Kwanini JF?

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,190
18,076

Habari wana JF woote na familia yoote ya MMU….

Nina exactly 46 days toka nisikie kuhusu Jamii Forums na 45 days toka nijiunge …. Kila siku inapopita nafurahia na kuappreciate uamuzi wangu wa kuamua kujiunga katika JF na kua mmoja wa GT.. Nimepata marafiki wengi, Chat mates, PM mates, admirers na non admires, Knowledge katika kila sphere kama habari, urafiki, mapenzi, utani, elimu, sheria, siasa, entertainment e.t.c. And most importantly nimepata exposure kubwa saana in a lot of things….

Sababu kubwa ilinifanya kujiunga ni baada ya kusikia mmoja wa viongozi wetu akilalamika kua Jamii Forums ina chafua na kuharibu image ya serkali as well as Chama cha magamba…. (Namshukuru Mungu kila siku kwa huyo Leader kuipromote mpaka nikasikia) Hio ilinipush ni google kutaka nijue ni kitu gani, then nikaenda moja kwa moja kwenye International forum ambapo nilikutana na thread ambayo nilitaka saana nichangie sababu nilikua against na mtu alokua ametuma hio Thread (in fact alikua Rutashubanyuma) who ironically turned out to be one of my friends sasa… I had to register hapo hapo!

From that moment kila kitu kilifuata mkondo hadi when I found my home in MMU a week later… Cha ajabu kilichonifanya nijiunge sio kinachonifanya nibaki saizi…. Napenda every fun and activity I do while in JF, napenda watu behind the Avatars na above the Signatures, napenda the challenges I meet (ndo maana siasa hua nakimbia…), napenda kua watu wako huru kujiexpress regardless of age or gender, napenda kua kuna variety of topics and forums, Hio ikisukumwa na watu ninaowasiliana nao na kubadilishan mawazo katika uzi mbali mbali….

Naamini kila mmoja ana sababu tofauti ingawa nyingine zaweza fanana.. wewe kama member wa JF naomba mchango na mawazo yako ni kwanini au nani alikusukuma na kukushawishi uweze kua moja wa member wa JF ukitaka/kubali kua GT…

Asha D.
Pamoja Sana.
 
maelezo yako mazuri..lakini bila shaka hiyo heading yako inahitaji majibu! siku zote critical thinking ni mwiba kwa wachakachuaji
 
maelezo yako mazuri..lakini bila shaka hiyo heading yako inahitaji majibu! siku zote critical thinking ni mwiba kwa wachakachuaji

I don't know kama hukumaliza kusoma au lah! maelezo ya juu ni sababu zangu...
nimeona ni highlight swali langu kwa hio rangi ya beige ili walau uweze ona...s.fm hope umeridhika...
Hivyo heading iko in support na paragraph yangu ya mwisho... inanifanya niwe na wasi kama kweli you have read...
 
mimi nilisukumwa baada ya kusikia sana kwa marafiki, nikaamua si mbaya kujiunga na kujionea mwenyewe kwa kweli nilifurahi sana ni mahali penye uhuru wa kutosha wa kuchangia na kujieleza na zaidi mimi naichukia serikali hivyo nilidhani ni vizuri kujua madudu yake zaidi na kutoa michango yangu kuliko kujinyamazia. kwa kweli naipenda jf every forum looks good for me. na zaidi napenda challenge za wanajf katika topic mbalimbali.
 
Hahahahahaaaa AshaD, nashukuru sana kusikia ni namna gani uliingia hapa, hii inanikumbusha mie pia kuna mahala hua tunakutana na marafiki zangu mara kwa mara, Mie mabest wangu wengi ni wanaume, kwa hiyo nikawa nawasikia kila siku wakiongelea JF, mie nikawaambia siwezi kabisa habari ya kusurf kwenye mablog na ma forum kila siku, na kumbuka hapo tukikutana wanaitana majina yao ya ID za humu.Hii imenifanya nikiingia humu nawajua wote na huwa nafurahia sana michango yao.

Mmoja akaniambia nijiunge akanambia ukijiunga utakuwa addicted hasa MMU, nikamkatalia,akanipa modem ya bure nilipofika home nika google kama kawaida nikaingia.tokea hapo nimekuwa sibanduki kabisa na sikuwaambia mpaka walipo guess ila still sijawahakikishia ID yangu. JF imenipa marafiki wa kila aina.Sijajutia kujiunga kila siku mpya inapoingia huwa kuna jipya na hii inafanya siku iende vizuri
Ahsante kwa kunikumbushia
 
Wakati ule nikiwa bado nakubali kuitwa Babu DC, nilioteshwa kuwa kuna uwanja mzuuri sana unaitwa JF....Nilipofika kwenye hiyo kitu nikakutaa actually kuna viwanja vingi....Baada ya kuranda randa huku na kule nikagota kwenye kimojawapo....

Kwa sasa niko kama addict wa hii kitu.....Nitafanya kila njia kuchungulia hata kama sitaongea kitu!!

Ubarikiwe sana Asha D na karibu kwenye ulimwengu huu wa uhuru wa maoni..Ila jiandae pia kukupana na visiki visivyo rahisi kuving'oa!!

Mzee DC
 
Gaga thank you for sharing..... Na the above statement is so true lol...... usipokua mjanja kazi zinalala.... enjoy dear..
 
Mzee DC nafurahi kwa maneno yako yenye insight na pia nashukuru kwa kuendelea/sisitiza hayo makaribisho, nimejipanga kuhusiana na hivyo visiki, najua sio rahisi but naomba Mungu aniongeze ustahimilivu na kwa kuwezesha hilo nimeona niweke signature ya kupambana nao ili nisije jisahau na kuingia mkenge... wala hata tu kuepusha BAN!
 
Gaga thank you for sharing..... Na the above statement is so true lol...... usipokua mjanja kazi zinalala.... enjoy dear..
We acha tu mie nikifika ofisini napanga kazi zangu kwa mafungu matatu, kila fungu nikimaliza naingia humu tena mpaka naondoka home, bila malengo kazi zinalala.siku nikiwa tight naingia wakati wa lunch
 
Me namshukuru zaidi yule jamaa wa chama gani vile? aloamua kulalama kuhusu jf kumbe anaipromote, safi sana, karibu!
 
We acha tu mie nikifika ofisini napanga kazi zangu kwa mafungu matatu, kila fungu nikimaliza naingia humu tena mpaka naondoka home, bila malengo kazi zinalala.siku nikiwa tight naingia wakati wa lunch

That is a good strategy, naona itabidi nijaribu adapt hii ya kwako - mimi ni kote kote na sometimes inafanya iwe ngumu, tena hapa ngoja i have something to attend to - umenikumbusha la maana saana!
 
Nilioteshwa kuwa siku moja Asha D ungejiunga JF.

Mhhhh Mdogo wangu TF,

Hiyo gia uliyoanza nayo ni nzuri sana....Sina shaka inaweza kukuvusha kila barabara hata kama ina matope na utelezi kiasi gani.

Nitazidi kukuombea ili huku tulipe na wewe siku moja ufike!! Ila usije kujinyonga ukikita si pazuri vile unavyotamani........Si unajua "hamu ni tamu kuliko tamu yenyewe"!!!!!

Mzee DC
 
Mzee DC nafurahi kwa maneno yako yenye insight na pia nashukuru kwa kuendelea/sisitiza hayo makaribisho, nimejipanga kuhusiana na hivyo visiki, najua sio rahisi but naomba Mungu aniongeze ustahimilivu na kwa kuwezesha hilo nimeona niweke signature ya kupambana nao ili nisije jisahau na kuingia mkenge... wala hata tu kuepusha BAN!

Hapo umeniondoa mashaka AD,

Maandalizi ni silaha au mkakati wa kwanza kabisa katika mbinu za kushinda vita...Naamini umeshashinda.

BUT...Chungulia na kuipigia hesabu kila hatua ...Miscalculation yoyote inaweza kukupoteza kabisa kwenye uso wa dunia hii ya JF!!
 
Mhhhh Mdogo wangu TF,

Hiyo gia uliyoanza nayo ni nzuri sana....Sina shaka inaweza kukuvusha kila barabara hata kama ina matope na utelezi kiasi gani.

Nitazidi kukuombea ili huku tulipe na wewe siku moja ufike!! Ila usije kujinyonga ukikita si pazuri vile unavyotamani........Si unajua "hamu ni tamu kuliko tamu yenyewe"!!!!!

Mzee DC
Hahahaha Mzee DC umenifanya niangue kicheko asubuhi asubuhi ofisini ngoja niendelee kutafakari hii statement yako maana ina mengi lol!!!!:biggrin1::biggrin1:
 
Hahahaha Mzee DC umenifanya niangue kicheko asubuhi asubuhi ofisini ngoja niendelee kutafakari hii statement yako maana ina mengi lol!!!!:biggrin1::biggrin1:

Poa TF,

Usinambia unajifunza mbinu za vita ndoni!!!! Hata hivyo strategies ni zile zile ama una-criminalize mtu ili umshinde au una-grolify ili mambo yako yanyooke. Hukujua hizo techniques kabla hujaanza kuzitumia hapo juu????

Mzee DC
 
Wewe nae kwani hilo ndo kauliza Asha D??

Mie kuna rafiki yangu aliadd bila mimi kujua nikawa napata reminder kwenye email kuwa we have missed you ..........................nikaamua kuanza kuchangia

Huyo hakika ni rafiki wa kweli (a friend in deed)...kizuri unakula na mwenzio kabaya unakufa nacho mwenyewe au?

Mzee DC
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom