Kwa nini Kandoro hataki maswali juu ya michango ya shule???

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,444
Kama wiki hivi nilisikia kupitia vyombo vya habari kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Abbas Kandoro aking'aka analipo ulizwa kuhusu michango ya secondary aliyo kuwa akichangisha hivi karibuni.
Jana tena nimesikia kang'aka hataki aulizwe kuhusu michango.Lakini hapo hapo amewahimiza wakazi waendelee kuchangia michango ya shule.
Sasa kuna haja ya kwendelea kuchangia hizo shule za YEBO YEBO au VODA faster huku mapato na matumizi tunanyimwa kujua ni kiasi gani kimepatikana na kiasi gani kinahitajika tena.Wana JF hamuoni kama kuna kaharufu ka matumizi yasiyo eleweka hapo?
Kwa hiyo twendelee kuchangia huku tukinyimwa taarifa kama pesa zinatumika kwa shughuli sahihi ambayo imeitishiwa harambee?Pesa si zetu tumechangia watoto waende kusoma alafu tunanyimwa taarifa ya makusanyo hii ni haki kweli?Kwa nini anakataa kutoa taarifa wakati alikuwa mstari wa mbele kutuchangisha sisi walalahoi hizo pesa?Ilifikia kipindi ni lazima uchangie.
Napenda kuwakilisha.
 
Ukiyaona madarasa yenyewe yanayojengwa na thamani ya mapesa tunayotajiwa kuwa ndio wamelipwa makandarasi wa majengo haya, utapata jibu zuri la swali lako. Kandoro hataisahau Dar na hasa mradi huu wa shule za sekondari.
 
Hata me namshangaa sana huyu mkuu wa mkoa. kama hela zimechangwa na wananchi kwa nini hataki kuwaambia kuwa hadi hivi sasa tumechangisha kiasi fulani, na tumetumia kiasi fulani katika ujenzi wa shule. lazima utakuwa ni mradi wa watu wachache. lazima wamekusanya hela nyingi sana.
 
Jamani mwenzenu anawania kiti cha Galinoma..........hukooo.....Iringa kwaoo mnataka akose ubunge awe mtumwa tuu wa ukuu wa mkoaa milele??nae anatajka kuitwa Mh.Kandoro soon labda atapewa unaibu waziri wa Tamisemi sababu atadai ana uzoefu na...................tawala za mikoa na serikali za mitaa...........ameshaona mbali sana huyu
 
ivi si Lowasa amesha achiangazi sasa hela zinaenda wapi tena??!! mana kwa mimi badala ya kuboresha shule zilizopo kwa kuziweka katika hali nzuri eti kujenga nyingine....wanafunzi wenyewe ukiwaona wa sasa tofauti na wale ya miaka ya nyuma ambao walikua wakijivunia na shule zao sasa utajivunia nini shule vumbi linaingia ndani utafikiri uko machimbo ya buzwagi vyoo ndo usiseme....mimi kwa hili la kuchangisha eti kwa ajili ya shule mpya dah sioni maana bado.
 
lazima wamekusanya hela nyingi sana.

Wamekusanya mamilioni walianzisha hata sticker za kuchangia kwenye magari usipo changia unakamatwa na jiji magari ni 10,000 kila gari,maduka ya kawaida 5000, maduka makubwa 50,000, na nyumba ni 2000 kila nyumba.Wakuu nisaidieni hapo ni mabilioni mangapi hawa jamaa wamekusanya?
 
Huyu Kandoro na watu wake wanachekesha sana. Walikuja ofisini kwetu mwaka jana kuchangisha pesa za shule wakataka pesa taslim tukawakatalia. Tuliwapa cheque. Mwezi Juni 2008 wakaja tena na hiyo cheque eti muda umepita hivyo "ime-expire!". Wanataka niwape cash. Nikawafukuza ofisini kwangu. Sasa naelewa kwa nini Kandoro hataki maswali huhusu michango ya shule.

Byase
 
Huyu Kandoro na watu wake wanachekesha sana. Walikuja ofisini kwetu mwaka jana kuchangisha pesa za shule wakataka pesa taslim tukawakatalia. Tuliwapa cheque. Mwezi Juni 2008 wakaja tena na hiyo cheque eti muda umepita hivyo "ime-expire!". Wanataka niwape cash. Nikawafukuza ofisini kwangu. Sasa naelewa kwa nini Kandoro hataki maswali huhusu michango ya shule.

Byase

Huyo ni ufisadi mwingine.
 
Ndio maanaya Chukua Chako Mapema jamani
huku wananchi wakiendelea kuchangia bila majibu, maana kila mtu anachukua lipo, na hiyo ndio maana halisi ya CCM

Huyu anajiandaa kwa uchaguzi 2010 nasikia anagawa mabati sana hapo Kalenga kwa ajili ya ujenzi wa shule., yawezekana michango inachangwa Dar shule zinajengwa Kalenga.
 
jamani sasa kuwang`oa tuanzie wapi? tulianzia juu kwa akina el kumbe hata huku chini nako jamaa wanatapanya kidogo tulichopata!!!!!
Mwaka umeisha sasa tangu tuanze kuchangia elimu hapa Dar hakuna taarifa,hivi kweli tutawalaumu wachangia harusi,sendoff,kitchenparty? angalao wao mwisho wa siku huburudika na moja moto moja baridi halafu wanavunja kamati baada ya shughuli nzito. Kandoro tupe maelezo usikae kimya mzee,hiyo ni pesa yetu
 
Ufisadi unatupeleka pabaya mno,itafika mahala tutakosa wa kumgusa.kila mmoja ataanzisha michango na regulations zake ambazo tutalazimishwa kulipa.mfano hai ni huyu muheshimiwa raisi wa daressalaam.madaladala yote walilazimishwa kulipa shilingi 5000 na zoezi lilisimamiwa na trafiki,leo hii inapokuja kwenye accounting wanakuwa wakali.this is unfair to tanzanians ambao wana work hard to sustain their well being wao wanaishia kusquander their efforts.
 
Sasa inatulazimu tuandamane hizi pesa zimechangwa nyingi sana sijaona hata darasa moja lililo jengwa kwa pesa hizi ambazo wavuja jasho tumechanga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom