Kwa nini J.K. Kikwete hajawashukuru wapiga kura?

thereitis

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
297
41
Shukrani ni desturi ya binadamu baada ya kutendewa jambo jema. Mwaka 2005 tulishuhudia JK akipita sehemu mbalimbali za nchi yetu Tanganyika akiwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa rais wao; Pia alitoa ahadi nyingi zilizoashiria maisha bora kwa watanzania.

Baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha rais wa Tz kwa mara ya pili(2010-2015), JK hajapita maeneo mbalimbali ya nchi hii kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa rais wao kwa kipindi kingine cha miaka 5. Je JK kwa kutowashukuru wananchi anathibitisha tuhuma kuwa yeye na chama chake walichakachua matokeo ya kura za Urais?. Je bado JK anayo "Legitimate"(ridhaa) ya kuliongoza Taifa hili wakati hawezi kuwatembelea wananchi kwa lengo la kuwashukuru na kujua matatizo yao?
 
Atatushukuruje wakati hatukumchagua?? Anajua akipita kushukuru tutamwuliza unatushukuruje wakt hatujakupa kura zetu?? Mwiz toka lini akashukuru?
 
hivi mwizi atawezaje kuja kukushukuru eti kwa sababu amekuibia?c utamkamata?kikwete dhamira inamhukumu kwa uchakachuaji na uwizi uliomwezesha kuingia madarakani!hawezi kurudi kuja kushukuru wananchi maana atahukumiwa.hvi huoni leo hata mafisadi waliomwezesha amewakataa sembuse sisi wananchi!tujaribu kusoma alama za nyakati!
 
Aliwashukuru walimsaidia kumweka magogoni (TISS na Tume ya uchaguzi), na si wananchi wa Tanzania.
 
Alivyo msahaulifu! Ni vema umemkumbusha. Utaona anaanza kuzunguka na migari chungu tele mpaka mingine inang'oka matairi katikati ya safari.
 
Hakushukuru kwa lipi wakati alikupa fulana na kofia halafu ukamtosa, mpaka akaamua kukuzunguka kwa kutumia "Kalikuleita mpya" akaichukua "kula" . sema wenzako walikuwa wajaja waliamua kukesha na" kula" yao haikuguswa na sasa hivi hawalalmiki kuwa eti hajawatembelea, wewe ulivutiwa na usingizi kwa hiyo hacha kulalamika. Kalaga bahooo!
 
Kwa kuwa yeye anauhakika hakushinda uchaguzi kihalali, ameanza kuwashukuru wale wote ambao hawakumpigia kura. Juzi aliwaalika TUCTA ikulu, ameahidi nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi ambao alishazikataa kura zao. Tutegemee walioipigia kura wa cdm kuitwa ikulu muda si mrefu. Huyu mbayuwayu haeleweki.
 
hahahahahaha! KG umenchekesha!
Kwa kuwa yeye anauhakika hakushinda uchaguzi kihalali, ameanza kuwashukuru wale wote ambao hawakumpigia kura. Juzi aliwaalika TUCTA ikulu, ameahidi nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi ambao alishazikataa kura zao. Tutegemee walioipigia kura wa cdm kuitwa ikulu muda si mrefu. Huyu mbayuwayu haeleweki.
 
Back
Top Bottom