Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Kwanza kwa wasiofahamau Mji wetu wa Dar ulijengwa kwa kufuata mfumo wa apartheid, Wajerumani waliupanga hivyo yaani maeneo ya Wazungu (Oysterbay, Msasani), ya Wahindi/Waarabu (Upanga, na maeneo ya Posta ya leo) na Uswahilini kwetu ambapo ni maeneo ya Magomeni, Temeke, n.k. Waingereza walivyokuja wakaendleza hivyo na tulivyopata Uhuru ikabakia kuwa hivyo isipokuwa Wazungu weusi wakaondoka Uswahilini na kuhamia Oysterbay kwenye Nyumba zilizoachwa na Wazungu!
Sasa wakati wa Utawala wetu na sisi tukaanzisha maaneo yetu mapya kama Sinza, Mwenge, Tabata na udosini kama Mbezi beach n.k. lkn labda kibaya zaidi na kinachosikitisha tumeurithi na kuukubali mfumo wa Apartheid ulioanzishwa na Mzungu na kuendelea kuutumia hata Dodoma tumeanzisha Uzunguni, Uhindini na Uswahilini kwanza nchi nzima utakuta hivyo kuna Uzunguni, Uhindini na mwishoni mkunduni mwa Dunia ndiyo Uswahilini kwetu!
Sasa swali langu ni kwa nini sisi ndo tunataka kwenda kuishi Upanga kwa Wahindi lkn hakun Muhindi anayetaka kuja kuishi Sinza kwetu?
Bila ya kuelewa Historia yetu ya tunakotoka hatuwezi kufanikiwa kwenda mbele kamwe tutapiga maki time hapa hapa tu, nashauri tufute mara moja Uzunguni, Uhindini na Uswahilini, hasa kwenye maeneo yetu mapya, ...