Kwa nini chadema wanatumia nguvu sana kwenye hili swala la Madawa?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kuna nini kimejificha nyuma yake? Kwa maana sioni political gain yoyote kwa chadema kwa kutetea wanaohojiwa kwenye hili swala la Madawa ya kulevya! Je kuna nini kimejificha nyuma yake? Kuna mtu/watu wenu mnajaribu kuwalinda, labda?
Kwa maana haingii akilini nchi nzima imeathiriwa na madawa ya kulevya siajabu hata ndugu na jamaa zenu wamo pia lkn bado mnatetea tu wauza unga kulikoni? Au ndiyo kama wenye Richmond pia wauza Madawa mnao huko kwenu? Je ni michango ya chama au ni nini?
 
Kuna nini kimejificha nyuma yake? Kwa maana sioni political gain yoyote kwa chadema kwa kutetea wanaohojiwa kwenye hili swala la Madawa ya kulevya, Je kuna nini kimejificha nyuma yake? Kuna mtu/watu wenu mnajaribu kuwalinda labda?
Chadema wametetea nini? Kwani wengi wanaotuhumiwa ni wasanini ambao ni ccm walishiriki kwenye kampeni za ccm, Sidhani kama Chadema wanatetea chochote zaidi ya kuhoji mbinu inayotumika kuwabaini mtandao wa wauza unga wasambazaji na watumiaji wakubwa, hiyo style ya kuweza majina pasipo kuwa na ushahidi wa 100% nadhani ndipo kuna tatizo zaidi ni vyema makonda angejipanga Vizuri awe anafanya upelelezi makini ,mzuri wenye uhakika kabla ya kumtaja mtu mbele ya vyombo vya Habari.
 
Umekosa vtu vya kuandika, cdm wamtete wema au diamond!!!!
 
Teh teh....mtu haruhusiwi kusema neno tofauti na mnalofikiria ninyi!!!!?
Kazi ipo.......
 
Chadema wametetea nini? Kwani wengi wanaotuhumiwa ni wasanini ambao ni ccm walishiriki kwenye kampeni za ccm, Sidhani kama Chadema wanatetea chochote zaidi ya kuhoji mbinu inayotumika kuwabaini mtandao wa wauza unga wasambazaji na watumiaji wakubwa, hiyo style ya kuweza majina pasipo kuwa na ushahidi wa 100% nadhani ndipo kuna tatizo zaidi ni vyema makonda angejipanga Vizuri awe anafanya upelelezi makini ,mzuri wenye uhakika kabla ya kumtaja mtu mbele ya vyombo vya Habari.
Labda walishajipanga zamani Mkuu, kinyume na hapo heshima zao zitawashuka. Ila kama ni kweli, imekaa vyema sana, ila hawa ni vidagaa tu. Wawalete mapapa wa hizi business, hainiingii akilini hata chembe, mtu toka manzese movie au vingunguti flavor awe ndo main drug abuser nchini.

Tunawataka mawaziri, igp, cdf, well known business men kimataifa wa hapa (levo hizo) hii biashara ni kubwa sana. Haiwezekani wahusika wakuu waishi na maisha hata ya Azizi Abood mmiliki wa magari tu. Kilo moja bei gani vile? No and bg no, bg up Makonda tunajua umeanza, maliza tatzo..... Tunawataka mapapa. Hili ni janga kuliko njaa tuloikalia saaana kooni.

Nguvu kazi inapotea hovyo kisa haya madawa, nikitoka pata biroba vyangu ka nokia kangu shida kufika nako kisa mateja. Watu wamekatisha ndoto. Ray c alikuwa mizani sawa au kumpita Lady jay dee, kiuno pasi mfupa, no, hapana, ni matajiri na waajiri wetu, msiwafirisi, walazimisheni mitaji waloipata huko waitumie kuwekeza ktk kilimo cha umwagiliaji kwa mazao ya kilimo.

Utajiri lazima uambatane na mambo kama haya. UK na kwingineko walipitia biashara haramu zaidi ya hizi pia.
 
Mkuu ni kweli umekurupuka kuweka uzi huu hauna mashiko hata kidogo, Nyavu haramu zipo nchini na kiwanda kinachozitengeneza unajua kilipo pia mawakala wakuu wa hizo nyavu unawajua kwa nini uangaike na wavuvi kule baharini! Suluhisho funga kiwanda au badili matumizi ya kiwanda.
 
Back
Top Bottom