Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,063
- 22,755
Baada ya kumsikiliza Mzee Cigwiyemwisi John Samwel Malecela kuhusu utamaduni wa ndani wa CCM kumwongezea kipindi kingine cha miaka mitano Raisi aliyeko madarakani, inabidi tukae chini kama wananchi tujiulize maswali kadhaa. Mwaka 2005, Raisi Col. Dr. Al Haj Jakaya Mrisho Kikwete alitoa ahadi na malengo kadha wa kadha na kuahidi kuyatimiza kwa ari, kasi na nguvu mpya.
Huu ni muda muafaka wa kutazama amefanikiwa kwa kiwango gani katika kufikia hayo malengo. Naomba tushirikiane kwa kuyaanika na kuyajadili hayo malengo na kupima kama yapo mafanikio na mapungufu. Mimi naanza na moja linalohusu nishati na hasa umeme ambapo miezi minne tu baada ya kuchaguliwa, Raisi alitamka haya kuhusu sakata la kupatikana kwa umeme wa uhakika.
Ni wazi hapa aliwaahidi wananchi kuwa chini ya miaka mitatu tatizo la umeme lingeshughulikiwa na tungeweza kuwa na mipango madhubuti ya umeme wa kuaminika. Sasa baada ya miaka karibu minne na tukikaribia uchaguzi mwingine mwaka kesho, kuna dalili zozote kuwa tumepiga hatua katika kutatua hili tatizo ? Je, kuna sababu yoyote ya kuendelea kumwamini Raisi kwenye hili na na kumwongezea kipindi kingine ?

We have been grappling with this problem for quite some time now but only with ad hoc measures.The recent power problems have afforded us the opportunity to rethink our energy strategy in holistic terms. We have learnt that ad hoc measures are costly in the long run and have their own limits. As we grapple with our energy problem, we are witnessing an upsurge of interest for investments in power generation in Tanzania. We are confident that in two years time, we will be on course to realize reliable power supply in Tanzania.
Ni wazi hapa aliwaahidi wananchi kuwa chini ya miaka mitatu tatizo la umeme lingeshughulikiwa na tungeweza kuwa na mipango madhubuti ya umeme wa kuaminika. Sasa baada ya miaka karibu minne na tukikaribia uchaguzi mwingine mwaka kesho, kuna dalili zozote kuwa tumepiga hatua katika kutatua hili tatizo ? Je, kuna sababu yoyote ya kuendelea kumwamini Raisi kwenye hili na na kumwongezea kipindi kingine ?
Naomba na wengine mtafute ahadi zingine alizozitoa tuweze kuzijadili - nawasilisha.