Kwa nini CCM ina HOFU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini CCM ina HOFU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Sep 6, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tofauti na chaguzi zilizopita ukiachilia ule wa kwanza 1995 CCM imeonyesha kuwa na wasiwasi wa hali ya juu kufanya hata waliokuwa hawafuatilii mambo ya uchaguzi kuanza kujiuliza kulikoni.

  Maswali haya wanayojiuliza wananchi ni kutokana na CCM kuacha misingi iliyowapatia heshima na kuanza kufanya yale yaliyokuwa yanatazamiwa yafanywe na wapinzani.

  Ukweli usiopingika ingawa CCM inadai wapinzani wanatumia lugha zisizo za ustaarabu lakini CCM itakuwa ya kwanza kulaumiwa kwa kukumbatia vitendo hivyo ikiongozwa na Katibu wake mkuu.

  Kitendo kingine kinachoonyesha CCM kuwa na hofu ni kuanza kutumia vyombo vya habari vikiwemo vya umma kukifanyia kampeni za waziwazi, heri zingekuwa za ustaarabu lakini ni kampeni za kuchafuana.

  Inasemekana kuna baadhi ya magazeti yameelekezwa na baadhi ya viongozi wa CCM yagawiwe bure kwa lengo la kuwachafua baadhi ya wapinzani wanaoonekana kuisumbua, hii yote ni kielelezo tosha cha hofu waliyonayo.

  Hofu nyingine inatokana labda na udhaifu alionao mgombea wake Jakaya Kikwete ikiwemo afya yake dhidi ya mgombea machachari wa Chadema Dr. Slaa, inawezekana CCM hawakutarajia kuwa Dr. Slaa atachukua fomu ya kugombea urais mwaka huu, ni hofu.

  Inawezekana pia hofu nyingine inasababishwa na CCM kutokuwa na majibu ya watuhumiwa wa ufisadi List of Shame. Huenda baada ya CCM kukosa majibu yake ndiyo maana imeamua kujiingiza kwenye vitendo vya kushambulia mtu badala ya kujibu tuhuma, ni hofu.

  Mwaka huu Chadema imeweka wagombea karibu asilimia 80 ya majimbo yote na CUF karibu asilimia 60 ya majimbo yote na kufanya upinzani kuvunja rekodi ya kuwafikia watanzania wengi. Hii nayo inaweza kuongeza hofu ndani ya CCM.

  Hofu nyingine inatokana na kukua kwa uelewa wa wananchi kwa dhana nzima ya upinzani kuwa si uadui tofauti na chaguzi zilizopita na hasa ujio wa kizazi kipya ambacho hakikushiriki uchaguzi wa 1995, ni hofu.

  Hofu hizi zinadhihirishwa na mikutano ya ndani ya CCM inayofanyika usiku na mchana kwenye maeneo tofauti nchini hasa Dar es salaam kwa kubadilisha venue (Hotel) mara kwa mara, ni HOFU.

  JE ni nini unafikiri CCM inahofia juu ya hatima ya uchaguzi huu au kwanini unafikiri isiwe na hofu.

  Naomba kuwasilisha,

  Luteni.
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfalme wa dhambi anaogopa kuondoka madarakani maana atavuliwea nguo; lazima ajifiche na ajiimarishe ili asivuliwe nguo; CCM hawawezi kumuachia Dr Slaa nchi wanajua atakalofanya litawavua nguo maana walishajivua kwa matendo ila wanajua kuyaficha ndio njia sahihi; hofu inatokana na hilo la kuvuliwa nguo
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama hofu ni kuvuliwa nguo ina maana watatawala milele!
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Umesahau kwamba kafu ni sisi m 'b'?
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Luteni umesahau kusema ni kwa nini vyombo vya umma vya usalama pia vinahaha?
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Asante MF kwa kunikumbusha ndio maana pale mwisho nikaachia wanaJF nao waziseme hofu, UWT wamejaa humu kweli hii nayo inadhihirisha hofu.
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu, Hayo magazeti yalifanya hivyo hivyo 95, 2000, 2005? unashangaa nini leo 2010?

  Nimekuuliza wameandika kashfa ipi? kuna tofauti kati ya kashfa na ukweli...mathalan, kusema Slaa ni mtaalamu wa kanuni za kanisa siyo kashfa ni ukweli! au siyo. Kusema Slaa amemuacha mke wake na yuko na mke wa mtu ni ukweli si kashfa au siyo..nk..kwakuwa wewe ni mpenzi wa Chadema unaumia sisi tunafurahi kwasababu jamaa si muadilifu na hafai kuwa rais

  Wananchi wanahitaji kumfahamu mgombea wa urais ndio maana magazeti ya serikali yameandika huo ukweli!
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Utingo, kuna wanaJF wanasema kwa vile CUF ni sisiem bii hata akiipigia kampeni sisiem ni sawa na kuipigia CUF.
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ccm hofu wanayo sana tena sana kwani kwa asilimia kubwa wadanganyika wameaanza kutoka usingizini wanajua pumba na mchele so wapo kwenye wakati mgumu
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hizo Pesa CCM walizonazo kwa Uchaguzi kama wangeziweka kwenye Maendeleo ya Nchi nadhani wangetawala ka Karne Nzima
  Mfano Masha ana Pesa lakini hajafanyia kitu chochote Nyamagana; angalia anapendekeza Uwanja wa Nyamagana Mwanza the only Stadium usio na makucha ya CCM mkoani kuuzwa kwa watu sio wazalendo; yaani wamesahau historia ya Uwanja Wa Mpira Wa Nyamagana - anyway Lau Hajui historia ya Mwanza... Hakukulia Mji wetu wa Miamba

  Nina Uchungu hata kama niko nje ya Nchi...
   
 11. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimesema kuna tofauti ya magazeti kuwa bias na kuandika kashifa, mfano gazeti kuandika mikutano ya chama kimoja hiyo si kashifa ni kuwa bias lakini gazeti tena la serikali kuandika maisha ya ndani ya mgombea wa upande mmoja hiyo ndiyo kashifa.

  Asante kwa kuwa muwazi kuwa unafurahia hizi kashifa kwa vile tu wewe si Chadema.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si humu tu wanatukela hata huku mitaani as if wao ndio watamchagua rais wa nchi hii peke yao au as if nchi hii ni personal property yao!
   
 13. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  hofu inatokana kupata utambuzi kuwa tanzania bila ccm inawezekana; ccm bila tanzania haiwezekani; na ufisadi wao bila ccm hauwezekani.
   
 14. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Vile vile wananchi wanahitaji kufahamu kwamba kina Mkapa, JK, Lowassa na Rostam walikwapua hela za EPA na Marando anasema ana ushahidi. Sasa CCM kupitia kwa Kinana wanalalama nini kuhusu Chadema? Ukweli ni ukweli. Mkuki kwa nguruwe.
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Kwanini wasiwe na hofu wakati hawana uhakiwa wa mgombea wao kufikisha roundi 12, afya bwana ndiyo hofu kuu.
   
 16. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtumwa wa mafisadi; na vyombo vyao; ukweli hupimwa mahakamani au kwa kuuliza wahusika wote; mbona vyombo havikumuuliza mhusika wa upande wa pili maan ayuko Singida na Mmewe; umesoma sawa na maprofesa kibao wajinga kabisa maanake elimu haijawakomboa; lazima ujue lengo la chombo cha habari; sio unaongea upupu hapa; taarifa bila balance ni udaku; ndio maana anatamba tanzania kwa kusema ana vyombo vya udaku wispering News media yaani habari zilizochakachuliwa; hata wenye akili waziishi hizo au sio utupu na machukizo machoni mwao; wewe unaweza kuwa uko upande wa pili
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  JK ndiyo msafi?
   
 18. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Ina mgombea dhaifu kikwete ambay serikali yake ilitegemea kwa kiasi kikubwa dr.slaa atasema nini...kwa maana nyingine kwa wale waelewa wanajua jinsi slaa alivyomsaidia kikwete kuongoza nchi indirectly kutokana na ujasili wake uliotukuka......hii ndiyo hofu kubwa kuwa wananchi wanajua mchango mkubwa wa slaa kwa hiyo kuna kila dalili kuwa kikwete kura haziwezi kamwe kumtosha labda waendee kuchakachua kama walivyofanya mbeya..........
   
 20. MAWANI

  MAWANI Member

  #20
  Sep 6, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi mimi baba; jakaya uadilifu wake uko wapi? Mademu kila kona tanzania na nchi za nje?
   
Loading...