Kwa nini chadema? Au ni ulelege wa ccm?au ni mapambano ya mahitaji ya nyakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini chadema? Au ni ulelege wa ccm?au ni mapambano ya mahitaji ya nyakati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Jun 17, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima kwanza!

  Leo nimechagua lugha ya mafumbo kuwakilisha misuguano ya kifikra juu ya kupanda kasi kwa CHADEMA na kuyumba kwa CCM. Natambua wapo wanabodi ambao hawapendi kusoma makala ndefu kutokana na sababu za hapa na pale, lakini naamini wataweka udhaifu huu pembeni na kusoma angalau kuambulia maneno mawili, matatu n.k. Endelea kusoma...

  Kwa wale wasioijua safari ya mchele kule ulikotokea, usemi huu " Mpunga mbaya, huonekana wakati wa kuukoboa "kwao unaweza kuwa mto mrefu usiovukika. Ni wale tu wanaoijua safari hii, inayoanzia kwenye giza la vumbi hadi kwenye weupe wa theluji ya mlima Kilimanjaro, ndio wanaoelewa kuwa, kabla ya mchele kuwako, ulitangulia mpunga.

  Kwa faida ya wale wasioijua safari ya mchele, niwafahamishe kuwa, mchele ambao ukipikwa unaweza kutupatia wali, pilau au biriani, ni tunda la mapambano makali kati ya mpunga na mashine za kukoboa.

  Kile kinachotokea ni kuwa, baada ya mpunga kuvunwa, huanikwa juani kwa muda mrefu kabla ya kuingizwa katika vinu vya ukoboaji. Ni wazi kama mpunga ungelikuwa nafsi hai, kitendo hiki cha kuuanika, kingeliuletea mateso na maumivu makubwa. Baada ya kukauka, mambo huendelea kuwa magumu, pale unapoingizwa kwenye meno ya mashine ili kuvuliwa maganda yake.

  Hapa tena, kungekuwa na kilio na kusaga meno, kama mpunga ungelikuwa na mwili wenye ufahamu ndani yake. Ni baada ya kupambana na miali ya jua na meno ya mashine za kukoboa, hapo ndipo chembechembe ndogo nyeupe zinapoanguka katika chombo, tayari kwa mapambano mapya yatakayougeuza kuwa wali, pilau au biriani.

  Kwa wale wasioujua mpunga, watangojea hadi wakati wa kuupika ndipo, waweze kuutambua kama ni mbaya au mzuri. Kwa wazoefu wa mpunga, mambo ni tofauti, kwao uzuri au ubaya wa mpunga, huonekana wakati wa kuukoboa. Kama mpunga umebeba mchele mzuri, katika kuukoboa utatoka ukiwa mzima kinyume cha hapo, utashindwa kustahimili mikiki mikiki ya kinu cha kukobolea.

  Baada ya kuielezea safari hii ya mpunga, hebu sasa tumrudie Mwenye hekima ili atueleze sababu zilizomfanya atuletee usemi huu.


  Kile Mwenye hekima anachotaka jamii ielewe katika hili, ni ule ukweli usiopingika kuwa tabia ya mtu mara zote, huonekana wakati wa misukosuko. Kama vile ubaya wa mpunga unavyoweza kuonekana wakati wa kukobolewa, nyakati ngumu zinapofika, ndipo wema au ubaya wa mtu unapoonekana. Kutokana na ukweli huu, baada ya Mwenye hekima kuona vile urafiki unavyoyumba wakati wa dhoruba, kope zake nyeupe zilisisimka na kukubaliana na moyo wake.


  Kwanini CHADEMA inshika kasi kisiasa namna hii na sio CHAUSTA, NLD, UDP, TLP, CCK n.k? Isiwe nongwa CHADEMA wanastahili sifa, vyama vingi si mwanzo tu wa mapambazuko ya kisiasa nchini bali vyama makini ndio chachu ya mabadiliko nchini, CCM dhaifu iwe changamoto ya kupata CHADEMA imara and viceversa is true.Mpaka hapa demokrasia itakuwa imechanua vizuri Tanzania.

  Mimi ni Mtanzania,
  Mungu ibariki nchi yangu
   
Loading...