Kwanini watumishi wa Halmashauri wana nyodo sana tofauti na watumishi wa Wizara?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!!

Wiki hizi mbili tatu nimekuwa busy sana na kuzunguka kwenye hizi taasisi za kiserikali.

Katika mizunguko yangu nimejifunza kwamba hawa watumishi wa halmashauri ni viburi,nyodo nyingi tofauti kabisa na wale watumishi wa ofisi za wizara.

Kibaya zaidi unaenda ofisi za halmashauri unakikuta kidada kiba sura mbaya lakini kina nyodo kibajifanya kijuaji wakati hakijui hata mtu anayemuongelesha ni nani.

Ila ukifika wizarani kuna heshima ya hali ya juu kwa watumishi wake,sio siri kuna tatizo la kimfumo kwenye hzi halmashauri zetu ziangaliwe upya.
 
Huko ndio zilipo PhDs.
kumbe hawa kenge wa halmashauri ni cheti na diploma tu.Maana kuna mjinga mmoja nilikuwa najaribu kumweleza jambo fulani jinsi anavyojieleza nikaanza pata mashaka kwamba alisoma chuo gani harafu anajiita mtaalamu😂😂
 
Ni kweli, wanakuaga na nyodo sana hasa ofisi ya UTUMISHI, hao wanaoitwa maafisa Utumishi wanajionaga Miungu flani, wana dharau sana.
 
Tatizo mnakuwa humble sanaa...

VAA KAUNTA SUTI
fika pale saini getini kama AFISA MAALUMU

sura mbuzi hucheki na mtu ,mwambie una shda na mkuu wa kitengo(ambacho anahusika na shda yako)

ukiuulizwa una shda gani?
mjibu una maelekezo maalum kutoka mamlaka Teuzi .

utapokelewa na begi lako na kusindikizwa juu


FANYA HIVYO AFU URUDI HAPA.
 
Tatizo Halmashauri nyingi zimeajiri wazawa sijui huwa ni swala la ki mfumo au ni ajali tu. Hii inachelewesha sana maendeleo na mambo mengine
 
Back
Top Bottom