Elections 2010 Kwa nini JK anaogopa kuzungumzia ufisadi katika kampeni zake?

Mafisadi wana nguvu sana. Akiwagusa, mbali na uchumi wa nchi kutikisika hata uchaguzi utaahirishwa. Si mnamkumbuka Pinda alisema "mafisadi wana nguvu sana, hatuwezi kuwakamata. Uchumi wetu utatikisika". Full stop
 
This guy is a big joke, yaani unajua mimi nashindwa kuelewa hata wanaomwamini ni kwa misingi ipi? Heleweki anasimamia nini, anaogopa debate, anaogopa hata kutja tu neno ufisadi and yet anatoa tu miahadi amabayo hata kama atajaribu kufanya hela zitaliwa as usual na kwa sababu walaji ndiyo wachangiajai wa kampeni yake............... basi itakuwa kama ilivyokuwa

Point to note:

" Ni wapi na lini raisi serious kwenye masuala ya rushwa na ufisadi anakuwa rafiki wa wafanya biasahara woote ndani ya nchi, wafanyabiashara wa aina tulionao hapo bongo"

Have u ever seen a candidate talkin' to rich people on television? thats the rule of the game
 
Mafisadi ndio nguzo ya CCM. Na ufisadi ndio msingi wa maendeleo ya CCM.

CCM ndio chama pekee tawala duniani kilichozaa sheria ya kukubali rushwa wakati wa uchaguzi(Takrima) na baadaye kuiondoa baada ya vyama vya upinzani, viongozi wa dini na wanaharakati mbalimbali kupiga kelele. Hapa nikiikumbuka PCCB na CCM kichwa kinawasha, hivi panakwenda kweli!!!

Sasa katika hali kama hii, na mambo ya kutambulisha mafisadi kwa wananchi kama wagombea safi, tutegemee nini? kwamba JK ataongelea ufisadi kweli? asemeje...atoe siri hii kwamba bila kukumbatia ufisadi hakuwezi kuwa na CCM???
 
Mkuu wewe unaweza kumkana mzazi wako hata angekuwa mkoma? Basi JK ni zao la ufisadi kwa hiyo na yeye ni FISADI VILEVILE
 
Ni kweli sijawahi sikia hayo nakumbuka kipindi ni mtoto wa ccm CHIPUKIZI tulikuwa tunasema "Rushwa ni adui wa Haki sitatoa wala Kupokea Rushwa.........bha..bha....." ndo ccm niliyokuwa naifahamu mimi but sasa ni hatari. Rushwa inakumbatiwa nashangaa hv kwenye kampeni zake watu hawamuulizi maswali hayo! mi huwa siendi nikimsikiliza hata kwenye TV siangalii, niangalie nini? wakati najua ataongea Upupu napatwa na hasila.
 
Back
Top Bottom