Kwa nini CIA walikubali Kwame Nkrumah apinduliwe na kukataa Uhusika katika Harakati za Kumpindua J.K Nyerere?

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Kwame nkurumah ndiye rais wa kwanza wa Ghana alizaliwa mwaka 1909 na miaka 13 baadaye alizaliwa rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania Julius Nyerere. Kwame Nkrumah anafahamika kwa misimamo yake hasa ule wa kutaka afrika iwe nchi moja. Afrika iungane. Ni wazo ambalo pia alikuwa nalo nyerere ingawa yeye alikuwa na mawazo tofauti kidogo kuhusiana na aina ya muungano huo wa afrika.

Lakini katika yote mwaka 1966 kwame Nkrumah alipinduliwa akiwa katika ziara ya North Vietnam na China. Hakuweza kurudi nchini mwake na mpaka mauti yanamkuta hakuwa nchini mwake nchi aliyopigania kupata Uhuru. Wakati nyerere aliweza kujiuzulu nafasi yake ya Urais kwa Heshima mwaka 1985.

KWA NINI KWAME ALIPINDULIWA NA NYERERE HAIKUFANIKIWA KUPINDULIWA?

A. Ukiangalia ufanano na ukaribu waliokuwa nao Kwame Nkrumah na Julius K nyerere inashangaza inakuaje mwingine alipinduliwa na mwingine alijiuzulu kwa heshima na kubaki kuwa mmoja ya mifano ya kuigwa katika siasa za ndani nan je ya nchi? Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kuwa zilichochea jambo moja kutokea kwa mwingine na kutotokea kwa mwingine. Ingawa kuna majaribio kadhaa yalipangwa kumpindua nyerere na yote yakashindwa bado anabaki kuwa alisurvive katika nafasi hiyo na kuwa mmoja ya maraisi waanzilishi wa mataifa kuondoka kwa Amani katika uongozi. Tunayo mifano mingine ya akina Mugabe n.k


Katika kipindi cha Nkrumah na Nyerere Serikali zote mbili zilikuwa zinasumbuliwa na rushwa. Isipokuwa kulikuwa na tofauti kiwango cha rushwa na amna ambavyo serikali husika zilishughulikia suala hili la rushwa. Chama cha CCP ambacho kilikuwa kinaongozwa na Kwame ni muda mrefu kilikuwa kikihusishwa na rushwa toka miaka yake ya mwanzoni kabisa hata kabla ya uhuru. Ambapo Kwame ameshawahi kushutumiwa kwa kukopa pesa toka kwa waliokuwa wakiki support chama chake ili aweze kununua gari aina ya Cadillac.

Pamoja na hilo waghana walikuwa wakitozwa kodi kubwa sana wanapotaka kuingiza bidhaa toka nje ya nchi. Na kodi yao ilionekana kutumika kuwa neemesha baadhi tu ya watu na hili lilianza kujenga chuki kwa watu mbalimbali.huku rushwa ikitamalaki kwa kiasi kikubwa .soma " the beautyful ones are not yet born - Arma. kuna mengi ambayo yameelezewa humo kuhisiana na utawala wa Kwame Nkrumah.
Kinyume chake huku Nyerere alikuwa akijitahidi kuonesha Ubinadamu na kujishusha kuwa sawa na watu aliokuwa akiwaongoza kiukaribu nah ii ilimfanya hata akatae kuitwa majina ya kumtukuza kama Mh,Dr, Mtukufu na kuamua kuwa aitwe tu Mwalimu. Na abaadaye alipowatembelea wakomunisti wa china alijifunza Zaidi kuwa mnyenyekevu kwa wananchi na kupiga marufuku wanasiasa kuitwa Mh. Na hapo akapunguza pia matumizi ya serikali kuwa hakuna kununua gari la serikali kwa Zaidi ya pound 900.


Alitangaza kuwa viongoz wa Tanu hakuna kupokea mishahara miwili au kufanya biashara au kazi nyngine Zaidi ya siasa . hivyo watu kujiondoa katika mazingira ambayo yangeweza kuhamasisha rushwa na upigaji deal kama miaka hii tunavyoona.alionekana kukemea na kuchukia rushwa katika ngazi zote za serikali

B. ingawa wote walikuwa na namna ya kuwa shughulikia wapinzani wao lakini Kwame alionekana Zaidi kuwa alikuwa akifanya kisiasa kuwazima wenzie kwa kuwafunga na kuwafungia makazini kwao. Wakati nyerere alijaribu hili kulifanya kwa akili kwa kuwakabidhi kwa wanakijiji katika serikali zao hivyo kuwapa nguvu wananchi kujiona kuwa nao wanahusika katika kurekebisha wale wote wanaonekana kuwa ni kikwazo cha maendeleo yao. Na hii ilimfanya yeye kujivua gamba la ubwana mkubwa au ubabe na kuwapachika wenyeviti wa vijiji.

C. Mabadiliko ya kiuchumi kiviwanda kwa miji na mabadiliko ya kiuchumi kuanzia ngazi za vijiji. Kwame aliamiani katika kuendeleza na kukuza ile miji ambayo tayari ilikuwa na uzalishaji mkubwa au iliyoonesha ina rasilimali nyingi kwa spidi kubwa ukiangalia ujenzi wa Volta River project nk. Ulifanya Ghana igawanyike kuwe na miji inayokuwa kwa kasi sana kimaendeleo na mingine ambayo inazorota. Hili lilianza kujenga chuki. wakati huo Kwame akiwaza kujenga kinu cha Nyuklia kuipa nafasi Ghana ya kujuliakan dunia nzima .Wakati huo nyerere yeye alikuwa akiamini katika Ujamaa na kujitegemea akitaka kila sehemu iweze kujitegemea na kuendelea kwa wati mmoja akitaka watu waachane na kilimo cha jembe la mkono watumie plau. Wahame waache kutumia plau watumie matrekta na kuendelea yaani maendeleo ya hatua kwa hatua.

D. CIA inasemekana walihusika pia katika kusupport kuondolewa kwa Kwame hii ni kulingana na nakala kadhaa ambazo zilikuja kuwekwa wazi kuonesha kuwa CIA walijua tukio hili kabla ila hawakutaka kuingilia kutokana na kuwa ilionekana wazi tayari wananchi walikuwa wameisha mchoka Kwame na hivyo suala hili lingeleta mgogoro mkubwa kama angeendelea kubaki aliyekuwa Balozi wa USA inchini Ghana William Mahoney na Ajent wa CIA Paul Lee waliwah jadiliana suala hili kuangalia wao wafanye nini na mwishowe balozi aliona hamna haja ya kuzuia sababu tayari Kwame alishakuwa amepoteza sana umaarufu. Hivyo CIA wakaendelea kulinyamazia na pia kuwa support walioasi na hata Kwame alipoomba pesa toka USA walikataa kumpa ili kuweza kuendeleza serikali yake ambayo tayari ilonekana kuwa inashindwa hata kutumia zile pesa vizuri.

Kwa upande wa Nyerere aliweza kuwaweka mbali CIA na wengi walikuwa wanashangaa kwa nini CIA walikuwa na hofu kiasi kwa Nyerere. Ingawa wote walikuwa ni viongoz wa Mlengo wa kushoto yaani Kwame na Nyerere ambao walijitoa kabisa katika siasa za kimagharibi lakini nyerere alikuwa si wa kusogelewa sogelewa sana na CIA ukilinganisha na wengine.

Mtafiti G.Mwakikagile anasema kuwa CIA hawakutaka kujiingiza katika harakati za kumpindua nyerere sababu waliona bado alikuwa ana Mvuto mkubwa kwa waanchi ,hakuwa mla rushwa ,hakuwa mwenye tamaa na hivyo ilikuw angumu kumuingia sababu hata ilikuwa ngumu kujua angewaza au kuamua nini.

Na hata Oscar kambona alipoomba asaidiwe kumuaondoa Nyerere CIA walimwambia ilikuwa vigumu sababu hakuwa corrupt na hakuwa amejiwekea pesa kwenye mabenk ya nchi za nje n.k ingawa siasa za nyerere kwao zilikuwa hazieleweki ukilinganisha na mtazamo wa kambona ambaye walimkubali kirahisi kwa kuwa alikuwa na mtizamo wa kibepari. Lakini walikiri kuwa nyerere alikuwa na aina yake ya uongozi na wananchi walimkubali so kumwondoa kungesababisha machafuko makubwa sana.

tofauti hizi ziliweza kum favor J.Nyerere abaki madarakani pamoja na majaribio kadhaa na wakati huo huo mwenzake Kwame kuondolewa madarakani.
 
Nyerere alikuwa Mwanasiasa Mnafiki na Siasa hizo za Kinafiki ndio alirithisha Kizazi cha baadae Unafiki wa Kisiasa!

Alikuwa Mjamaa ambae Mabepari walimtuma kuunganisha Tnganyika na Znz ili Znz ya kina Prof Andulrahman Babu isiangukie mikono ya Makomunist
1964, January 19 Alipokoswa koswa kupinduliwa ni Waingereza Mabepari waliomuokoa!
 
Ha ha ha... Bujibuji hizi hard news vijana wengi hawapendi na pia sometime zinasababisha matatizo na wakubwa ndo maana kuepuka shida tunaamua kuuza chai kule kwingine.mfano hii mimi nlipost jana mapema sana ikawa chini ya uangalizi kwa muda mrefu sana. Thread za namna hii mods kwangu huwa sometme wanazipoteza au mpaka wazisome na kuzikagua sana
 
Asante GuDume kwa kuja kivingine, hongera sana kwa ujio mpya.
All in all Nyerere alikuwa ni mpakwa mafuta, ndio maana hadi sasa anaitwa mwenye heri Na huenda akafika kwenye daraja la utakatifu
I heard hiyo process huwa inachukua 20 years coz uchambuz unafanyika vatican direct. So mpaka aitwe mwenye heri ni process ndefu sana.
 
Ha ha ha... Threads za namna hii huwa nagombana sana na mods ndo maana nikaona niwe naenda tu kuuza chai kule kwingine. Hii ilikaa sana kabla ya kuruhusiwa hewani. Ilikuwa chini ya uangalizi wao kwa masaa kadhaa

guDume mwaga nondo habari za mapenzi waachie wafanyaki wa tanzania ya viwanda
 
Mkuu upo vizuri sana ...sema ukiwa kule unajitoa ufahamu tu... hii kitu nimeisoma na kuielewa nimejifunza kitu. ila kule pia usituache huwa unatufanya tusahau machungu ya dunia hii.
 
ha ha ha.............
Mkuu upo vizuri sana ...sema ukiwa kule unajitoa ufahamu tu... hii kitu nimeisoma na kuielewa nimejifunza kitu. ila kule pia usituache huwa unatufanya tusahau machungu ya dunia hii.
 
ha ha ha... Bonny ukirudi nyuma kwenye baadhi ya threads zangu utanikuta naandika but sometime kwa lugha flan ambayo wengine huwa inawapa shida kuielewa.

Kwel safar ya bagamoyo imekubadilisha umerud kivingne kabisa
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom