuanza kupaka ! That dont make sense, au ndio zile za "no matter if u r wrong or right u r still right "! jamani tuangalieni sana hasa hapa kuwasifia viongozi wasipostahili hizo sifa mnawapa vichwa na wao wanaona wanachokifanya ni poa kumbe utumbo !
no hatred intended but sometimes u have to do what u have to do, and sometimes u might have to take a life to saves the MANY LIVES ya mabibi zetu wanaoishi vijijini kusikokuwa na maji huku akina Lowassa wanaiba pesa na kula maraha katika mahoteli eksipensivu halafu hapo hapo tunachekelea, ujinga gani tuliokuwa nao ! Mimi na wewe tunaweza tusilalamike na sidhani kama mtu yeyote humu JF anatakiwa kulalamika ukilinganisha maisha yetu wanaJF na hao wanaoisi vijijini, wengine u cant even believe the conditions they live in, halafu anatokea lowassa anaenda kuomba mvua mexico hata wao wenyewe hawajawahi kuitumia anataka akateketeze watu tz, elimu hana bali kajaa tu uropokaji, na maamuzi yasio na maana ! I Wonder why muungwana bado anamuacha madarakani.

Nimejaribu kuweka picha hapa kuonyesha wazee, vijana, watoto wanaoishi tz vijijini lakini nimeshindwa, wana matatizo kibao na misaada inatolewa kila leo lakini haifiki kutokanan na kuliwa kwa wachache walio na opportunity ! ndio maana nasema atengenezwe mmoja wao halafu tuone wengine wata-react vp ? Muungwana upo ?
 
JF tunaweza kufikiri kuliko hapa tulipofikia.

Chinga nadhani unaweza kuandika vizuri zaidi ya kiwango hiki.

Naomba tuwe na tabia ya kumjadili mtu kuendana na utendaji kazi wake na siyo habari za mtaani ambazo zinaweza kuwa na mantiki tofauti kabisa na utendaji wa mtu.

Ni muda nimeona watu wanasema mambo bila kukaa na kuchambua habari yenyewe. tulianza vizuri na tunachangia vizuri lakini naona tunaanza kuwa "obsessed" kuandika habari hapa JF. Tunaandika bila kuangalia habari tunazoandika.

Turudi kwenye hoja

1. Kuteuliwa au kutoteuliwa kwa mtu kuwa Gavana, hakutokani na habari za magazetini au kuhudhuria vikao vya rais bali hutokana na utendaji wa mtu na matarajio ya anayeteua. Kwa maneno mengine mtu mwenye akili makini na anayetaka kuteuliwa na mteuaji hawezi kwenda kujitangaza kwenye magazeti bali atafanya kazi kwa vitendo na kuonesha matunda ya kazi yake. Vile vile nitamwona mteuaji kuwa mwendawazimu kama atateua mtu kwa kuzingatia sifa au dharau za magazetini au kwenye makongamano.

2.
Tujiulize je tangia CRDB ibinafsishe imebadilika au la na kama imebadilika imeleta mafikio au hasara?

3. Kwa mantiki yangu na ya watanzania, ni kwamba CRDB imepiga hatua mbele kuliko benki nyingi Tanzania hata unapolinganisha na za kigeni. CRDB ni benki ambayo ni ya kwanza Tanzania kuunganisha matawi yake kwa kutumia mfumo wa kisasa ambao ulifanya watu kutuma pesa papo kwa papo na kuchukua pesa kwenye Tawi lolote nchini bila usumbufu. CRDB ni benki ya kwanza kuanzisha huduma ya malipo kwa Kadi. Ni benki ya kwanza kuwajali watanzania waishio nje ya nchi kwa kuwafungulia akaunti ya TANZANITE (ijapokuwa ina mapungufu bado)

4. Je ni benki gani Tanzania ambayo inaongozwa na mtanzania ni kuwa na mafanikio makubwa katika riba na huduma kwa jamii (mikopo).

Swala la kujiuliza mafanikio haya yaliletwa wakati gani na ni nani alikuwa Meneja wa Benki hiyo.

Ni lazima tuweze kuweka swala la ukabila na dini pembeni na kujadili mafanikio na mapungufu ya mtu au Taasisi katika utendaji kazi yake.

Tusiseme ovyo kama kipindi fulani kule BCS Times watu waliposema Mengi anadaiwa bilioni tano na TRA na kesi ipo mahakani, lakini tumesubiri mpaka leo hatujaona ushahidi, bali watu wanakuja na hoja eti kisa ni mchagga hawezi kushitakiwa.

Kama kweli tunahitaji mabadiliko ya kweli kwa Tanzania yetu hatuna budi kuanza kuangalia hoja kwa miwani ya kweli na siyo polarized.
 
AL-JAZEERA.

umesema mambo ya ukabila na udini yawekwe pembeni kwani kwenye hii mada umezungumzwa udini au ukabila? mbona mnatutisha? ina maana Kinana. Ditopile, JK mnawajadili humu kwa sababu za dini na kabila zao? mnatufungua macho.
KUHUSU suala la magazeti sio kweli lazima habari za magazeti tuzisikilize. wewe hukuona habari za Lowassa kuwa waziri mkuu kwenye magazeti yote? hukumsikia Salva rweyemamu na B.B.C? na si kweli akawa waziri mkuu?

hujasoma juzi juzi kuwa Membe atakuwa waziri wa mambo ya nje? hata kuna mwanabodi aliandika humu. mbona yote yamekuwa?

kama KIMEI mtendaji kwanini anunue magazeti ?

kama watu wana wasiwasi na phd yake kwanini nyie mkasirike? mbona hamkukasirika kumuumbua marehemu ramadhani Kihiyo kuwa ana cheti za uongo? basi na wenye phd za uongo tuwaite VIMEI na akiwa mmoja ni KIMEI kwani phd yake ina mashaka makubwa.
 
AL-JAZEERA.

HIYO TANZANITE account ni utapeli hamna kitu.acha kudanganya watu.
nakupa mfano mdogo tu Uganda kulikuwa na benki tena binafsi ikiitwa Green land bank iliweza kufungua matawi Tanzania.

na kuna bank ya kenya hapa Tanzania. naomba tawi la CRDB nje ya nchi? au kwenye briefcase ya innocent Mungy? nae kamuachia kinemo.
 
Kikwete awateua mawaziri wapya

na Hellen Ngoromera

HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete ametangaza rasmi mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kuziba nafasi mbili zilizo wazi.

Katika mabadiliko hayo, Kikwete amemteua Bernard Membe, kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akichukua nafasi ya Dk. Asha-Rose Migiro, aliyeteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo.

Kuteuliwa kwa Membe kushika wadhifa huo, kumehitimisha minong’ono iliyosambaa kwa siku kadhaa sasa, ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikimtaja mwanasiasa huyo ambaye ana shahada ya uzamili katika masuala ya uhusiano wa kimataifa, aliyosomea katika chuo maarufu nchini Marekani cha John Hopkins kilichoko Washington DC.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Membe kuguswa katika mabadiliko ya mawaziri, kwani Oktoba 15, mwaka jana, wakati alipofanya mabadiko madogo ya kwanza ya mawaziri, alimwamisha kutoka kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na akampeleka Nishati na Madini.

Sambamba na uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Dk. Batilda Salha Burian, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu). Kama ilivyokuwa kwa Membe, hii inakuwa ni mara ya pili kwa Burian kuguswa na mabadiliko.

Dk. Burian ambaye awali alikuwa Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Juma Akukweti ambaye alifariki dunia nchini Afrika Kusini alipokuwa akipata matibabu ya ajali ya ndege iliyotokea mjini Mbeya.

Katika uteuzi huo, kwa mara ya kwanza, Kikwete amelazimika kuwateua wabunge wawili kuwa naibu mawaziri, mmoja akichukua nafasi ya Membe na mwingine ya Burian.

Wabunge waliopanda ni pamoja na mwanasheria kijana na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, ambaye anakuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Gaudence Kayombo, ambaye ni Mbunge wa Mbinga Mashariki, anayekuwa Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya uteuzi huo, iliyotolewa na Ikulu jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, mawaziri na naibu mawaziri hao wataapishwa leo saa 10.00 jioni.

Gazeti hili katika toleo lake la jana, liliandika kuhusu Rais Kikwete kukamilisha uteuzi wa mawaziri wapya, na kwamba tayari alikuwa ameshawasiliana nao.

Katika habari hiyo ya jana, kama ilivyokuwa ile iliyotoka katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili, Membe alitajwa kwa uhakika kabisa kuwa angepandishwa na kuwa waziri kamili, akichukua moja ya nafasi mbili za uwaziri, ile ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa au kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora).

Aidha, gazeti hili lilisema bayana kwamba, katika uteuzi huo, Kikwete atalazimika kumteua mbunge mmoja kutoka mkoani Ruvuma au mikoa ya Kusini kuwa waziri (kama alivyofanya kwa Kayombo), akichukua nafasi ya Akukweti, ambaye alikuwa akitokea wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma.
 
Phillimon mikael.

mbona unanifuatafuata bila sababu? kama umeshindwa hoja nyamaza tu.

naomba acha uongo zee zima linakuwa kila dakika linaongopa tu.

NAOMBA NIONESHE WAPI NILIANDIKA KUWA KUNA MAJINA YAMEKWENDA KWA MUUNGWANA NIKAMTAJA KIMEI KWENYE MADA YA UKABILA? KAMA KUNA KITU HICHO UKITHIBITISHA HAPA BASI MIMI SINTOENDELEA KUSHIRIKI HUMU KWANI NITAKUWA NIMEDANGANYA.

NIMELAZIMIKA KUANDIKA KWA HERUFI KUBWA KUTOKANA NA MATATIZO YAKO YA KUTIZAMA MADA KIMAKENGEZA.

NAOMBA NIONESHE WAPI NIMEWASILIANA NA CHINGA AFUNGUE THREAD YA KIMEI?

kwanini unaishi kwa chuki na uongo kila dakika? mimi nina data za TRA huko Ikulu kwa Muungwana unazijua wewe.

naomba unikome kunizushia kila jambo baya nimekukosea nini? au Chinga kufungua thread ya kumfanananisha MBOWE NA CHIFUPA mnaona nae anachuki wachagga?

wanabodi.

mfuatilieni Phillimon Mikael ananinyanyasa bila sababu.basi lipueni na computer yangu kama mlivyochoma nyumba ya Benny LUSEGE WA TRA.
"Amani iwe nanyi...nawaachieni amani yangu"
 
Kuna jina moja ambalo linasahauliwa...GRAY MGONJA! He has a bigger chance of landing the job than the other two,ndio maana hata kampeni hafanyi.Kwanza bado yuko kwenye payroll ya BoT,he was seconded to the finance ministry enzi za Mkapa from BoT,na aliacha sifa nzuri tu huko BoT.Na huko Ministry pia wanamsifu sana.Lakini,i cant really say much,maana kama Makamba aliweza kuwa Katibu Mkuu wa CCM,then anything is possible.
 
chance ni kuwa kama mtu ni Mchagga....sidhani kuna watu watapenda iwe hivyo... Wachagga TRA.. wachagga BOT...??? what a conspiracy!
 
Mkjj, "Mgonja" - Mpare, au sio. Still no. He is a northerner, remember! Na asiwe wa kuja. You can narrow the list mpaka tumpate anayekubalika!
 
Back
Top Bottom