dos santos
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 256
- 128
Akijibu swali kwa nini CUF imekubali kushirikiana na CCM kuunda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar,Mh. Hamad Rashid (mbunge) katika mdahalo uliofanyika katika hoteli ya movepick ulioandaliwa na vox media iliyo chini ya anserb ngurumo wa Gazeti la Tanzania Daima na kushirikiana na east Africa media,alianza kwa kuelezea chanzo cha kupatika serikali za namna hiyo
"
Serikali za umoja wa kitaifa zinatokana na mambo kadhaa,na kubwa ni utashi wa wananchi
" alisema na kutoa mfano "Waingereza conservative(chama cha siasa,uingereza) ambao ni rafiki wa chadema wameungana na liberals ambao sisi ni rafiki zetu vyama ambavyo uhusiano wao ulikuwa mbali sana. libers walikuwa karibu sana labour party kuliko onservative lakini mazingira ya wapiga kura yakawalazimisha ama conservative ama labour party waungane na lbers bahati nzuri makubaliano yakafikiwa libers na conservative wakaunda serikali ya pamoja hiyo ni sababu moja".Alisema na kuendelea, "Lakini ya pili ambayo imeibuka sasa hivi hasa afrika ni machafuko yanapotokea basi watu wanatafuta suluhu wanafika pahala wakasema maisha ya watu yamepotea hebu tuangalie mbele, watu wanaungana. Kwa mazingira ya Zanzibar ambayo chanzo chake na chimbuko lake ni migogoro ya kisiasa iliyotokea kabla ya hata kubenea hajazaliwa ilisababisha tufike pahala tuseme the way forward ni ipi? tutaendelea na mgogoro huu ili maisha ya watu yapotee? au tutafute njia muafaka ambayo tutafanya. Kwa hiyo tuliingia sisi katika makubaliano ya muafaka wa kwanza, wa pili na wa tatu." Akiendelea kufafanua alisema" kwahivyo kwamba katika kutafuta suluhu na katika kuwafanya watanzania na wazanzibar waishi pamoja basi ilikuwa ni lazima ipatikane njia ya kuwashirikisha kila upande ili tuingie serikalini hiyo ndio sababu kubwa wala hiyo haina unafiki kama vile libers na conservative hawajapoteza muelekeo wao, bado wameshirikiana katika mambo ya msingi wanaokubaliana. Kwa hiyo kwa utaratibu huo mnaunda tu programu ya pamoja ambayo kila chama itaikubali, hatimaye mnasema tunakwenda kutekeleza katiba hiyo kwa wananchi, ndicho kilichotokea hata Zanzibar hivi sasa. Kwahiyo si tatizo na hasa linapotokea kwa maamuzi ya wananchi wenyewe.Na hili ndo la msingi kubwa sana, kwamba wazanzibar wenyewe walipiga kura ya asilimia 64.8 hili ndio la kuzingatia kwamba sisi katika vyama mategemeo yetu ni maamuzi ya wananchi si maamuzi ya vyama vyenyewe,maamuzi ya wananchi ndo yanayotupelekea kufikia maamuzi na mifano kama hiyo niliyoitoa",alimalizia mh Hamad Rashid