Kwa nini Chidumule kawachana waimbaji wa bongo flavor pamoja na wale wa dini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Chidumule kawachana waimbaji wa bongo flavor pamoja na wale wa dini?

Discussion in 'Entertainment' started by Johnsecond, Dec 17, 2010.

 1. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakati nikisikiliza taarifa ya habari ITV Chidumule akiwa msibani kwa Dr. Remi Ongala alipewa nafasi ya kuongea chochote. Alisema kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki mahili lakini alikuwa hatembei mabega juu ila anashangaa wanamuziki wa bongo flavor ambao kwanza wamepanga kwenye mabanda ya uani harafu wanatembea mabega juu na wale wa dini kasema wakitoa kasingle kamoja basi wanamsahau hata askofu.

  My take: Wanamuziki wa zamani hawawapendi vijana wa bongo flavor maana nilishamsikia ngurumo pia akiwachana kuwa wanaimbia juu, hivyo hawana maana.

  ebu nisikie views zenu nanyi pia wana jf.
   
 2. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 3,173
  Trophy Points: 280
  Kasema kweli kabisa.
   
 3. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  ''neno ya Muzee, ukabisha
  Mwisho utapata shida''....Quotes from Hayati Dakta.


  Sasa nirudi kwenye mada yako.
  Alichokisema Cosmas ni cha kweli kabisa kwani tumeshashuhudia wasanii kadhaa wa kizazi kipya waliokuwa ndani ya makundi then baada ya kung'aa ktk single moja basi anatoka ktk kundi then akishapewa kagari ''vilts'' na Muhindi anayemnyonya basi nyodo zinaanza.

  Au ukija kwenye medani ya muziki wa Dini mambo ni yaleyale, mtu akipata kaujiko basi hata tuzo zinazoitwa na kudhaminiwa na kilevi yeye atataka aende tu ili mradi keshajiona star.

  Tuliona kwaya kama Makongoro, kwaya ya mtakatifu Cecilia Mwenge, kwaya ya Nkinga, kwaya ya Ulyankulu barabara ya 13, kwaya ya Mabibo walioimba ''sauti ikatoka'' Maranatha, New life Band...tuliwaona watu kama kina Nyambele, Mzungu Four, Faustin Munishi na wengine weeengi ambao ulikuwa ukisikiliza nyimbo zao ni sawa na kusoma Bilble au kusikiliza mahubiri.


  Mfano hii kwaya ya mtakatifu cecilia Mwenge walitamba sana na albam yao inayomsifu Mama Maria mwanzoni mwa miaka ya 90 na mpaka leo ikipigwa utakubali kweli ujumbe unaupata.

  Tuje kwa ulyankulu:
  Hawa jamaa waliimba nyimbo kama
  Nuhu, Samson, na nyingine nyingi zenye ujumbe.
  Albam hii iliimbwa kwa ustadi wa hali ya juu sana. Kwani kila nyimbo iliyomo humu ni Mstari ktk Bible.
  Kwa mfano kuna nyimbo inayosema ''mtu mkubwa mmoja aliuliza akisema mwalimu, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa Milele?''...huu ni mstari ndani ya Bible na umezungumziwa ktk nyimbo. So ina maana hata kama hujui kinachozungumziwa ktk Bible basi utakielewa ktk nyimbo.


  Sasa rudi uje uwasikilize hao wanakwaya wenu wa siku hizi nyimbo zao utasikia ''nibebe'' mara huyo Frola Mbasha ana wimbo unaSema ''mwanamke simama imara'' kauimba kama mchiliku...lool

  Ni ushuzi mtupu.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wachungaji tunapata shida sana kutumia nyimbo za enjili za sasa kuhubiri neno!
   
 5. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sina tatizo na waimbaji wale wasiokuwa na dini maana wenyewe ni ile free style tu. Ila wale sasa wa dini wanaharibu sana na ndo maana hata wa miziki mingine wanawapaka. Angalieni muziki wa shaggy church heathen
   
 6. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wa-Bongo flavour si wanamuziki ni waimbaji. Ni wachache wanaweza kuwa na hadhi ya uanamuziki. Kijana akiwa na sauti ya kuimba basi ni kuandaa single tu, ndiyo maana karibu wanafunzi wote wa kiume wa sekondari wanaigiza uanamuziki. Mob psychology!!! Wao hawajijui, umri bwana!!!
   
 7. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #7
  Dec 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  flora mbasha ndio anachefua kabisaaaaaa! Hafai kabisa kumwimbia bwana.
   
 8. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi Bongo fleva nao ni wanamuziki?
  Mi huwa siwafagilii hata chembe..namfagiliaga prodyuza siku zote kwa ku copy, cut and paste mirindimo na mautamu ya nyimbo za watu na kuwawekea mabongo fleva!

  Mnakumbuka prodyuza alivyoiba wimbo wa watu akamuwekea TID... TID akajiona yuko juu hadi alipoteremshwa kwa aibu kwa kuwekewa wimbo original sambamba na ule wake feki?

  AIBU!
   
 9. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo unawapongeza jamaa kwa ku copy and paste? lakini wanazikamata saana pesa za watz. Ila ndo hivyo mimi pia nimekuwa nikifuatilia nyimbo nyingi za wa bongo wana copy kwenye olds za siku nyingi sana.
   
 10. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Hawa wana mziki wa Ubongo wa fleva,ni sawa kabisa alivyosema Cosmas-DUDU BAYA ni upi wimbo weake ambao mtu anaweza pata fundisho?
  Ni kweli awa wakitoa singo tu wanajiona madona au Michael Jackson
  Yupo wp Mr Nice?,Pig black,etc.
  Wanalewa masifa tena sana na kusahau wametoka wapi
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  chidumule wewe mwisho. unanikuna sana kwenye usitumie pesa km fimbo, barua toka kwa mama.
   
 12. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wabana pua wanaridhika haraka af wanajiona wamemaliza safari ya muziki..wakati wanaimba tungo nyepesi tena kama Big G zina heat leo,kesho kapuni...........Naunga mkono hoja.
   
 13. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  :noidea::A S-confused1::nono:
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Very True

  - Bongo Flavours siyo wanaMUZIKI ni waimbaji wa MUZIKI

  - Ni Kweli Bongo Flavours "akitoa single" utadhani amepata "Platinum" :: Haishi baa na vibinti na ujinga ujinga mwingi!
   
 15. M

  Mubii Senior Member

  #15
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu naona wanamuziki wa zamani hawakufaidika kimaslahi kama hawa wa bongo flavour wanavyofaidika nyakati hizi. Huenda hii imeleta msuguano kwa kuwa wale wa zamani walitunga nyimbo nzuri za kitanzania, walipiga kwa kutumia vyombo kama gitaa, saxaphone nk. Licha ya kufanya hivyo wengi wamekuwa na hali ya umasikini. Angalia vijana wa bongo flavour. Hajui kupiga hata aina moja ya muziki, hajui nota, lakini akiingia studio anatoka na nyimbo na michuzi zaidi kuliko wana muziki wa zamani. Katika hali ya ubinadamu, lazima utaona uchungu fulani kwamba wewe uli 'toil' sana hukupata mafanikio ya hali na mali ya kutosha na sasa wanakuja vijana wadogo wana 'toil' kidogo na anatoka na nyumba, ka-saloon n.k. Nashukuru Mwenyezi MUNGU yupo na anaona haya yote. Tumuachie kwani yeye anatawala vitu vyote ulimwenguni.
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wanamuziki wa zamani walifanyakazi zao kwenye mazingira magumu ukilinganisha na wanamuziki wa Bongo flavor.
  Enzi za Chidumule na wanamuziki wa zamani hawakuwa na fursa nyingi kama ilivyo kipindi hiki cha wanamuziki wa kizazi kpya.studio za kurekodi ilikuwa moja hapa Tanzania RTD kuliwa pia masharti ya nyimbo kurekodiwa mashairi yalifanyiwa uhariri kabla nyimbo haijaruhusiwa kurekodiwa.Wanamuziki wa Tanzania walilazimika kwenda nchi jirani ya Kenya kurekodi muziki kwenye santuri mahandalizi ya safari pamoja na gharama kubwa zilihitajika kabla ya Bendi ya muziki kwenda Kenya.Muziki wa zamani ulitumia vyombo [hala] za muziki hivyo ujuzi wa ulihitajika zaidi.Vipaji vya wanamuziki ilikuwa ni jambo lisilokwepeke hata kidogo.

  Muziki wa kizazi kipya ni vurugu kubwa hakuna wataalamu wa kupiga hala za muziki eg Solo guita,Rhyzim,Bass,Saxphone,Drum,Tumba na kinanda.Wapo waimbaji wa mashairi ambao ukiwapa hata kinanda hawawezi kutumia.hawana ujuzi wa muziki hata kidogo mara kadha nimehudhuria maonyesho ya muziki wa kizazi kipya nimegundua wameathiria sana na utamaduni wa wanamuziki wa Marekani na Ulaya.Utakuta mwanamuziki wa Kizazi kipya anashusha suruali chini ya makalio,katoboa masikio,kasuka nywele,kajichubua na upuuzi mwingine mwingi unaoufahamu.

  Wanamuziki wa Injili wa siku hizi tofauti na wa zamani hawana ujuzi wa muziki mbaya zaidi hawatumii neno la Mungu kwenye muziki wao maneno ya mitaani yamejaa kwenye muziki wanaouita muziki wa Injili.Muziki wa Injili unapaswa kwa namna yoyote ujikite kwenye maandiko matakatifu na si vinginevyo.Muziki wa Injili unapaswa kutumia tune ya kanisa na si Sebene au Rhumba na nk.Sebene na Rhumba hazina nafasi kwenye muziki wa Injili [Kanisa].Uchezajiwa wa wanamuziki wanaojiita wanamuziki wa Injili hauna tofauti na wanamuziki wa bendi za muziki wa dansi kabisa wakati mwingine nalazimika kubadiluisha chanel kukwepa kuangalia wanamuziki wa Injili wanvyodhalilisha kanisa na ukristo.Uvaaji wa wanamuziki wa Injili unatia kichefu chefu.

  Wapo wanamuziki wa Injili na kwanya mbali mbali zinazojitahidi kufuata njia sahihi ya uimbaji wa muziki wa Injili lakini hazipewi umuhimu wa kipekee kwenye TV station zetu pengine uelewa wa mdogo wa muziki wa Injili ndani ya vyombo vyetu vya habari umechagia kuporomosha muziki wa Injili.
   
 17. Kabota

  Kabota Member

  #17
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 15, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Ni kweli waimbaji wengi wa kizazi si wanamuziki kama wengi wanavyosema siku zote. Lakini hata hivyo katika biashara ya muziki hicho si kitu cha ajabu. Najua wengi wenu mnaosoma maoni haya ni wasomi na mnafahamu namna muziki kwa wenzetu unavyohusisha watu wengi mpaka wimbo ukausikia hewani.

  Kuna wanamuziki wengi wa nje ambao ni waimbaji tu(kutoa sauti basi) ambao hawahusiki katika kutunga, kuandaa melody, kupiga chombo chochote cha muziki na zoezi zima la utayarishaji. Kila kitu kinafanywa na mtu mwingine. Lakni niambie jinsi albam zao zinavyouza! Mwimbaji asipoweza kucheza chombo chochote cha muziki haimanishi kuwa hawezi kabisa kupewa heshima yake. Sababu kubwa inayowafanya wanamuziki wa zamani wawadharau wale wa bongo flava ni wivu tu. Walikuwa na nyimbo nzuri sana katu sikatai lakini hazikuwapa chochote.

  Leo hii vijana wanaodharauliwa kuwa si wanamuziki bali wababaishaji tu ndo ambao wamefanikiwa hata kuiweka kdg Tanzania kwenye ramani ya muziki duniani. Ni bendi gani ama mwanamuziki gani wa zamani ambaye amewashawahi kutajwa kuwania tuzo yoyote kubwa duniani? Kwa wengine yaweza kuwa ni sababu ndogo lakini hivyo ndo vigezo vya kutambua kama wanamuziki wetu wanatambuliwa nje ya mipaka. Wanamuziki wa zamani waache wivu kwani kulalama hadharani juu ya vijana wa sasa hv hakutasaidia chochote kama ujumbe wao wanautoa kwa dharau.

  Pengine hawafurahishwi na maisha wanayoishi vijana wa sasa yaani jinsi wanavyovaa, wanavyoongea, maudhui katika nyimbo zao lakni watambue kuwa hao ni vijana sio wazee. Namheshimu sana mwanamuziki anayeipa heshima kazi ama style ya mwenzie hata kama haipendi.

  Michael Jackson kabla ya kufa alikuwa ameshafanya kazi na wasanii wa sasa kama Akon, 50 Cent. Wil.iam kuonesha heshima katika mabadiliko ya muziki na pia kuwavutia mashabiki ambao muziki wa zamani hawaujui. Hayo ni maoni tu.
   
 18. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mkubwa hakika nimekupata maelezo mazuri sana,
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  anachokiona ndicho alichokisema na ni klweli usiopingika
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hawa wa bongo fleva wanajulikana tu, ila hawa wa muziki wa injili ndio huwa nawashangaa hawana tofauti na wa bongo flava
   
Loading...