Kwa nini Chadema wasidai Tanganyika yenye histria ya nchi wadai katiba bila nchi?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Mimi nahisi lamsingi zaidi kwa Chadema nikudai Tanganyika yenu ambayo Mwalimu Nyerere alitumia jasho lake lote na nguvu zote kudai uhuru wa Tanganyika (11 December 1961) kuliko kudai katiba mpya bila ya kuwa na Nchi yenu yenye historia ya nchi yenu na watu wake?.
Kusema kuwa Tanganyika ni Tanzania munakosea kwa watu wasomi kama nyiyi? au kusema Tanganyika iko ktk tumbo la Tanzania na historia ya Tanzania ndio Tanganyika vile vile mutashekwa na mutazaraulika ktk ulimwengu kwa vile historia huwezi kuifuta na itakuwa juhudi za kugombania uhuru wenu na jitihada zote zitakuwa (work done ziro).

Mimi nasema katiba haina makosa yenye makosa ni kurizika kuliwa nchi yenu na historia ya nchi yenu na kuanza kudandia dandia historia ya kunda unda ya Muungano,ktk Muungano wa Tanzania ukiuliza how is looser utambiwa ni Wtanganyika, kivipi nikuwa wamekubali kuua nchi yao na historia ya nchi yao.
Ndipo pale Wz'bar wanaposema Tanganyika nikifo cha kujitakia cha kusudi,walipo muona Mwalim mtu moja ana akili za Wtanganyika wote? kuita Bunge la Tanganyika na kusema Tanganyika ime kufaa kuanzia sasa hakuna tena Tanganyika kutakuwa na Tanzania na kila palipo andikwa Tanganyika andikeni Tanzania.
Sasa ujanja mwingi waswahili wanasema mbele kizaaa ndio huu, kwa upande wa Zanzibar wao hawakuua utaifa wao wala nchi yao, wana Rais wao,Bendera yao,Bunge lao,wimbo wa taifa wao,mawaziri wao Smz na mipaga ya nchi yao.
Ukija Bara utaona wamekuwa comfuse hawajuwi kipi kilichokuja mwanzo katiba au historia ya nchi yao,hivi sasa hujinasibu kuwa wao ni Wa-Tanzania na uhuru wa Tanganyika uita uhuru wa Tanzania na Wzanzibar wakiwaita Wtanganyika hukasirika na ugomvi lakini mshirika wao Zanzibar wao wanaona ufahari kujita Wzanzibar kwa vile wana nchi yao.
Waswahili husema mkataa kwao mtumwa ndio hivi? hakuna jambo la aibu kumkataa mzazi wako na kumpenda mzazi asokuwa wako(Tanzania) .
Nyiyi mumebaki kukumbatia Muungano tu na muko tayari kupoteza historia ya nchi yenu lakini tulinde Muungano ili tuwe na Wzanzibar? Wzanzibar hawana haja na Muungano na hivyo vijineno vyenu vya uongo kuwa Muungano ukivunjika watakao kula hasara ni wazanzibar hizo ni kasumba zenu munazotiana kabla ya Muungano Wazanzibar walikuwa matajiri kuliko sasa na Zanzibar ilikuwa free-port na nchi nyingi za africa wakija kushukuwa biashara Zanzibar lakini mulipotutawala tu mambo yote yaliyayuka.
Kwa hio kwa tarifa yenu sisi ndio tunataka Muungano ufee na kila mtu kuwa na mamlaka ya nchi yake na chake, na Kwa tarifa yenu wazanzibar hawako bara tu, ukenda nchi nyingi za africa kweli utawakuta na niwafanya biashara na matajiri na ukenda bara arab hivyo hivyo lakini nyiyi muko Zanzibar hamuna mulilo nalo ispokuwa kutumiliwa kutia shuki za kisiasa na kufitinicha na kungoja siku ya uchaguzi kuja kuua.
Katika uchaguzi uliopita kauli za viticho kuhusu umwagaji damu ilikuwa ni bara na sio Zanzibar zanzibar ilikuwa ni shuari na Wazanzibar walikuwa wamoja lakini kutokana na kuzowea kuua lilimiminwa Jeshi Zanzibar kuja kulinda koloni lao hivi sisi ndio tunawashukia nyiyi?.
Kwa hio Chadema mkomvi wao sio Hamadi Rashi(Cuf) mgomvi wa Chadema awe Nyerere alowauzia nchi yenu na historia yenu?.ni Hamadi Rashid (Cuf) Hamadi Rashid ana nchi yao na ikiwa kubadilika katiba kifungu cha 10 kimewakera basi kwa nini musiishitaki SMz au Wananchi wa Zanzibar kama ubavu upo?.
 

Attachments

  • Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere on Tanganyika Independent day.jpg
    Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere on Tanganyika Independent day.jpg
    18.9 KB · Views: 87
Sasa wewe hujawasikia chadema wakidai serikali 3? Hilo likifanikiwa si ndiyo tanganyika itakuwa imerejea?
 
Kwa nini tuwe na serikali tatu? Tunashindwa kuendesha hizi mbili ni lipi linatupa moyo kwamba serikali tatu zitafanya kazi? Tunatakiwa kukaa chini na kujadiliana either kuuwa moja ya hizi serikali mbili. Au kuboresha moja na kufanya nyingine kama kivuli (zanzibar). Kuwapa mawaziri wachache na wabunge wachache na baraza la wawakilishi likawa kama baraza la madiwani. Sera zote ziendeshwe na bunge tukufuku.

Inaniuma sana kuona Watanzania wengi tuna understatement umasikini wa Tanzania. Mnadhani tunaweza kuendesha serikali tatu? How? Where will the fund come from? Jamani kwa nini hatufikiri?

Tuuwe moja hiyo ndio dawa tuu, ambayo ni obvious kabisa ZNZ hawaitaji serikali yenye makamu waraisi na makawa mawaziri, this is insane. The poor country like Tanzania ina spend almost 25% ya budget yake kwa payroll and operating cost ya serikali yake. Sasa hapa tutaweka ngapi kwenye miradi ya maendeleo na kuboresha jamii?
 
ndugu yangu kweli mzanzibar ni aibu kuitwa mtanzania na kweli hapendi kuitwa mtanzania.

wala wazanzibar hawataki muungano, kila anayetaka muungano ni mkuja au ni yule muhafidhina.

1. mapinduzi hayakufanya na wazanzibar ila yalifanywa na watanganyika na tanganyika haikuwa na bandari sehemu zote za mwambao wa bahari wa tanzania hivi sasa ilikuwa ni zanzibar kuanzia tanga kwenda dar mpaka mtwara yote ni zanzibar.
watanganyika walikuwa hawana ruhusa kuingia sehem hizi ambazo ni zanzibar. na hata ukiona kiswahili cha watanganyika kutoka huko bara na wazanzibar kuanzia mwambao wa tanga dar mpka mtwara kilikuwa tofauti. waliingia sehem hizo watanganyika kufanya mapinduzi ambayo walishirikiana na miengereza mpaka zanzibar.
ndio ukaona tanga dar mtwara kukajazwa wakuja mpaka zanzibar.
sehem zote hizo za zanzibar zilifanywa mapinduzi na kuuliwa wakuja wengi sana, hakuna mzanzibar aliyefanya mapinduzi ila kuna wazanzibar waliofanyiwa mapinduzi na kuuliwa na mpaka hii leo mapinduzi daima.
tanu ndio iliyofanya mapinduzi kwa kushirikiana na baadhi ya wakuja wachache walioletwa na muengereza kwa makusudi.
baada makubaliono ya mapinduzi ya zanzibar walitakiwa watanganyika wabadilishe historia ya zanzibar na waengereza. waengereza ndio waliokuwa wakifanya biashara kuu ya utumwa kuuza waafrika na kuwaficha makanisani. na muengereza yeye alikuwa anayo haki kuuingia tanganyika kama koloni lake lakini muwarabu ilikuwa koloni lake ni mwambao wa bahari kuanzia tanga kwenda dar hadi mtwara.
muarabu alikuwa akienda kukamata wazee wake akina shibuda na kuwafisha makanisani kule zanzibar. makubaliano ya mauaji waliyoyafanya watanganyika ilikuwa ni kumfichia siri muengereza kama alikuwa akiuuza watumwa na kuwaficha mahandakini chini ya makanisa.
muengereza alishindwa kusambaza ukafiri zanzibar chini ya utawala wake ambao alikuwa akimlinda murabu pale.
waliletwa watu wengi kupitia tanganyika ili kujiandaa na mapinduzi kuanzia tanga dar mpaka mtwara. baada ya kupewa uhuru tanganyika muengereza aliifanya mbinu hiyo kushirikiana na tanganyika ili kuwaua wazanzibar yaani mauaji ya kimbari.

YouTube - ‫

YouTube - ‫
ha watu walitoka tanganyika kwenda kuuua wazanzibar

na utaona mpaka leo kukiwa na uchaguzi zanzibar tanganyika wanapeleka majeshi zanzibar yaani kabla ya uchaguzi basi kunakuwa lile jeshi lishaweka mapinduzi na kama zanzibar watakataa mapinduzi hayo watauliwa ni kukubali tu mapinduzi daima

2.wazanzibar hawataki muungano kabisa hata hizo serikali 3 hiyo ni sababu tu. ndio ukaona ccm ambao ni mahafidhina wanaotoka zanzibar ambao ni wachache wanasema tutalinda mapinduzi na tutalinda muungano.
wakiulizwa wazanzibar munataka muungano basi jibu hawataki wanaotaka ni wajuka na wale wakuuwa smz ambao ni mahafidhina.

muungano wa zanzibar kama kujadiliwa basi na kufanyike kura za maoni uone wazanzibar watasema nini?
wanaotaka muungano ni wachache ambao ni smz
suala la muungano waachiwe wazanzibar sio smz na sio serikali ya muungano.

suala la muungano ni la wazanzibar.

hii nchi sio ya watanganyika ni ya wazanzibar masuala ya muungano waachiwe wazanzibar wapige kura ya muungano wanataka muungano au laa?

kabla ya kura ya serikali ya mseto nilimsikia shibuda akileta uzushi eti zanzibar ni ya watanganyika nafikiria akasome sio kusoma historia ya nyerere basi namwambia shibuda rwanda na burundi ni tanganyika.
wazanzibar hawataki muungano wala hawataki kutambuliwa kuwa wao ni watanzania au watanganyika. hii yote ni kuzidiwa nguvu na mauaji.

visiwa vidoo lakini sasa idadi ya wakuja imekuwa kubwa mno kulizingatia ardhi yenyewe.

murudi mwakenu mutuachie nchi yetu na taifa leo na uhuru wetu. tanganyika hawana bahari wala bandari hili mufkirie uzuri.
na kila siku tukisema kweli munatuletea majeshi na wakuja
 
Huwa nashangaa! tunapo sherehekeya Uhuru wa Tanganyika, tunasherehekeya nchi isiyokuweko? Mapinduzi yanasherehekewa na Wazanzibari, basi kwanini uhuru usisherehekewa na watanganyika? Ni nani aliyekwenda mchomo, Watanganyika au Nyerere katupeleka pute?
 
inaezekana unayosema ndiyo mawazo ya baadhi ya wazenji hata wabara, ila nina mashaka na wewe kama ni zenji.Nadhani humu ndani tumeingiliwa.
 
inaezekana unayosema ndiyo mawazo ya baadhi ya wazenji hata wabara, ila nina mashaka na wewe kama ni Mzenji.Nadhani humu ndani tumeingiliwa.
 
Back
Top Bottom