Kwa nini Karume, Nyerere na Union Day?

RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,966
2,019
Hapa Tz tuna siku kadhaa za kitaifa, ambazo huwa ni mapumziko na hutumika kuadhimisha au kukumbuka jambo fulani.
Ukiondoa siku za kidini kuna siku zifuatazo (ambazo zinakua mapumziko):
  1. 12/jan - Mapinduzi Zanzibar
  2. 07/april - Karume
  3. 26/april - Muungano
  4. 01/mei - wafanyakazi
  5. 07/julai - biashara
  6. 08/agusti - wakulima
  7. 14/octoba - Nyerere
  8. 9/desemba - uhuru Tanganyika
Hapa ongezea Krismas siku 2, mwaka mpya siku 1, pasaka siku 2, idi elhaji 1, idi elfitri 2, maulidi 1. Inawezekana nimesahau nyingine (mnisamehe)!

Kwa maoni yangu, siku hizi ni nyingi mno kwa taifa kupumzika (sina takwimu za nchi nyingine za ukanda huu).

Hoja yangu ni hii, tunapoadhimisha siku ya muungano wa Tz kwa nini tusiwakumbuke na waasisi wa muungano huo? Kama tunawakumbuka...kuna haja gani ya kuwa na Nyerere day na karume day?
 
Mkuu Roya Roy, Mie ninajiulizaga pia kwa nini tunapumzikaga wiki end? (Jumamosi na Jumapili).
Mie ningeshauri tuwe kama Wachina tusiwe na Mapumziko yoyote ndani ya wiki.
Au kama itawezekana kwa vile Taifa letu lina Wanataifa wenye dini/Imani zao basi siku ile ya ibada yake huyo mtu asiende kazini bali siku zote zilizobakia sita aende kazini.
Kwa hiyo kutakuwepo na watu watakaopumzika J1 wengine J2, wengine J3 hadi Ijumaa. hivyo siku zote ziwe ni siku za kazi.
 
Leo ni Karume day... sijui kinachofanyika kustahili siku nzima ya mapumziko.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom