Kwa nini dawa ya jiko na siyo chumvi?

Ntandaba

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
922
1,472
Habarini Wapendwa.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwahoji wafanyabiashara (wajasiriamali wadogowadogo) juu ya wateja wao kuwasihi watumie jina la dawa ya jiko muda wa usiku na siyo chumvi.Pamoja na jitihada zangu za kuwahoji nimeshindwa kupata jibu kwa kuwa nao wanasema wanaigana tu kutumia jina hilo,
Naombeni mwenye ufahamu wa jambo hilo kwa sababu ukienda kununua usiku bidhaa hiyo na ukataja kwa jina la chumvi unaweza kukosa huduma
 
Nilivyowahi kusikia ni kwamba kutamka hivyo usiku ni mwiko ila siluambiwa ni kwa nini. Ngoja waje wakubwa tuambiwe. Na ni makabila katibuni yote
 
Mimi naona ni taboo ambayo haina athari yeyote.Wenyewe wanadai ukisema chumvi usiku basi ukiipikia haitokolea kwenye chakula hata uweke pakti nzima kitu ambacho hakina ukweli wowote.
 
Back
Top Bottom