Kwa nini Israel ilimnyima Idd Amin ndege kuipiga Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Israel ilimnyima Idd Amin ndege kuipiga Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamayu, Oct 7, 2011.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Jamani ni kwa nini Israel ilikataa kumpa Idd Amin ndege za kisasa (wakati ule) ili kuipiga Tanzania mwaka 1972? Na kwa nini walifunga Ubalozi Tanzania au tulivunja mahusiano ya kidiplomasia na hao jamaa?
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Ubalozi wa Israel nchini Tz ulifungwa na Nyerere akipinga kukaliwa kwa palestina.
   
 3. kitonsa

  kitonsa JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Alikuwa muislam
   
 4. Nish

  Nish JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 732
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  na nyenyere alikuwa mgalatia mwenzao
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana. Msipotoshe hapa. Idi Amin mwaka 1972 hakuwa na jeshi la hewa. Baada ya kumpindua Obote aliwaita wanajeshi wote wa kikosi cha anga na waliokwenda akawaua. Waliosalimika baadhi walikimbilia Tanzania. Akaanza kujenga kikosi kipya. Amin asingekuwa na uwezo wa kuishambulia Tanzania wakati huo. Hata pale aliposhambulia Mwanza kwa mabomu mwaka 1973 ndege zake zilipita kwa mbali kwa sababu ya kuogopa kutunguliwa ndio maana mabomu yake yalianguka kwenye kisiwa cha Nane Nane.
   
 6. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Mkuu jasusi heshima mbele,kwanza asante kwa kuwahi kuweka sawa mambo hapa.lakini mpaka sasa uganda inaaminika kuwa na jeshi bora kabisa la anga afrika mashariki toka enzi za KjAR kuweka headquarter ya jeshi ka anga huko,sababu za kikosi kizima(na vifaa?) kuangamizwa ni ngumu kudhibitisha,hebu tusaidie kufafanua hili mkuu,wale wana jeshi la anga,kuuwa jeshi la anga mkuu! Imenistua kidogo.natangulisha heshima mkuu.
   
 7. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waisrael wenyewe walikuwa Taabani wakati huo. Walikuwa wanatagemea kila kitu kutoka kwa Bwana wao USA.
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wangemsaidije idd amin wkt yeye mwenyewe aliteka ndege yao?
  kuna makala inaonyeshwa NAT GEO channel kuhusiana na uvamizi
  wa makomandoo wa Israel ktk uwanja wa entebe kukomboa watu wao.
  kwa ufahamu wangu mdogo ndio hivo nijuavo hawakuwa na mahusiano mazuri.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Uganda had the best air force in East Africa. Shule ya marubani wa ndege naturally ilikuwa Uganda. Lakini baada ya Amin kumpindua Obote hakuwaamini kabisa wanajeshi wa kikosi cha anga kwa hiyo akafanya njama kuitisha mkutano. Wote waliokwenda waliuawa. Waliobaki waliweza kutorokea Tanzania. Hebu jiulize wakati wa vita vya Kagera kwa nini Amin hakutumia ndege zake kutushambulia? Na huyu ndiye aliyekuwa anatishia kuwa atateka eneo la Tanzania hadi Tanga. Ndege zake zilikuwa hazifanyiwi matunzo tena kwa sababu most of the senior and experienced pilots had been killed. Soma kitabu cha David Martin "Idi Amin" analizungumzia kwa kirefu suala hilo.
   
 10. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mwongozo naomba tusijadiri mada hii kwa kutumia movie(film) ya Kagera War,The last king of Scotland etc Amin hasingepata kupata msaada kutoka toka Israel kwani aliwachukia wao watu kama alivyokuwa Hitler.Hiyo ni moja,lakini ata Amin mwenyewe alijua vizuri kuendesha ndege za kivita hapo hatujui kwanini yeye hakuendesha ndege kuja kukomboa ardhi yao ya Kagera.Je unajua Uganda ni mojawapo ya nchi ambazo zilikuwa zimependekezwa kuwapokea wana Israel?
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  vita ya iddi amini ina mambo mengi ya kushangaza....

  kwanza tanzania haikupata sapoti kutoka israel wala uingereza wakati nchi hizo

  zilikuwa na uadui na iddi amini.....

  hatukupewa 'baraka za kumpiga iddi amini ' na UN wala OAU......

  kuna mtu anaitwa NOLAN...huyu jamaa aligeuka milionea kwa ajili ya vita hivi....

  ndie alimuuzia nyerere silaha.....na akabaki nchini kuendelea na biashara zake...

  alikuja kuoa mdada wa kinigeria aliyefungua duka la nguo lilikuwalinaitwa CONIE OF DAR pale Sheraton...now sijui inaitwa movenpick...sijui...
   
 12. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hawakuwa taabani-mwishoni wa mwaka 1972 walikuwa wanapigana vita
  then swala la wao kusaidiwa na USA kipindi hicho naweza sema lilikuwa kwa percent ndogo sana
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Nchi yenye jeshi bora la anga kwa dunia ya sasa ndio tishio zaidi.tumeshuhudia wamarekani wameshinda vita vingi kwa kutumia sana jeshi la anga hivyo kuwaachia kazi ndogo sana askari wa miguu.Waganda wanasifika sana kwa ubora wa jeshi la anga na kama kweli wanacho mpaka chuo lazima tukubali wanaweza kuwa superpower kijeshi Afrika Mashariki na kati,nafikiri ule ushindi wetu mwaka 79 usitudanganye,Museveni amejenga jeshi bora sana na bajeti yake ya jeshi ni kubwa kupitiliza hadi mataifa ya nje kupiga kelele.sisi ndio hao tunanunua helcopta feki zinadondoka hovyo! Sijui kama kuna operation gani kubwa na ngumu ukitoa vita vya kagera tunayoweza kutumia kupima uwezo wetu kijeshi nyakati hizi.tafadhali tusitaje ya commoro,kule hata mgambo wa jiji wangeshinda tu!
   
Loading...