Kwa nini JK Alishtuka na KUSHANGAA Sana PINDI Wabunge wa CHADEMA Walivyotoka Bungeni

Bado Niponipo

JF-Expert Member
Aug 15, 2008
680
168
Mh. Alishtuka na kushangaa sana pindi wabunge wa CHADEMA walipoinuka na kutoka bungeni, Kwa mtazamo wangu hakuwa na taarifa kwamba CHADEMA walikuwa na mpango ule, Cha kushangaza watu kwa maelfu nchini na nje walijua fika kuwa pindi atakapokaribishwa ili aanze kutoa hotuba ya kufungua bunge basi wabunge wa CHADEMA wangetoka bungeni,
JE inamaana alikuwa halijui hili na kama ndivyo wasaidizi wake huwa hawamwelezi ni nini kinaendelea kwenye vyombo vya habari?.

Wasalaam

BNN
 
Naamini alikuwa anafahamu kwa vile dalili zilikuwa wazi toka Pinda anaapishwa. Ila nadhani aliamini vijana wake wangekuwa wamezima joto
 
hana maarifa ndo maana jana aibu imemkuta na hatakaaa asahau maisha yake yote
 
Naimani alikua na taarifa ila hakuwa na uhakika kama kweli jamaa wamedhamiria
 
labda wanamuona zoba,ukumbuki siku ile alipochakachuliwa mafuta ya GARI lake,wanamuona kama kicheksesho mana kwa taarifa yako hat wasaidizi wake wamemchoka.
 
Hakuna aliefanikiwa kupata angalau picha jamani.
Maana kwenye luninga alionekana kuduwaa alafu baadae akajikaza kisabuni
 
labda wanamuona zoba,ukumbuki siku ile alipochakachuliwa mafuta ya GARI lake,wanamuona kama kicheksesho mana kwa taarifa yako hat wasaidizi wake wamemchoka.

Kwa hiyo kuna uwezekano wasaidizi wake walimwambia mzee usitie shaka tumeshasawazisha mambo kumbe wanampiga fix mzee wa watu?..
 
Hakuna aliefanikiwa kupata angalau picha jamani.
Maana kwenye luninga alionekana kuduwaa alafu baadae akajikaza kisabuni

Njowepo!

Ule mshuko na simanzi ulimfanya mkuu akaduwaa kwa dakika kadhaa, hata alipotea ni wapi alifikia kwenye hotuba, ikadidi aanze upya, super LOW
 
ninauhakika hakujua maana ni msee wa kudanganywa tu, wasaidizi wake walishamwona ni boya tu. Pengine wakati wa kumwapisha Waziri mkuu aliambiwa gari lililowabeba chadema limepata pacha lakini wanakuja muda si mrefu naye akaamini. si mnajua kila kitu huwa anawakubalia tu wasaidizi wake?
 
Mtoa maada uko sahihi kabisa, walio karibu na JK walikuwa wanadumisha mila za 'ndiyo mzee' na kuogopa kusema ukweli, utamaduni wa kuficha ukweli unavitafuna hata vyama vyetu vya upinzani, tumezoea kufichaficha sana issue ambazo ni za ukweli.

atie huruma, atiwe huruma shauri zake!!, alipata sawa kabisa kilichotakiwa muda huo!
 
Mkuu ule mshangao na mshtuko ulikuwa mkubwa sana, alitia huruma aisee, hakuamini macho yake.

Hakua na uhakika kama wangetekeleza azma hiyo na ilimuongezea imani zaidi pale alipoenda mbele na hakuna kilichotokea ndio maana akaanza hotuba yake kama kawa. Ilikua ni bonge la suprise kwake pale alipoinama kusoma hotuba na kuinuliwa na zile kelele ndio maana macho yalimtoka mbaya!!!
 
ila noma alishangaa hadi mate yakataka kumdondoka baba wa watu, ila sithani kama atasahau uchaguzi na hii ungwe yakae ya mwisho maishani mwake!
 
ninauhakika hakujua maana ni msee wa kudanganywa tu, wasaidizi wake walishamwona ni boya tu. Pengine wakati wa kumwapisha Waziri mkuu aliambiwa gari lililowabeba chadema limepata pacha lakini wanakuja muda si mrefu naye akaamini. si mnajua kila kitu huwa anawakubalia tu wasaidizi wake?

Hii inanikumbusha issue zake za kwenda kukabidhi dummy cheques lakini figure inasema 7,000,000 na maneno yanasema laki saba, anaenda kufungua daraja hewa, anaenda kukabidhi ambulace kwa mkurugenzi wa wilaya tofauti.
Wasaidizi aina hii watatukost siku moja.
 
Mh. Alishtuka na kushangaa sana pindi wabunge wa CHADEMA walipoinuka na kutoka bungeni, Kwa mtazamo wangu hakuwa na taarifa kwamba CHADEMA walikuwa na mpango ule, Cha kushangaza watu kwa maelfu nchini na nje walijua fika kuwa pindi atakapokaribishwa ili aanze kutoa hotuba ya kufungua bunge basi wabunge wa CHADEMA wangetoka bungeni,
JE inamaana alikuwa halijui hili na kama ndivyo wasaidizi wake huwa hawamwelezi ni nini kinaendelea kwenye vyombo vya habari?.

Wasalaam

BNN

Hapo ndio ujue hana wasaidizi wa maana walitakiwa wamwandae ki saikolojia
 
Mimi nadhani alifikiri kwa uoga wa watanzania hakuna mtu atayeweza kufanya kitu kama hicho hajui kuwa siasa zimebadilika sana siku hizi.
 
zamani tulikuwa tunamuona raisi kama MUNGU hzo enzi haziko tena siasa imeshakuwa hapa TZ na hyo ni traler mazee sipati picha vikao wanavokaa ccm sasa hv wanajadili nini
 
Back
Top Bottom