Kwa nini hata wanawake hutumia majina ya viungo vyao nyeti kutukana!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini hata wanawake hutumia majina ya viungo vyao nyeti kutukana!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gosbertgoodluck, Mar 12, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Jamani kama kuna jambo linalonikera basi ni hii tabia ya kutumia majina ya viungo nyeti vya wanawake kutukana. Utakia mtu bila aibu mbele ya hadhara anamtukana mwenzie eti k.... mamako. Ajabu ni kwamba kuna wakati nilimsikia dada fulani akimtusi mvulana kwa tusi hilo hilo!! Hivi ni kwa nini tunawadharirisha mama zetu kiasi hiki!? Kwa kweli hii ni laana tena laana kubwa sana!
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160


  Ubarikiwe sana kwa kutuheshimu asubuhu yangu imekuwa njema  The Following User Says Thank You to Gosbertgoodluck For This Useful Post:

  Dena Amsi (Today) ​
   
 3. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  asante kwa kuliona hilo,,,barikiwa sana
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ni kweli inakera. nafikiri wanatumia viungo vya mama kutokana na sensitivity yake. ikitokea mwanamke na mwanaume wanatemea uchi, ni most likely kuwa kwa mwanamke watu watakuwa sensitive zaidi. ndio maana hata mwanaume atembee kifua na mapaja yote nje, hutasikia mtu anatia neno, ila iwe hivyo kwa mwanmke, utasikia hata watu wakisema "ana laana huyu"!

  kwa kuwa tusi ni neno linalotamkwa kwa lengo la kuudhi au kuumiza roho, basi atukanaye huchgua hapo kwenye viungo vya wakina mama kwani ndipo sensitive zaidi na mtu yoyote anayejiheshimu na kumheshimu mama yake hataweza kuvumilia si tu kuona, kushika nk kiungo cha mama yake, bali hata kusikia kikitajwa. nafikiri hata daktari akijikuta anatakiwa kumtibu mama yake sehemu hizo, itabidi kutafuta msaada wa daktari mwingine

  Glory to God
   
 5. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kwa hilo nakubaliana nawe, pili maumbile ya mwanamke na ya mwanaume hayafanani kwa mvuto! Tumeona maumbile mengi ya wanawake na wanaume ukitukanwa kwa kiungo cha mwanamke then uvute picha ilivyo lazma utaghadhibika tofauta na yakiume!
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hivi hayo matusi mengine yaliyobaki sijui maana zake nini.
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii ni dunia nzima huko america hutumika "Mother F*c*er" kwa wanaume na wanawake
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi bado nafikiri kuwa hiyo ni laana tu. Kimsingi, hakuna binadamu ambaye hajazaliwa na Mama. Hata Bwana na Mwokozi Yesu Kristo alizaliwa na Mama. Sasa inakuwaje lile eneo tulilopita sote wakati wa kuzaliwa litumike kama tusi la kumuudhi mwenzio!! Wanadamu tumefika mahali tunakejeli uumbaji mtakatifu wa Mungu!! Ndiyo maana magonjwa hatari yanaendelea kutugaragaza na tusipobadilika tutaangamia kabisa.
   
 9. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  K...mamake walahi hata mimi hiki kitu kinanikela sana
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :A S 13::crazy:
  :A S 13:
  :crazy:
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye bold, nadhani unaikimbia homework yako kaka.

  ni kweli inamkera kila mtu, kusema ni laana pekee, haitoshi, labda utuambie nani alimlaani nani hadi matusi yanayoaminika kuwa makali na ya kuudhi zaidi yakaelemea huko kwenye kiungo cha mama. hata kusema wote tulipita hapo haitoshi, najua wengine hasa waliozaliwa kwa mikasi ya upasuaji hawakupita. labda ungetumia maziwa ambayo wengi wamenyonya, ila pia wengine hasa waliopoteza wazazi wakati wa kuzalia hawakunyonya nk. lakini hata kwa hayo bado uatakuwa umekimbia homework yako. pia kumbuka kuwa tusi ni socially defined na linategemea hisia za atukanae na atukanwae

  umedadisi sababu na inakuwaje na maoni ndio kama hivyo kuwa source ya haya matusi kumuelemea mama yaweza kutazamwa kiantropolojia zaidi na hapo hutakwepa suala la fermine sensitivity.

  fikiria hivi, kati ya mwanume na mwanamke, nani sensitive zaidi ya mwingine, ukipata jibu mwnamke, jiulize tena hivi, katika mwili wa mwanamke ni sehemu gani sensitive kuliko nyingine, halafu jiulize tena katika wanawake wote nani sensitive zaidi kwako ukipata jibu kuwa ni mama yako, basi hutoshindwa kuelewa how sacred is this organ, hasa iliyo kwenye mwili wa mama yako na kwa nini ntu anayetaka kukudhi atakutukania hilo.

  ni kama vile mtu anayekufuru dini fulani ili kuwaudhi waamini wa dini ile, hupenda zaidi kukufuru fundisho kuu la imani na sensitive ya dini nyingine na sio mafundisho madogo madogo

  haya mambo yana mizizi yake katika saikolojia na hayakutokea kwa nasibu bali yametokana na mchakato wa kiantropolojia

  nafikiri sasa umenielewa.

  Glory to God
   
 12. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uchambuzi murua. Bila shaka umeeleweka tena vizuri sana.
   
 13. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Nikimnukuu Notorius BIG akilaumu akisema "Shit my mama got kid in the west" hii nayo ilitokana na mama yake kutumia hicho kiungo.
   
 14. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Asilimia kubwa ya Binadamu wana utamadumi wa kuwapenda na kuwaheshimu Mama zao zaidi kuliko Baba zao kwa kuwa huwa kuna true love kati ya mama na mwana pasipokujali jinsia. Ili umkere zaidi adui yako ndo maana watu hu-opt kumtukana mama wa adui ili achukie zaidi.
  Ukichunguza utagundua kwamba hata reaction ya mtu aliye karibu zaidi na mama yake anapotukanwa ni tofauti na ambaye hakupata bahati ya kuwa karibu na mama katika kukua kwake. Huyu aliyejaaliwa kuwa karibu na mama anaweza hata kukuua ukimtukania mama.
   
 15. GodfreyTajiri

  GodfreyTajiri JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 846
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 60
  kwani viungo hivyo vinapotumiwa kusifia haikeri?
  msisahau watu hutumia viungo hivyo hivyo kusifia
   
 16. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Ku.... mamake walakhi mijitu inayopenda kutukania viungo vya mama zetu huwa inaniudhi kweli yaaani basi tu nashindwa uwezo wa kuiangamiza ipotee kwenye uso wa dunia hii.
   
Loading...