Kwa nini Kikwete aliwakimbia waandishi wa habari?

ukweli Rais ametuaabisha sana maana alionekana kwanza mwishoni amekasirika sana bara baada ya kutaja jina la mwisho nikaona anaondoka haraka haraka kwa kifupi uwezo wa rais wetu kujibu maswali sio mzuri ila kwa kuwa yuko kwenye system tukubaliane ndiye Rais wetu na hatuna jinsi
 
Kweli kamanda tuwe wavumilivu 2015 tuweke rais wa ukweli siyo mwanasesere, hatuna jinsi tukubali matokeo japo kwa mbinde
 
kama kweli wewe ni mwandishi wa habari basi ulitakiwa ujue kua kuna wakati rais anaiita waandishi wa habari na kunakua na maswali na majibu...na kuna wakati mwingine akitaka kutangaza kitu kwa wananchi wote then anafanya hivyo kupitia kwa media i.e waandishi wa habari, television na radio... ukiangalia hata obama, cameron na viongozi wengine duniani kuna saa za maswali na majibu na kuna saa za kutanganza kitu muhimu kwa nchi nzima kupitia nyie media alafu basi wanaondoka zao kuendelea na shuhuli zingine...kama hiyo ulikua wewe hujui basi ningeomba urudi tena shule ukaendelee ukasome zaidi:thinking:

Kikwete lini amepata kuwa na 1-2-1 na waandishi wa habari? Unamtetea kwakuwa kakutuma siyo?
 
Na siku hizi anazeeka kwa kasi hata kile kitambi cha dawa kinapotea
 
Rais aliwaita wanahabari ili awatangazie Watanzania Baraza jipya. Labda tupate nakala ya mwaliko ili tuone kama kuna kitu hakukitimiza, vinginevyo tuwe wapole tu.
 
kama kweli wewe ni mwandishi wa habari basi ulitakiwa ujue kua kuna wakati rais anaiita waandishi wa habari na kunakua na maswali na majibu...na kuna wakati mwingine akitaka kutangaza kitu kwa wananchi wote then anafanya hivyo kupitia kwa media i.e waandishi wa habari, television na radio... ukiangalia hata obama, cameron na viongozi wengine duniani kuna saa za maswali na majibu na kuna saa za kutanganza kitu muhimu kwa nchi nzima kupitia nyie media alafu basi wanaondoka zao kuendelea na shuhuli zingine...kama hiyo ulikua wewe hujui basi ningeomba urudi tena shule ukaendelee ukasome zaidi:thinking:

Mkuu nenda karevise guidlines za Press Conference.....PC isiyokuwa na maswali na majibu ni "MFU"
 
Kama walikuwepo hawa Said Kubenea, Absalom Kibanda, yule wa gazeti la mwananchi, (nani sijui, nimemsahau though nilimwona) Charles Kulingwa, mzee wa maswali magum wa Tanzania Daima na wale wa Raiamwema unategemea nini...........
Hili bandiko lako linaonyesha wazi wewe sio msomaji wa magazeti
 
Rais Jakaya kikwete aliwaita wahariri wa vyombo mbali mbali ikulu ili kuwatangazia uteuzi wa mawaziri. Lakini alipomaliza tu kutangaza akakimbia! Kulikoni mh Jk? Si uliwaita? Kwa nini hukutaka maswali mheshimiwa?. Kama ulijua utatukimbia kwanini utuite?

Kwa kweli nimesikitika sana kuona Rais anakimbia maswali!
Nadhani aliogopa kuulizwa kuhusu kumwacha ktk baraza la mawaziri Mkuchika, Maghembe, na Wasira?

Ukweli ni kwamba aliogopa kuulizwa maswali ambayo yangmsuta na kumfanya aaibike mbele ya camera za nchi nzima na huenda ilitokana na ushauri wa watu wa usalama waliomshauri saa ya mwisho
 
Mhh hebu nifikiri,issue yenyewe nimeshinikizwa,uteuzi wenyewe lengo ni kuzuga watu,halafu niwaruhusu waniulize maswali hawa ?badala ya kuniuliza si wataniliza hawa, ebu nisepe mie!
 
Kwa hili jk huku
watendea haki,
tungekuwa ni jeshi
sawa!
 
Rais aliwaita wanahabari ili awatangazie Watanzania Baraza jipya. Labda tupate nakala ya mwaliko ili tuone kama kuna kitu hakukitimiza, vinginevyo tuwe wapole tu.

Mbona tunajua aliwaita ili aoneshe jinsi wasiowajibika wanavyowajibishwa ndiyo hoja ya kusuka upya baraza la mawaziri na mwishoni akasema na wale wa chini watapaswa nao kuwajibishwa...hapa ndipo tunapata kigugumizi kwa dhana (concept) ya kuwajibika ya rais wetu...hivi hajui kama anawajibika kwa watanzania tuliomchagua? Sasa tukitaka kumuuliza masuali akaacha kuwajibika nani amwajibishe yeye? Busara ingekuwa hata kama haikuwa nia yake angewaomba radhi tu kuwa leo sintakuwa na muda wa masuali kwa sababu nina shughuli nyingine, vinginevyo na yeye ingekuwepo 'bodi' ya waajiri angewajibishwa kwa kutokuwajibika kwa wananchi wake. Kwani si huyu huyu ndo aliingia na namba ya kupiga moja kwa moja na kumuuliza masuali? Leo anapata kigugumizi gani kujibu masuali...ama kweli 'ukiona chongo huita kengeza'
 
wewe unaemwambia mwenzio arudi shule we ndio uanze kurudi faster....kama hataki maswali si angeijumuisha kwenye hotuba zake za mwisho wa mwezi au wangepeleka press realese kila media au angeenda tbc akakae na malin hassan watangaze nini maana ya kuita watu wakusikilize? That means kama wanaswali wakuulize kama hawajapublish.......msizarau hoja za wenzene kwa maslahi ya hisia zenu.

watanzania amkeni....umeshaona speech za obama, bush, sarkozy, cameron...mara ngapi obama anaita waandishi wa habari pale white house anatoa speech akimaliza anaondoka hajibu swali hata moja....mbona hujiulizi kwanini hicho alichotaka kusema hakusema kupitia press release??? kuna saa kiongozi wa nchi anataka kuzungumza na wananchi wake kupitia radio na television lakini kunakua hakuna maswali tena kabla ya hiyo speech tayari mkurugenzi wa mawasiliano wa ikulu anawaambia kabisa kua leo mnasikiliza anayosema rais basi hakuna maswali ndio maana hata alipomaliza kuongea hakuna mwandishi wa habari aliyepanua mdomo wake ni kwa sababu walijua kua hakuna maswali na majibu...

Umesema kwanini asisubiri mpaka mwisho wa mwezi...well mwisho wa mwezi atakua yupo safarini marekani na angesubiri mpaka mwisho wa mwezi wananchi wangelalamika hapa...kila mtu alikua anataka baraza la mawaziri livunjwe haraka...

Wabongo bana wabishi kweli kuridhishwa...mlitaka rais abadilishe mawaziri amefanya..sasa mnalalamika kwanini hakujibu maswali...ule haukua muda wa maswali...msubiri wakati wenu utafika ambao rais anakaa chini anajibu maswali ya media.

dayuuuummm:frusty:
 
Upo sahihi Mkuu, lakini bado suala la kwa nini kawaita? Kawaita kwa sababu tu Obama, Cameron wanafanya hivyo na Kikwete afanye? Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu isingeweza kurekodi hiyo hotuba ya mheshimiwa na kuituma kwa wakati mmoja kwa vyombo vyote vya habari na waandishi wa habari wote, bila ya yeyote kupoteza wakati, kupoteza mafuta?

Leo unaita waandishi wa habari saa tisa, wanakuja unapowaita, wanakaa mpaka saa kumi na nusu ndio unatoa hotuba ambayo kila mmoja angetumiwa aliko. Hapana, hii ni kuishi enzi za giza.

hapana hii ni sio enzi za giza bali kumbuka sasa hivi media imejiendeleza sana, sasa hivi tanzania tunajivunia na live television...kila kitu siku hizi ni live sio kama zamani vitu vinarekodiwa... Kikwete kila wakati yuko marekani na uingereza so nadhani amekua aki study wenzake wanavyo handle media na yeye kaamua kuiga...nitakupa mfano...wenzetu ulaya kukitokea kitu cha dharura either ni janga au kitu chochote ambayo kiongozi wa nchi inabidi aongee na wananchi wake basi wanaita waandishi wa habari kiongozi awe ni rais au waziri mkuu anakuja kwenye chumba anaongea anachotaka kuongea akimaliza anaondoka...nadhani kikwete anajaribu kuleta ile style ya america/europe hapa dar. Sema sasa wabongo wengi hawaijui hiyo ndio maana mnapiga makelele hapa..mnaona kua rais akiita waandishi wa habari ni lazima ajibu maswali....angalieni cnn/bbc muone wenzenu wanavyofanya....kikwete anajua hilo kwa sababu kila mwezi anawatembeleaga huko makwao:)
 
Kikwete lini amepata kuwa na 1-2-1 na waandishi wa habari? Unamtetea kwakuwa kakutuma siyo?

:happy: hajanituma kama unasomaga michango yangu utaona kua kuna vitu vingi sana anafanya ambavyo sikubaliani navyo lakini hili la juzi namtetea...hakua na haja ya kujibu swali and as much as i dont like him as a president bt kwa hili namtetea 100%. He wanted to send his message across and he did that. Maswali yana wakati wake, kueni na subira kuna wakati mtakutana nae mtamuuliza maswali yoooote mtakayo!!
 
Rais Jakaya kikwete aliwaita wahariri wa vyombo mbali mbali ikulu ili kuwatangazia uteuzi wa mawaziri. Lakini alipomaliza tu kutangaza akakimbia! Kulikoni mh Jk? Si uliwaita? Kwa nini hukutaka maswali mheshimiwa?. Kama ulijua utatukimbia kwanini utuite?

Kwa kweli nimesikitika sana kuona Rais anakimbia maswali!
Nadhani aliogopa kuulizwa kuhusu kumwacha ktk baraza la mawaziri Mkuchika, Maghembe, na Wasira?
Are yu
ou a serious Editor au kilaza. Je hakutekeleza alichowaitia? Acha hizoooo.
 
Naamini alijua kasoro za uteuzi wake na aliogopa maswali ya waandishi wa habari,kwa mfano haiingii akilini kumtema Ngeleja na kumuacha naibu wake Malima.Cha kushangaza hata Mkuchika nae kabebwa wakati TAMISEMI ni uozo mtupu mfano yaliyotokea halmashauri ya kishapu na waziri yupo tu mpaka CAG aje aweke mambo hadharani na bado hakuchukua hatua yoyote.Kwa kifupi huyu raisi hana uchungu na nchii hii na mimi binafsi naomba muda wake uishe tu vinginevyo taifa linaelekea kubaya.
 
Back
Top Bottom