Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,730
- 6,273
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao na makumi ya wengine wameuawa baada ya mapigano kuzuka kati ya wanajeshi wa Jamhuriya Kidemokrasia yaCongo na kundi la waasi wa M23, katika moja ya migogoro mirefu na mbaya zaidi duniani.
Sasa, vikosi vya Kenya vinajiunga na vita kusaidia jeshi la Congo, kwa lengo la kuleta amani katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini ambayo inapiganiwa na makundi tofauti yenye silaha.
Mapigano yanahusu nini?
Mzozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yalizuka miongo mitatu iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu milioni sita huku wengine milioni 4.5 wakilazimika kutoroka makwao.Katika mwaka uliopita, ghasia zimeongezeka kwa mara nyingine huku vikosi vya usalama vikipambana dhidi ya zaidi ya makundi 100 yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo, licha ya kuwepo kwa operesheni kubwa ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
Wanamgambo wa M23 na jeshi la Congo wameshutumiana kwa kuanzisha mapigano yaliyosababisha mgogoro wa sasa.
Hali imekuwa mbaya hadi siku ya Alhamisi Rais Félix Tshisekedi akatoa wito wa mapigano na kuwomba vijana wa nchi hiyo "kujipanga katika makundi" kusaidia jeshi.
Mzozo huo haujaathiri DR Congo pekee, lakini pia umedhoofisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hiyo na Rwanda, ambayo inashutumiwa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 na matokeo yake ikaishia kufurushwa kwa balozi wa Rwanda wiki iliyopita.
Rwanda inakanusha madai hayo.
Kundi la M23, ambalo liliundwa miaka 10 iliyopita, linadai kutetea maslahi ya jamii ya Watutsi wanaoishi nchini DRC dhidi ya wanamgambo wa Kihutu.
Rais wa Rwanda Paul Kagame aliingia madarakani akiongoza jeshi la waasi la Watutsi wanaopigana na Wahutu wenye itikadi kali ambao waliwaua maelfu ya Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994.
Wengi wa waliohusika na mauaji hayo wanadaiwa kukimbilia DR Congo baada ya majeshi ya Bw Kagame kuchukua madaraka nchini Rwanda, na ndiposa mzozo huo ukavuka mpaka na kuingia nchi jirani.
Ni wanajeshi wangapi wataenda DRC?
Idadi kamili wanajeshi watakaopelekwa haijatolewa. Tunachojua hadi sasa ni nchi nne tu Kenya, Uganda, Sudan Kusini na Burundi ndizo zinawapeleka wanajeshi wao.Wanajeshi elfu moja wa Kenya wataungana na wenzao wa Burundi waliowasili DR Congo mapema mwezi Agosti kwa oparesheni ya pamoja dhidi ya waasi.
Haijabainika iwapo Tanzania itapeleka wanajeshi.
Maafisa wa kijeshi wamekataa kufichua idadi ya wanajeshi waliohusika, wakitaja sababu za kiusalama na za kimkakati.
Wanajeshi wa Burundi kwa sasa wako Luberezi karibu na Bukavu huko Kivu Kusini.
Kikosi cha Kenya kitapiga kambi karibu na Goma huko Kivu Kaskazini na kitaongoza Kikosi cha Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rwanda pia ni mwanachama wa EAC lakini iliamuliwa kwamba isichangie jeshi la kikanda.
British Broadcasting Corporation