Kwa nini elimu bure inawezekana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini elimu bure inawezekana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rugemeleza, Oct 13, 2010.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii makala imekaa kisomi na ni jibu la wale wasiowapenda watoto wetu.

  [​IMG]


  Kwa nini elimu bure inawezekana?

  [​IMG]


  Dk. Kitila Mkumbo
  CHANZO: Kwa nini elimu bure inawezekana?

  Dk. Kitila Mkumbo

  TANGU kuanza kwa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010, kumekuwa na mjadala mahsusi kuhusu sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya chekechea hadi kidato cha sita.

  Sera hii imepingwa na kuzomewa vikali na Chama cha Mapinduzi (CCM). Binafsi awali sikutilia manani upinzani wa kutoa elimu bure kwa sababu ulitolewa na Kampeni Meneja wa chama hicho, Abdulrahmani Kinana, nikidhani kwamba alifanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kipropaganda ukizingatia kwamba vyama vya siasa viko katika ushindani mkubwa wa kuomba ridhaa ya wapiga kura.

  Hata hivyo, nimeanza kutilia manani upinzani huu baada ya Rais Jakaya Kikwete naye kujitokeza hadharani kupinga sera hii na kuungwa mkono na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Upinzani wa sera hii kutoka kwa viongozi hawa wakuu katika nchi yetu umetia uzito wa kipekee hoja ya kwamba elimu bure haiwezekani kutolewa katika nchi maskini kama Tanzania.

  Bila kufafanua dhana ya kutoa elimu bure na uwezekano wake, wananchi wataanza kuamini kwamba hili ni jambo lisilowezekana hasa watapoambiwa na viongozi wa chama tawaka na serikali yake. Ufafanuzi huu ni muhimu ukizingatia kuwa tupo katika jamii ambayo imejengwa katika mfumo wa kipropaganda wa kuamini au kuaminishwa kuwa chochote kinachosemwa na viongozi wa serikali na chama tawala kuwa ni kweli.

  Aidha bado kuna watu katika jamii yetu ambao hutilia shaka chochote kinachosemwa na viongozi wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine, bila kuzingatia mantiki ya hoja.

  Pengine kabla ya kufafanua juu ya uwezekano wa kutoa elimu bure, ni vizuri kuweka kumbukumbu sawa. CCM wana historia ya kupinga sera zenye kujaribu kuwapunguzia wananchi makali ya maisha, na hawajaanza na hili la elimu bure.

  Itakumbukwa kuwa mwaka 1995 wapinzani waliahidi kufuta kodi ya kichwa (CCM waliita kodi ya maendeleo) ambayo ilikuwa inaleta adha kubwa kwa wananchi hadi wengine kufikia hatua ya kujificha porini ili wasikamatwe na askari mgambo.

  CCM walipinga vikali sera hii wakisema kuwa haiwezekani kuendesha serikali bila kodi hiyo. Hata hivyo, baada ya uchaguzi mkuu wa 1995 serikali ya CCM iliifuta kodi hii, aghalabu kwa shinikizo.

  Mwaka 2000 wapinzani walikuja na sera ya kufuta ada katika shule za msingi kama njia ya kuwawezesha watoto wengi zaidi kujiunga na elimu ya msingi. Kama kawaida yao, CCM walicharuka tena wakidai kuwa wapinzani wanaota ndoto.

  Hata hivyo baada ya uchaguzi wa 2000 ada katika shule za msingi ilifutwa, japokuwa kwa shinikizo kubwa la Benki ya Dunia. Kwa hiyo, kwamba CCM leo hii wanapinga vikali tena bila aibu sera ya elimu bure sio jambo la kustaajabu.

  Pengine jambo pekee la kustajaabu ni kwamba wapinzani wa sera ya elimu bure ni viongozi wa chama kinachojiita cha kijamaa. Haingii akilini hata kidogo kwa kiongozi wa chama kinachojiita cha ujamaa kupinga sera ya kutoa elimu bure. Msingi wa ujamaa ni usawa na fursa kwa wote.

  Wana ujamaa popote walipo wanakubaliana kwamba njia rahisi ya kufikia usawa na kutoa fursa kwa kila mtu ni kuhakikisha kwamba elimu na huduma zingine za jamii zinamfikia kila mtu. Ili kutimiza hili, wana ujamaa wanakubaliana pia kwamba ni muhimu na lazima kwa huduma hizi kugharamiwa na serikali bila wananchi kuzilipia moja kwa moja.

  Hii ni mantiki ya msingi ya ujamaa ambayo mwanachama wa kawaida wa chama kinachojiita cha kijamaa anapaswa kuielewa, achilia mbali kiongozi wake.

  Wapinzani wa sera ya kutoa elimu bure wametumia kigezo cha gharama katika kuhalalisha upinzani wao. Kwamba haiwezekani kutoa elimu bure kwa sababu kufanya hivyo itamaanisha serikali iache kutekeleza majukumu mengine ya msingi.

  Katika makala hii ninaonyesha kwa ufupi sana jinsi ambavyo inawezekana kwa serikali kulipia gharama ya elimu kwa kutumia fedha za walipa kodi bila kumbebesha mzazi gharama za ziada.

  Katika kufanya hivi nitaenda hatua kwa hatua, nikianzia na kufafanua dhana ya elimu bure kwa mazingira ya Tanzania, na kubainisha vyanzo mbadala vya mapato kwa serikali ili iweze kulipia kikamilifu gharama za elimu na huduma zingine za jamii. Elimu bure maana yake ni nini?

  Watu wengi wanaopinga mpango wa CHADEMA wa kutoa elimu bure wamefanya hivyo bila kuelewa sawasawa nini hasa mantiki yake katika mazingira ya Tanzania. Nitafafanua.


  CHADEMA inapoongelea kutoa elimu bure inamaanisha kufuta ada zote wanazotozwa wazazi katika shule za sekondari. Tayari wanafunzi wa shule za msingi hawalipi ada na kwa hivyo kinadharia elimu ya msingi inatolewa bure Tanzania. Hivyo basi, katika kujibu swali la je inawezekana kutoa elimu bure ni muhimu kukokotoa mahesabu ya ada wanazolipa wanafunzi.

  Hii itatupa picha halisi ya fedha ngapi zinakusanywa kwa malipo ya ada na ni kiasi gani cha mapato serikali itapoteza kwa kufuta ada hizo. Ukishamaliza kukutoa katika hatua hii ni muhimu vilevile kuonyesha vyanzo vya mapato mbadala vitakavyoziba pengo hili. Katika aya zifuatazo nitajaribu kukokotoa mahesabu haya.

  Ada ya shule ya sekondari kwa sasa ni shilingi 20,000/= kwa shule za kutwa na shilingi 70,000/= kwa shule za bweni. Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 35 ya wanafunzi wa sekondari wanaacha shule kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kwa wazazi wao kushindwa kulipa ada.

  Kuna taarifa kutoka baadhi ya wilaya ambapo wazazi na walezi waliwashauri watoto wao wasifanye vizuri katika mitihani ya darasa la saba ili wasiingie katika matatizo ya kulipa ada kwa kuwa hawana uwezo. Hiyo ndiyo athari ya ada katika shule za sekondari hapa nchini.

  Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo za mwaka 2010, idadi ya wanafunzi katika shule za sekondari za serikali ni 1,401,330. Katika shule zaidi ya 2000 nchi nzima, shule za bweni zipo 170 zenye wanafunzi wasiozidi 120,000.

  Hii inamaanisha kuwa kwa mwaka serikali inakusanya takribani shilingi bilioni 25.6 ikiwa ni ada kutoka kwa wanafunzi wa kutwa na takribani shilingi bilioni 8.4 kutoka kwa wanafunzi wa bweni. Kwa hivyo, serikali inapata jumla ya shilingi bilioni 34 ikiwa ni mapato yatokanayo na ada ya wanafunzi katika shule za serikali, na hii ndiyo pesa ambayo serikali itaikosa kwa kutekeleza sera yake ya elimu bure.

  Kama serikali itafuta michango mingine yote ambayo wazazi wenye watoto katika shule za sekondari wanalipa italazimika kuongeza bajeti yake kwa ajili ya shule za sekondari kwa kiwango cha shilingi takribani bilioni 40. Hii ndiyo kusema kuwa gharama ya kutoa elimu bure, kwa maana ya kumuondelea mzazi mzigo wa ada na michango mingine, ni shilingi zisizozidi bilioni mia moja (bilioni 100) kwa mwaka!

  Swali ambalo wenzetu wapinzani wa sera hii wanauliza ni kuwa je serikali itatoa wapi hizi pesa? Katika aya zinazofuata ninakokotoa mahesabu mengine kuonyesha vyanzo vya mapato vya kugharamia sera ya elimu bure.

  Katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA msingi mkubwa wa kukuza uwezo wa serikali wa kuhudumia wananchi umejengwa katika kubana matumizi ya serikali na kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kodi. Katika hili wameeleza waziwazi kwamba watapunguza ukubwa wa serikali kutoka mawaziri zaidi ya 40 wa sasa hadi wasiozidi 20, ikiwa ni pamoja na manaibu mawaziri.

  Hii ndiyo kusema kuwa CHADEMA watapunguza gharama za kuendesha serikali kwa zaidi ya nusu.

  Kuhusu kupanua wigo wa mapato ya kodi, Ilani ya CHADEMA imeweka mkazo katika mambo mawili. Mosi, katika kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija. Pili, mkazo umewekwa katika kuongeza vyanzo vya kodi ambavyo vimeanishwa vizuri katika bajeti mbadala mbalimbali zilizowasilishwa na kambi ya upinzani bungeni kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  Nitatumia mfano wa kupunguza misamaha ya kodi kuonyesha jinsi ambayo serikali inaweza kujiongezea mapato ya ziada na kujenga uwezo wake wa kutoa huduma kwa wananchi.

  Wataalamu wa kodi wameshauri kwa miaka mingi kuwa misamaha ya kodi isizidi asilimia moja (1%) ya pato la taifa au asilimia 10 ya makusanyo yote ya kodi. Wataalam hawa wanabainisha kuwa punguzo la kodi kwa kiwango hiki hakitaathiri mazingira ya uwekezaji hapa nchini. Hata hivyo, Serikali ya CCM imepuuza ushauri huu wa kitaalam.

  Matokeo yake serikali imeendelea kupoteza mapato mengi ya kodi. Kwa mfano, serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2008/2009 ilisamehe kodi kwa kiwango cha asilimia 2.7 (2.7%) ya pato la taifa ikiwa ni sawa na shilingi bilioni 731.3.

  Kama serikali ingefuata ushauri wa wataalam wa kodi ingesamehe kodi kwa kiwango kisichozidi shilingi bilioni 270. 8 na hivyo kuokoa takriban shilingi bilioni 500!! Ilani ya CHADEMA imetamka waziwazi kuwa Serikali ya CHADEMA itatekeleza ushauri wa wataalam na kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi haizidi kiwango cha asilimia moja ya pato la taifa.

  Hii ndiyo kusema kuwa kwa hatua ya kupunguza misamaha ya kodi pekee, Serikali ya CHADEMA itaweza kuokoa takribani shillingi bilioni 500, ambazo ni mara tano ya kiwango kinachotakiwa kuwasomesha watoto wa maskini bure.

  Tuangalie mfano wa pili. Katika ilani yake, CHADEMA wameahidi kubana matumizi ya serikali kwa kuachana na matumizi ya anasa. Moja ya eneo ambalo CHADEMA wamelenga kuokoa fedha ni eneo la posho. Mifano michache itasaidia kuonyesha kiwango cha pesa kinachoweza kuokolewa kupitia posho.

  Kwa mujibu wa vitabu vya bajeti, katika mwaka wa fedha wa 2008/09, Serikali ilitenga shilingi bilioni 506 kwa ajili ya posho, kiwango ambacho ni sawa na mishahara ya walimu 109,000, au zaidi ya theluthi mbili ya walimu wote nchini.

  Katika mwaka wa fedha wa 2009/10, kiwango kilichotengwa kwa ajili ya posho kilikuwa sawa na asilimia 59 ya mishahara yote ya wafanyakazi wa serikali. Sehemu kubwa ya posho hizi ni zile zinazolipwa kwa viongozi na maafisa katika taasisi za serikali na haziwahusu watendaji wanaofanya kazi katika mazingira magumu huko vijijini.

  Katika Ilani yake, CHADEMA imeahidi kupunguza kiwango cha posho ili kisizidi asilimia 15 ya mishahara wanaolipwa wafanyakazi wa serikali. Kwa hatua hii, Serikali ya CHADEMA itapunguza kiwango cha posho kutoka shilingi bilioni 506 za sasa hadi shilingi bilioni 126, na itakuwa imeokoa shilingi bilioni 380, ambazo zitaenda katika miradi ya maendeleo, ikiwemo kuboresha mashule na huduma zingine za jamii.

  Kwa hatua mbili tu za kupunguza misamaha ya kodi na kupunguza posho zisizo na tija kwa viongozi na maafisa wa serikali, serikali itaokoa shilingi bilioni 880!! Hii ni mifano miwili tu ya namna ambayo serikali makini inaweza kutumia vizuri pesa za walipa kodi kwa ajili ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma za jamii, ikiwemo kutoa elimu bure.

  Hatujakokotoa fedha zitakazookolewa kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri na kufuta nafasi za wakuu wa wilaya. Hatujakokotoa fedha zitakazopatikana kwa kutokomeza ufisadi serikalini, na wala hatajukokotoa fedha zitakazopatikana kwa kuimarisha mikataba ya madini. Kwa hiyo utaona kuwa, kwa kutumia mifano michache niliyoitoa hapo juu, tatizo letu sio ukosefu wa fedha katika kutoa elimu bure na huduma zingine za jamii. Tatizo letu kubwa ni utashi wa kisiasa na kukosekana umakini na uvivu wa kufikiri miongoni mwa watu tuliowakabidhi dhamana ya uongozi. Tukiwa na uongozi makini, adilifu na wenye upeo, utakaotumia raslimali zetu vizuri na kukusanya mapato ya kodi sawasawa na kuyatumia ipasavyo, tuna uwezo wa kutoa sio tu elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, bali pia huduma zingine za jamii.

  -------------------
  Mwandishi wa makala hii ni mhadhiri katika Idara ya Saikolojia ya Elimu na Taaluma za Mitaala, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anapatikana kwa simu namba 0754 301908
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  asante kitilam, ujumbe umefika,
   
 3. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nawashukuru nyote kuijadili hii hapa
   
 4. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kudos mkuu Kitila, analysis nzuri

  Na hiki ndicho nilichokuwa naomba kama ikiwezekana waelezwe watanzania kupitia redio binafsi na za umma na kupitia televisheni za binafsi na za umma katika kipindi maalumu hata cha dakika 20 ili kila mwenye masikio asikie ili wataalamu wa mipasho na wasio na huruma na taifa hili nao wasikie!

  Umma wa watanzania umeanza kuelewa hili hata kama watachakachua matokeo mwaka huu lakini naamini mwanzo wa mwisho wao uko karibu sana.

  Mungu akubariki na Mungu awabariki watanzania na taifa letu.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi Rais Kikwete ameanza kwa makusudi kuzungusha maneno; ameanza kusema ati watu wanadai watatoa huduma zote za jamii "bure"!
   
 6. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Utashi wa kisiasa ndio suluhisho la msingi, tatizo wapo pale kuangalia maslahi yao kwanza, kisha bakshishi ndio itufikie wavuja jasho. Hatuwezi fika kwa mtindo huu wa kiutawala.
   
 7. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  HONGERA SAMA MKUMBO KWA UFAFANUZI AMBAO WATU KAMA MALARIA SUGU, TANDALE ONE NA WALAMABA MAKOMBO YA UFISADI WENGINE WANAHUHITAJI SANA.

  KWA HAKIKA INATIA KINYAA KUMSIKIA MGOMBEA URAIS WA CCM AKITOA AHADI KUWA CCM ITATUMIA BILIONI 260 KUJENGA NYUMBA ZA WAALIMU NCHI NZIMA KATIKA KAIPINDI CHA MIAKA MITANO 201-2015; ILIHALI KWA MUJIBU WA MTIRIRIKO WA UBANAJI MISAMAHA YA KODI NA MATUMIZI YA SERIKALI KAMA INAVYOONYESHWA HAPO JUU SHULE ZOTE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZINAPASWA KUWA NA NYUMBA ZA WAALIMU ZA KUTOSHA NDANI YA KIPINDI CHA BAJETI YA 2011/12 (YAANI MWAKA MOJA TU).

  HII NI DALILI KUWA CCM IMEPOTEZA DIRA NA MWELEKO WA KUENDELEA KUONGOZA TANZANIA KUTOKANA NA KUSHINDWA KUTEKELEZA KIFUNGU CHA 9 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinatamka kuwa "

  …..Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha- (a) a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;
  (b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
  (c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumyonya mtu mwingine;
  (d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
  (e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;
  (f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;
  (g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali yamtu;
  (h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
  (i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha
  umaskini, ujinga na maradhi;
  (j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
  (k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
   
 8. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Shukrani Kitila
   
 9. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna njia nyingine ya kuelezea unyonyaji zaidi ya kuonesha jinsi CCM inavyowanyima Watanzania elimu. Ujinga wa watanzania waliowengi, ndio mtaji wa CCM. Laiti WAtanzania wengie wangeelewa hoja ya Kitila vizuri ili ifikapo Oct 31 hukumu iwe ya haki
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hii makala imewekwa kwenye magazeti?

  Nafikiri MKJJ ungeidesa kwenye Cheche kama bado lipo halafu likasamazwa kwa nguvu sana in these coming weeks ili kuwapa wananchi mwamko.
   
 11. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Friday, October 1, 2010 (via FaceBook)

  Watanzania tusidanganyike kuambiwa kupata huduma ya afya na elimu haiwezekani!

  Watu wengi wanaotafuta nafasi mbalimbali kutuongoza katika taifa letu la Tanzania wanatuambia kuwa huduma hizo zinaweza kutolewa bure.

  Watu wengine
  wanapinga sana hoja hizo. Mimi nasikitika kuona kuna watu wanapinga wakisema huduma hizo haziwezi kutolewa bure!

  Kadri yangu mimi nahisi inawezekana.

  Kwanza
  , wakati wa mwalimu Nyerere miaka hiyo vitu hivyo vilitolewa bure kabisa. Kama katika kipindi hicho mambo hayo yaliwezekana iweje leo isiwezekane. Watuambia kitu ambacho kinafanya huduma hizo ziweze kutolewa bure.

  Pili
  , wakati wa mwalimu Nyerere hapakuwa na miradi mingi kiasi cha miradi iliyopo sasa. Kadri ya wenyewe wanasema uchumi umekua. Kama uchumi umekua ina maana sasa tunao uwezo zaidi kuliko wakati huo. Kama tunao uwezo wa kiuchumi zaidi kuliko wakati huo, basi tunao uwezo zaidi wa kutoa huduma bure kuliko wakati ule.

  Tatu
  , ufisadi mkubwa uliotokea katika nchi yetu unaashiria kwamba mali nyingi sana za nchi yetu zimefanya watu wengi tuamini kuwa kama pangekuwa na uaminifu katika serikali na ulinzi mahsusi wa mali za umma, basi watanzania wengi wangeamini kuwa huduma nyingi zaidi zenyi ubora zaidi zingewafikia Watanzania wengi zaidi.

  Nne
  , misamaha ya kodi kwa wafanya biashara wakubwa inaonesha kuwa serikali haikusanyi mapato kwa makini zaidi ili kuhakikisha ina boresha huduma za jamii na pengine kuleta uwezekano wa kutoA HUDUMA HIZO BURE!

  Tano
  , uzembe katika uimarishaji wa miundo mbinu yetu kwa ajili ya kukuza biashara zetu na nchi jirani unafanya watu waone kutoa huduma hizi bure haziwezekni! Kama tungeimarisha biashara yetu ya nje pato letu la taifa lingeongezeka sana na hivyo kuifanya serikali yetu iwe na uwezo wa kutoa huduma za kijamii bure.

  Ukiangalia kwa makini
  sana utaona kuwa kutokuweza kufanya hivyo kunategemea sana watendaji wa serikali yetu waliopo madarakani. Kama wangejitoa kwa moyo wote kuwatumia wananchi mambo hayo yangewezekana.

  Ili kuhakikisha tunakuwa na uwezo wa kupata huduma hizo za msingi bure, hatuna budi tudhamirie kweli tarehe 31-10-2010 tukapige kura na kuchagua viongozi wenye uwezo na mwelekeo chanya wa kuwatumikia wananchi kwa kuachana na viongozi mafisadi, wasio na uwezo wa kuona mbali na wenye ubinafsi ili wote na vizazi vyetu baadaye tufaidi matunda ya nchi yetu.
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Natamani ujumbe huu ungemfikia kila mpiga kura nchini ili watambue ni kwa vipi CHADEMA in mikakati makini ya utekelezaji wa Ilani yake. Shukurani sana kwa analysis makini.
   
 13. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #13
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elimu bure inawezekana kabisa,wapingao wana yao na hawalitakii mema taifa letu!
   
 14. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Ipo kwenye magazeti si chini ya mawili. Nadhani ipo Mwanahalisi na Tanzania Daima. Niliisoma kwanza huko.
   
 15. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Elimu bure kwa mantiki hiyo inawezekana kabisa. Wazazi wanatakiwa waendelee kuchangia vifaa tu kama madaftari, kalamu, uniform, n.k. Maposho wanayolipana viongozi wa nchi hii ni makubwa kuliko hicho kiwango kilichotajwa hapo. Fedha nyingi sana kwenye bajeti zinaishia kwenye posho na gharama nyingi zisizokuwa na tija. Ukitaka kuifumua serikali hii ni kwamba Tanzania inaweza kubadilika kabisa katika kipindi cha miaka kumi tu.

  Hawa maofisa wa serikali ambao mishahara yao ya kwenye makaratasi ni midogo sana ndiyo hao hao wanaojenga majumba ya thamani kubwa katika miji yetu tena bila kuchukua mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha. Wanajenga kwa kuchota serikalini na njia ya kuchota ni haya maposho. Fedha nyingi za bajeti, zinaishia humo ndo maana unaona miradi yote inayogusa wananchi inatelekezwa kwa kusua sua mno au haitekelezwi kabisa.

  Sasa hivi wakati wa uchaguzi safari za ndani na nje ya nchi, makongamano, warsha na semina mbali mbali zimepunguzwa ili kuelekeza fedha kwenye uchaguzi na kuisaidia CCM kupata ushindi serikali imeweza kupitisha matingatinga katika bara bara nyingi sana na zinapitika. Yaani hii sadakalawe ya kugawana mapato ya serikali kwa mtindo wa posho mbali mbali ikipunguzwa hata kwa asilimia hamsini tu, serikali ina uwezo wa kulipia ukarabati wa bara bara zaidi ya asilimia 80% na kuzifanya zipitike kwa misimu yote.

  Kwa kweli jinsi serikali inavyoendeshwa leo, inatia kinyaa. Huwezi kuamini kama watanzania wanafikiria hata kidogo. Mabadiliko ni lazima, bila mabadiliko miaka mitano ijayo itakuwa ni balaa na kusaga meno!
   
 16. C

  Chamkoroma Senior Member

  #16
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BIG UP Dr. KITILA,

  Tanzania bila Nyerere imewezekana japo kwa kufumbia ukweli alioutaka baba wa Taifa lkn bila CCM inawezekana sn, napenda kusema kuwa KAMA CCYEM NA MAFISADI WASEMA ELIMU BURE HAIWEZEKANI, Je,mbona wao wametenga pesa kwa wafanya biashara kutokana na mdororo wa uchumi duniani hizo pesa wametoa wapi na za elimu na afya bure zisiwepo?

  Duniani kote Serikali inakuwa na uamuzi wakutengeza pesa kwa kuiamuru Benk kuu kuongeza pesa kwenye mzunguko wake, n apili huamua kutoa matumizi yasiyo ya lazima na kuyaweka katika huduma za jamii, na pia huangalia vyanzo vyake vya pesa na kuviboresha vitoe zaidi na pia huamua kuwabana watu wote wenyeuwezo wakuchangia pato la serikali kufanya hivyo kwa kuwaelimisha umuhiwake, na kuwapunhguzia kila tatizo linalowapata ili kufanikisha upatikanaji wa pesa bila kunung'unika, lkn leo wanasistizia kuwa hawawezi je, kwanini wasiondoke waachie wenzao wanaosema wnaweza kwa mfano wa Kenya na Mwalimu Nyerere?

  Kweli walioshiba hawaoni masikini wa TZ na kuwalazimisha wakubalikuwa haiwezekani wakati kila kitu kinwezekana chini ya jua nini lisilowekana? Hata kwenda Mbinguni unaanzia chuni ya jua, na kwenda jehanamu huanzia hapa, wana hoja gani?

  TUNAYAWEZA YOTE KTK YEYE ATUWEZESHAE, MUNGU MWENYE UWEZO WOTE.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  I do hope hii taarifa itawafikia watanzania vijijini wapate kuelewa
   
 18. pumbwes

  pumbwes Member

  #18
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Waweza kuipata Hapa
   
 19. fige

  fige JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najisikia vibaya sana pale watz wanaposhangilia kuwa elimu bure haiwezekani,najiuliza wanawaza nini? Ukizingatia wengi wa wale wanaoshangilia ndio wenye kuathirika zaidi na kutotolewa elimu bure. Ndugu wanajamii tufanyeje ili watz waelewe kutotolewa elimu bure.

  Ni kuendeleza pengo la Mabwana na Watwana? Najiuliza kama hawapendi chama au mgombea fulani hivi ni busara kushabikia kushindikana kwa jambo muhimu kama hilo?

  Nadhani watz wote wanatakiwa wainamishe vichwa chini pale watawala wanaposema haiwezekani.

  HAPA NDIPO NIONAPO HATA MAANA YA KILIMO KWANZA KABLA YA ELIMU INAPOKOSEKANA.

  Wanajamii hebu tuwaelimishe watz wenzetu wanachoshangilia.

  Nawasilisha
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Fige,

  Umaskini wa akili kitu mbaya sana. Wanaoshangilia wengi ni wale ambao kuanzia kibiriti hadi chumvi ni vya kugongea kwa jirani. Taratibu wanarubuniwa kuwa serikali haina wajibu wowote kwao.

  Walianza kukamuliwa kwa kuchangishwa michango ya lazima eti kujenga shule za kata ambazo ni za serikali hadi pale wizi wa richmond ulipostukiwa, jukumu la serikali ni nini? Sasa hivi wanalazimishwa kukesha kwenye patrol na mapolisi eti ulinzi shirikishi.

  Hivi serikali kama haiwezi kusimamia majukumu yake muhimu kama ya usalama wa raia wake, tuna haja gani ya kuwa na hiyo serikali?
   
Loading...