benghlasis
Member
- Nov 29, 2016
- 49
- 54
Satelaiti ndogo za upelelezi
Mwaka 1988, Israel ilirusha satelaiti yake ya kwanza ya upepelezi angani, na kuingia katika kundi la mataifa nane yenye uwezo wa kurusha satelaiti angani.
Hadi sasa nchi hiyo inaendesha zaidi ya satelaiti nane angani na kuipa uwezo mkubwa wa kukabiliana na tishio kutoka kwa mataifa kama Iran, ambayo inadhaniwa kwamba siku moja inataka kuunda bomu la kinyuklia.
Ndege zisizo na rubani, ama Drones
Inajulikana kama ndege isiyo na rubani ambayo inaweza kufika Iran. Heron TP ni ndege kubwa zaidi isiyotumia rubani ikiwa na bawa lenye urefu wa futi 85, sawa na ndege ya Boeing 737. Ina uwezo wa kukaa angani kwa masaa 24 na kubeba silaha zenye uzito wa tani moja.
Wakati nchi hiyo haisemi hilo wazi, Heron TP inasemekana kuwa na uwezo wa kurusha makombora kwenda ardhini.
Israel ni taifa la kwanza duniani kuanza kutumia drones katika mapambano ya kivita. Matumizi ya kwanza yalikuwa mwaka 1969 wakati iliporusha ndege hizo zikiwa na kamera kando ya mfereji wa Suez ili kuipeleleza Misri.
Drone aina ya Heron TP ikiruka nchini Israel.
Kifaru cha siri
Hadi leo, kifaru aina ya Merkava ni moja ya miradi ya siri kabisa ya nchi hiyo. Inasemekana kuwa huenda kikawa ni kifaru hatari zaidi duniani, na uundwaji wake kuwa ni muhimu – Uingereza na mataifa mengine yalikataa kuiuzia nchi hiyo vifaru. Mwaka 1970 ilianza kuunda vifaru vyake.
Aina mpya – inayofahamika kama Merkava Mk-4 – kinavutia zaidi. Kinaweza kufikia mbio ya kilomita 40 kwa saa na hufungwa ngao kulingana na aina ya operesheni ambayo kinaenda kufanya.
Kifaru cha Merkava wakati wa mazoezi na jeshi la Israel kaskazini mwa nchi hiyo. IDF
Mfano, katika eneo ambalo linafahamika kuwa na mabomu maalumu kwa ajili ya kulipua vifaru, ngao nzito hutumika wakati operesheni isiyokuwa na tishio la aina hiyo huhitaji ngao kidogo.
Mwaka 2012, kifaru cha Merkava kilifanyiwa mabadiliko makubwa – kwa kuwekewa mfumo mpya unaofahamika kama Trophy. Mfumo huu ni maalumu kwa ajili ya kulinda kifaru hicho na shambulizi lolote la kombora.
Makala kwa msaada wa Yaakov Katz (mwandishi na mhariri mkuu wa gazeti la The Jerusalem Post) na gazeti la Raia mwema.
~benghlasis