kwa nini hatuwezi kutumia Kiswahili Ipasavyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini hatuwezi kutumia Kiswahili Ipasavyo?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kigarama, Oct 12, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Napenda sana kusoma yale tunayoandika humu JF (Pamoja na mabandiko yangu) na wakati mwingine hujipa muda wa kutafakari kama kweli sisi kama ndiyo wahifadhi na wamiliki halali wa Lugha ya kiswahili tunaijua lugha yenyewe Ipasavyo.

  Kuna toafuti kubwa sana kati ya Maneno, sentensi, na mtumizi sahihi ya Lugha. Kuna wakati unaweza kusoma bandiko la mtu hadi unafikia hitimisho kwamba inawezekana mwandishi wa bandiko hilo anadhani kila neno huunda sentesi na kila sentensi hutengeneza aya inayoeleweka.

  Wakati mwingine kunakuwa na sentensi nyingi zinazounda aya isiyo na muunganiko, msawaziko, mtiririko wa wazo, uwiano wa hababri yenyewe na mwisho wa siku hata kusudio la mwandishi halieleweki. Ndani ya hayo yote mwandishi anatumbukiza maneno ya Kiingereza au ya mitaani bila ya kuonyesha kwamba maneno hayo si sehemu ya Lugha Rasmi iliyotumika kwenye uandishi wake.

  Wakati mwingine hata matumizi sahihi ya herufi ua maneno hakuna. Nadhani ni wakati sasa hapa JF tuwe mfano wa matumizi bora ya Lugha yetu ya Kiswahili. Mdharau chake Mtumwa!!
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kiukweli hata mimi kiswahili kinanipa shida my dear
  anzisha darasa
   
 3. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama mtu anapokuwa anachanganya maneno mfano; kiswahili na kingereza anakuwa anadharau lugha,
  na ndio maana kiswanglish kikaruhusiwa kutumika kwa mawasiliano ya kawaida.
  Iko hivi - sehem nyingi - maofisini na mashuleni; kingereza kimekuwa kikitumika kama 'a medium of communication', na kwasababu nzuri tu kwamba tunafanya kazi/tunasoma na foreigners sasa ili kila mtu aeleweke tunatumia kingereza, wakati huo huo kiswahili ndio mother language na ndio lugha ambayo wengi wetu tunaitumia mtaani, nyumbani etc.

  Now mtu anapokuwa anachanganya lugha muda mwingine ukute ni kwasababu ya ile kutumia lugha mbili muda wote, ni kawaida sana, sio kudharau but mazoea. Japo mi binafsi nimepokea ushauri wako! asante sana!
   
 4. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Smiles kwenye uandishi unapotumia maneno yasiyo Rasmi au si ya lugha unayotumia kuandika, basi bila shaka unatakiwa kuonyesha kwamba hiyo lugha unayotumia umeiingiza tu labda kwa mazoea au kwa kushindwa au kukosa msamiati wake. Ingawa uandishi mamboleo umejikita sana kwenye dhana ya "Lugha ni ujumbe unaoeleweka bila kujali ujumbe huo unatolewa katika Lugha fasaha au sanifu kiasi gani""

  Uandishi huo mamboleo ndiyo umetapakaa kwenye mitandao pendwa ya kijamii hadi kuwatia hofu magwiji wa Lugha duniani, kwamba inawezekana lugha pamoja na uandishi murua na Jadidi vikapiga hodi kuzimu siku si nyingi badala yake Lugha Upogo zikatamaliki kwenye jamii yetu.

  Kuchanganya lugha kusikoweza kuleta mantiki huifanya habari inayotolewa kuchusha au kupoteza maana. Elewa lugha ni kama chakula. Haitoshi tuu kuwa na vitu vyote vinavyotakiwa kupika pilau lakini mpishi akawa hajui kama viungo vya pilau hutiwa mwanzoni au mwishoni mwa upishi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo unaongelea kwenye 'official communications' au haya maongezi yetu humu ya kawaida?
  Kwa maana kama ni humu ndani sidhani kama hicho ni kitu unaweza ku-control!
  Unaweza kuwa cautious ukiwa ofisini but kama na huku tena mtu anatakiwa kuwa cautious na lugha naona kama its going to be too stressful....!
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Smiles nazungumzia ya humu sizungumzii yale ya Ofisini kwani hayo ni magumu zaidi. Hebu fikiria umependa kichwa cha habari fulani halafu unaingia ndani unajiuliza "huyu naye alitaka kusema nini?" sizungumzii sarufi ndugu yangu nazungumzia lugha tunazotumia kuwasilisha hoja zetu.

  Kama mtu hajui tofauti ya M-Puuzi na M-jinga si anakera?? hivi **** na Zebe ni sifa zinazofanana na kulingana!?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Wanabodi lugha yetu ya Kiswahili ni nzuri na tamu. Tujitahidini isitutoke, maana imekuwa mazoea kuchanganya kiingereza na kiswahili. Itafika wakati tutaipoteza lugha yetu. MDHARAU KWAO MTUMWA.
   
 8. chamlungu

  chamlungu JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Ni kweli lugha yetu ya Kiswahili ni nzuri. Wengi wetu tuna upungufu wa misamiati na matumizi sahihi ya maneno na alama. Tuendelee kujifunza.
   
 9. O

  OMARY2012 Senior Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni kwasababu hatuna sera ya lugha Tanzania ambayo inatuongoza kukifanya Kiswahili kitumike katika nyanja zote za mawasiliano. Nafikiri wakati umefika sasa Kiswahili kitumike hata kufundishia Elimu ya Sekondari na Elimu ya juu. Huwezi kufikiri kwa kiswahili halafu ukajieleza kwa lugha nyingine ukategemea kupata maendeleo ya jambo ulilofikiria. Tuige wenzetu wajapani, wachina, warusi na nchi zote zilizoendelea wanatumia lugha zao. Kiswahili kikipewa nafasi yake hapa Tanzania basi kila mmoja wetu atajifunza kuongea lugha fasaha.
   
 10. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  jamani walimu wetu toka msingi hadi sekondari wanachanganya lugha nyumbani wanachanganya lugha unategemea mtu huyu ataongea lugha iliyo safi kati ya hizo. wakati mwingine sio kupenda tunalazimika kufanya hivyo kwa kusoka kuwa kamili katika moja ya lugha hizo. unakuta mtu kiukweli hana msamiati anaamua kutumia mwingine katika lugha nyingine.
   
Loading...