Kwanini hospitali zina mchoro na picha ya nyoka?

Sasa mkuu hizo ni story ndani ya kitabu cha Biblia Tuna uhakika gani kuwa siyo hadithi kama hadithi zingine??? Tuna uhakika UPI wa kuamini yaliyopo ndani ya Biblia ni ukweli na siyo story za kutunga???
 
Kasome kitabu cha Hesabu 21:4-9 juu ya safari ya wana wa Israel.

Muhimbili Hosp wanaitumia sana nembo hiyo.
Siyo mhimbili tu sehem nyingi Sana sasa Tuna uhakika gani na story ya Hes 21:4-9 kuwa siyo story kama story zingine??
 
Siyo nyoka ni mnyoo na hiyo fimbo iliweka ili mnyoo ufuate fimbo. Hayo maelezo niliwahi kuyasikia kutoka kwa daktari wa muhimbili
Mkuu Hayo maelezo ya huyo Dr hukumuuliza sasa mnyoo ukifuata fimbo ndo inakuaje labda
 
Habari zenu wana Jamvi.
Nimefuatilia sana hili swala na nimeamua kuomba msaada na majibu,kwa wale wanaoiamini Biblia ktk historia ya Kuumbwa kwa Adamu na HAWA kiumbe huyu Nyoka ndiye aliyetumiwa na shetani kumdanganya HAWA na baadae Adamu na hivyo wakaingia ktk Dhambi na Mungu akaweka Uadui kati ya uzao wa Nyoka na mwanadamu hivyo Nyoka ni Adui wa mwanadamu, Sasa Hospitals na sehemu zingine za kutolea Huduma za Afya ni sehemu tunazokuwa na matumaini ya kupata uponyaji.sasa kwa nini kuna hii picha au mchoro wa huyu kiumbe Nyoka?? Nani mwanzilishi wa Nembo hii ya nyoka na ilianza kutumiwa wapi na maana halisi ya nembo ya kiumbe huyu ni nini?

Naombeni majibu na ufafanuzi AhsanteniView attachment 501467

Pia kuna miungu ya kiyunani na kigiriki kwenye michoro inaonekana inebeba fimbo zenye nyoka kwa kukujuza zaidi majina ya sayari ni majina ya miungu ya kigiriki upende usipende hata uwe mlokole utaitukuza hii miungu bila kujua
 
Pia katika historia ya binadamu inaonyesha katika viumbe vya porini ni nyoka ndio mwenye utambuzi wa miti au mimea ambayo ni dawa.

Mathalani nyoka akipata kadhia ya majeraha yanayiweza mpotezea uhai wake aidha yeye au wenzake hutafuta miti au majani ambayo ni dawa na kujitibu au kumtibu nyoka mwenzao.

Pia kama mdau alivyosema hapo juu, ukisoma biblia fresh, historia ya waizraeli kuna kipindi walipona kwa kumuangalia nyoka wa shaba aliewekwa kwenye fimbo ya musa kama sikosei, hivyo walipohingwa nyoka tu, wakiangalia hiyo fimbo walipona.
Sasa mkuu kama nyoka ni Genius kiasi hicho kwa nini wasitumiwe kutafuta Dawa za magonjwa sugu kama Ukimwi na Saratani??? Yaani nyoka anaambukiwa Ukimwi Then Anakuwa karibu na nyoka wengine na Akikaribia kufa wenzake lazima wataenda pori kutafuta Dawa then wanamfuatilia kimya kimya na kumfanyia surveillance hadi kwenye hiyo dawa watakayomleta mwenzao na tayari Dawa ya Ukimwi inakuwa imepatikana kupitia huo MTU utakaoenda kuchumwa na Nyoka wenzake
 
Pia kuna miungu ya kiyunani na kigiriki kwenye michoro inaonekana inebeba fimbo zenye nyoka kwa kukujuza zaidi majina ya sayari ni majina ya miungu ya kigiriki upende usipende hata uwe mlokole utaitukuza hii miungu bila kujua
Aiseee kumbe tunavyopita hapo getini Tunaabudu hiyo miungu bila kujua???
 
Mtaani kwetu wananikoma aiseee...wananiita mi mtaalam wa kila kitu kumbe nakuja huku nazoa maujanja bureeee then naenda kumwaga mavitu. Jamsn JF idumu milele
Wote tuseme aaameni.
Hahahahahah sawa dk machale
 
Habari zenu wana Jamvi.
Nimefuatilia sana hili swala na nimeamua kuomba msaada na majibu,kwa wale wanaoiamini Biblia ktk historia ya Kuumbwa kwa Adamu na HAWA kiumbe huyu Nyoka ndiye aliyetumiwa na shetani kumdanganya HAWA na baadae Adamu na hivyo wakaingia ktk Dhambi na Mungu akaweka Uadui kati ya uzao wa Nyoka na mwanadamu hivyo Nyoka ni Adui wa mwanadamu, Sasa Hospitals na sehemu zingine za kutolea Huduma za Afya ni sehemu tunazokuwa na matumaini ya kupata uponyaji.sasa kwa nini kuna hii picha au mchoro wa huyu kiumbe Nyoka?? Nani mwanzilishi wa Nembo hii ya nyoka na ilianza kutumiwa wapi na maana halisi ya nembo ya kiumbe huyu ni nini?

Naombeni majibu na ufafanuzi AhsanteniView attachment 501467
mshana jr
uwanja wako
 
Hii alama ina historia ndefu na ya kusisimua, hasa ukifuatilia historia za wanaohusishwa na alama yenyewe. Asili yake imetokana hasa kutokana na mungu wa Kigiriki anayeitwa Asclepius, lakini inahusishwa pia na hadithi ya Musa kwenye Biblia. Ipo hivi:

1. Fimbo ya Asclepius (Rod/staff of Asclepius)

Kwa mujibu wa hadithi na imani za wagiriki (Greek mythology), mungu Asclepius alikuwa anashika fimbo kama hiyo yenye nyoka. Mungu huyu ndiye anayehusika na uponyaji/dawa/udaktari. Ni alama ambayo imekuwa inatumika muda mrefu sana na inatambulika vizuri na yeyote aliyesomea udaktari/uuguzi. Alama hii ipo pia kwenye bendera ya World Health Organization (WHO).

320px-Flag_of_WHO.svg.png


Mwanzoni mwa miaka ya 1900, jeshi la Marekani likaanza kutumia alama nyingine yenye nyoka wawili, fimbo/fito na mbawa juu, ambayo imekuwa ikitumika kimakosa (Caduceus, angalia hapa chini). Caduceus ina maana tofauti kabisa na hii ya nyoka mmoja. Caduceus ni alama ambayo asili yake ni mungu Hermes (ugiriki), ambaye yeye alikuwa anahusishwa zaidi na uwakala wa miungu na muunganishi wa ulimwengu wa wafu/roho. Hermes anafahamika zaidi kwa huo uwezo wake wa kuingia na kutoka kwenye ulimwengu wa roho/wafu na kusaidia wale wanaokata roho au wanaotaka kufa waingie kwenye ulimwengu wa wafu/roho bila shida pamoja na mambo mengine mengi. Alikuwa anafahamika pia kwa mambo mengi, ikiwemo udanganyifu wa kujibadilisha ili kuwazuga miungu wenzie ilimradi tu afurahi mwenyewe. Baadae, Warumi walimuhusisha Hermes pamoja na hiyo alama yake na mungu Mercury, ambaye alikuwa ana tabia za kufanana. Kwa hiyo, popote utakapoona hii alama ya Caduceus inatumika na taasisi ya tiba, jua kuwa hawajasoma historia vizuri.

Alama zenyewe hizi hapa:

snakesformedicine.png


Sanamu ya mungu Ascelipus:
256px-_Asklepios_-_Statue_Epidauros_Museum_2008-0.jpg


Sanamu ya Mungu Hermes:
219px-_Hermes_Ingenui_Pio-_Clementino_Inv544.jpg


2. Hadithi ya Musa kwenye Biblia, kitabu cha Hesabu, mlango 21, mstari wa 4 hadi wa 9:
4. Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. 5. Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. 6. BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. 7. Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. 8. Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. 9. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Nadhani hiyo ya hadithi ya Musa kwenye Biblia inajieleza vya kutosha.
Nafikiri kwa maelezo uliyotoa Fimbo ya Asclepius ndo ukweli na uhalisia wa Alama hii ktk sehem zinazotoa Huduma za Afya Ila Historia ya Fimbo na nyoka wa shaba Imeingizwa maksud ili kuwapotosha Wakristo na kuwavuta japo hawamaanishi Hbr za Musa
 
Ile ya muhimbili ni mnyoo (una historia yake na research, kasome) sio nyoka,,

Ila machame hospital nliona wanatumia nyoka na fimbo- hii nahis inahusiana na biblia
Unaweza tupatia hiyo historia ya huo mnyoo wa mhimbili au tukasome wapi kupata habari hiyo??
 
Mtaani kwetu wananikoma aiseee...wananiita mi mtaalam wa kila kitu kumbe nakuja huku nazoa maujanja bureeee then naenda kumwaga mavitu. Jamsn JF idumu milele
Wote tuseme aaameni.
duh!haya bana wasalimie idodi
 
Nyoka ndiye mnyama mwerevu kuliko wote duniani basi hiyo alama itakuwa inamaanisha kuwa hospitali inatumika akili na werevu zaidi kufanya uponyaji.
 
Back
Top Bottom