Kwa nini CCM itaendelea kushinda kwa zaidi ya miaka 50 ijayo?

CCM inavuma katika anga za kimataifa kwa kuleta ukombozi barani Afrika,na Afrika nzima sasa kuwa huru.Jivunie CCM.CHAGUA CCM,CHAGUA KIKWETE.
Hiyo sisi m inayoleta ukombozi kwingine na kuua uhuru nyumbani kwa kukandamiza demokrasia na uchumi mimi na familia yangu na ndugu zangu hatuitaki
 
Pia hata Daniel Arap Moi alisema KANU itatawala miaka 100 mbele, hazikupita chaguzi mbili chali.
 
ajira milion moja kiwete juuuuuuuuuuuuuuu

dsc00019%2b%5b800x600%5d.jpg

duh! Swahiba sikutegemea kama na wewe ni miongoni mwa wanaolalamikia hili, sasa ndugu .........nchi ganii isokuwa na

wafanyabiashara ndogo ndogo?, au unajua level ya shule ya huyu dada na wafanyabiashara ndogo ndogo? Wataka apewe

ajira wizara ya fedha?, au tanroads? Au bot? Au ikulu?, hebu niambie wataka iweje?.

Unasikitisha ndugu.
 
ccm inavuma katika anga za kimataifa kwa kuleta ukombozi barani afrika,na afrika nzima sasa kuwa huru.jivunie ccm.chagua ccm,chagua kikwete.

ni uweli unaothibitika kuwa ccm wanajulikana anga za kimataifa kwa kazi nzuri waliyoifanya kuleta ukomozi katika nchi za africa(kusini mwa africa) lawama zote zinazotupwa na wana chadema forum ni kwa kuangalia watu wachache wanaoharibu mambo ndo wanachukulia kuwa wana ccm wote wametenda hivo kitu ambacho me nadhani sio kizuri kukichambua chama kwa kuangalia watu wachache ambao kwa mtazamo wao wanasema kuna watu wabaya ndani ya ccm kitu ambacho si kweli.
 
When I read Mikole and the likes of him, current supporters of ccm, I kneel and pray to the Almighty that He save us from Wishfull thinkers. Amen
 
ni uweli unaothibitika kuwa ccm wanajulikana anga za kimataifa kwa kazi nzuri waliyoifanya kuleta ukomozi katika nchi za africa(kusini mwa africa) lawama zote zinazotupwa na wana chadema forum ni kwa kuangalia watu wachache wanaoharibu mambo ndo wanachukulia kuwa wana ccm wote wametenda hivo kitu ambacho me nadhani sio kizuri kukichambua chama kwa kuangalia watu wachache ambao kwa mtazamo wao wanasema kuna watu wabaya ndani ya ccm kitu ambacho si kweli.
KAMA NI WATU WACHACHE NI JK (mwenyekiti), SI WACHACHE TENA. Watoeni hao wachache kwanini muwakumbatie!!! mbona Nyerere hakuwakumbatia viongozi wachafu!!
 
Hatupo kwenye ajira.cc ni wazalendo wa nchi yetu tunaojua CCM imetutoa wapi na sasa tuko wapi na tunaelekea wapi.
Hatuwezi kumpa nchi mtu tapeli,mnyang'anyi na mpotoshaji wa jamii.Hura zetu tutampa KIKWETE kwa kuwa amefanya mazuri tumeyaona na kuna mengi mazuri yaja.
 
ni uweli unaothibitika kuwa ccm wanajulikana anga za kimataifa kwa kazi nzuri waliyoifanya kuleta ukomozi katika nchi za africa(kusini mwa africa) lawama zote zinazotupwa na wana chadema forum ni kwa kuangalia watu wachache wanaoharibu mambo ndo wanachukulia kuwa wana ccm wote wametenda hivo kitu ambacho me nadhani sio kizuri kukichambua chama kwa kuangalia watu wachache ambao kwa mtazamo wao wanasema kuna watu wabaya ndani ya ccm kitu ambacho si kweli.
Hapo ndio watz wengi tunapopotoka. Hivi tukisema Tanzania rushwa imekithiri inamaana watanzania wote wananuka rushwa? Ama tukisema Tanzania ni masikini wa kutupwa ina maana watz wote ni masikini wa kutupwa? Fikirieni kwa mapana zaidi. Hatuichukii CCM kwa jina lake wala wanachama wake, kwani wote ni watz kama watz wengine. Tunachopigia kelele ni uongozi mbovu wa chama hicho, ulioshindwa kutekeleza na kusimamia yale inayoyapigia debe.
Rushwa: Ahadi ya mwanaccm "Rushwa ni adui wa haki, sintapokea wala kutoa rushwa". Je, unaamini katika utimizwaji wa ahadi hiyo na viongozi wa CCM? Mifano hai unayo na Mwenyekiti wa chama alilipigia kelele suala hilo katika chaguzi za jumuia za chama. Ni mwaka jana tu. Je, kulikuwa na uthubutu wa mwenyekiti kupambana na rushwa ndani ya chama chake?
Ubinadamu: Ahadi ya mwanaccm "Binadamu wote ni ndugu zangu na afrika ni moja". Je, viongozi wetu wanaishi kutokana na ahadi hii? JK kwa maslahi binafsi alimuengua Bashe, kibaguzi kabisa. tena akiwa kiongozi mkuu wa serikali bila ya kufuata taratibu walizoziweka wenyewe alimtangaza Bashe kuwa sio raia. Ubaguzi upo wa aina nyingi, ukiwepo wa kuwatenga wakosaji wa kosa lilelile katika utoaji wa adhabu (Ushahidi unao, refer EPA). Kama kiongozi wa nchi anafanya hivyo, bado anafaa kuitwa kiongozi wa watu wote?
Ujamaa na kujitegemea: Ahadi ya mwanaccm "ujamaa na kujitegemea ndio njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru". Kitu pekee ambacho JK na nyie wafuasi wake hamkukielewa ni maana ya ujamaa. Nadhani bado mna fikra kwamba ujamaa ni umilikaji wa njia za kiuchumi kijamaa na watu binafsi kutomiliki mali na pia mnadhani kwamba ujamaa ni umasikini. Nawapa darasa dogo na mumweleze JK, ujamaa aliomaanisha Baba wa taifa ni ujamaa wa kiafrika, sio ukomunisti wala ujamaa wa kichina. Katika ujamaa wa kiafrika, alimaanisha ushirikiano wa kindugu katika maisha ya kila siku ambapo kila mtu alitakiwa kula kwa jasho lake, pasiwe na mtu wa kumnyonya mwingine. Mali ya mtu itokane na pato halali. Waliotekeleza falsafa ya Mwl, walielewa ujamaa kama anavyouelewa JK, wakadhani ujamaa ni kunyanganya mali halali za watu.
Kazi: Kazi ndio msingi wa maendeleo, ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi. Ndugu zangu kama kuna mahali serikali inayoongozwa na ccm ilifeli ni kwenye kusimamia wajibu wa kila mtu kufanya kazi. Mmekuwa mashuhuda wa kuibuka kwa makundi mengi ya vijana wa vijiweni maarufu kama "camps". Camps hizo zimekuwa maficho ya vibaka na wavuta bangi, na vingi vimekuwa pia vikiitwa vijiwe vya wakereketwa. Kisingizio kikubwa ni kukosa ajira. Hivi kweli katika nchi hii, hakuna watu wenye ubunifu kabisa wa namna ya kuondoa tatizo hili? Wenzetu wa Tandika, Tandale na maeneo mengine ni wahanga wa vijana hawa.
Ewe mwananchi, hatima ya nchi yako iko mikononi mwako, tumewapa fursa viongozi wa CCM kwa muda mrefu mno lakini wameshindwa kutupeleka tunakotarajia kwenda. Hii ni kwa ajili yako, mume wako, mke wako, watoto wako, ndugu zako na jamii yako yote. Fanya mabadiliko sasa, sema hapana kwa CCM. Kwa kufanya hivyo utasaidia sana kuamsha serikali usingizini, serikali itatambua kwamba inao wajibu kwako.
 
CCM inavuma katika anga za kimataifa kwa kuleta ukombozi barani Afrika,na Afrika nzima sasa kuwa huru.Jivunie CCM.CHAGUA CCM,CHAGUA KIKWETE.
mikole
Banned

Join Date
Mon Oct 2010
Posts 5
Thanks 0
Thanked 1 Time in 1Post
Rep Power 0

Mkuu inategemea uelewa wako ukoje. Ukitaka kujua ukweli jinsi TAnzania inavyosemwa kwenye anga ya kimataifa unaweza kukataa kuwa mtanzania. Ukisikia jinsi Tanzania inavyosemwa Afrika unaweza kulia. Kwa wewe inaweza kuwa ni sifa na inawezekana ni kwa kuwa huji kinachosemwa, unaweza kushangaa kampeni manager wa CCM ana kashfa na watu wa nje wanafahamu vizuri, wabunge wengi EPAs mpaka sasa wanapeta tena wanasifiwa na rais kuwa watu safi.

Kama swalim lako ni kwanini CCM itanedelea kutamba kwa miaka 50 ijayo, basi ni kutokana na yale aliyosema Profesa Baregu. Poloitical capital ya CCM ni ujinga wa majority ya electorate, kama wewe unapenda iendelee kwa miaka 50 inachekesha sana.
 
Back
Top Bottom