Kwa nini bei ya cement iko juu sana hapa Tanzania ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini bei ya cement iko juu sana hapa Tanzania ??

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mu-Israeli, Jul 18, 2012.

 1. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hi wana JF wote.
  Najiuliza sana kwa nini bei ya cement iko juu sana hapa Tanzania.
  Najiuliza hivyo kwa sababu naona kuna cement toka nje ya nchi inakuja na kuuzwa kwa bei nafuu kuliko cement inayozalishwa hapa Tanzania.
  Hiyo cement inayotoka nje imezalishwa kama cement yetu hapa, imesafirishwa, imelipiwa kodi, imelipiwa bima ya usafirishaji, n.k. halafu bado ni nafuu kuliko cement yetu !!!???
  Nimeangalia bei za cement za nchini Pakistan ambako ndio inatoka cement nyingi inayoletwa hapa Tanzania.
  Bei ya tani moja ya cement ni dola za kimarekani (USD) 62.00 kwa tani (ukinunua huko). Pia bei pamoja na usafirishaji mpaka bandari ya Dar es Salaam au Mombasa ni USD 90.21 kwa tani.
  Bei hizo ukizibadilisha kuwa shilingi ni kama ifuatavyo:-
  USD 62.00 = Tzs 99,200 kwa tani, ambayo ni Tzs. 4,960 kwa mfuko wa kilo 50.(Ukinunua kule Pakistan bila kusafirisha)
  USD 90.21 = Tzs 144,336 kwa tani, ambayo ni Tzs. 7,218 kwa mfuko wa kilo 50 (bei pamoja na usafiri toka Pakistan mpaka Dar es Salaam).
  Swali:-
  Kinachofanya bei za cement zinazozalishwa Tanzania kuwa juu sana (Tzs. 12,000 au zaidi kwa mfuko wa kilo 50) ni nini ??

  Visit: http://www.alibaba.com/product-free/107472674/Cement_52_5_in_20_ft.html
   
 2. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ...Mkuu kuna mikono michafu y watu....
  Malawi na Zambia, bei ya diezel ni Tshs 750/= ni mafuta yaleyale yanayokatisha hapa Ubungo.
  je, si zaidi sana Cement toka Afghanstan?
   
 3. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kwakweli inaudhi sana
  ngoja waje wanaofahamu labda kuna sababu
   
 4. mito

  mito JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,635
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Bei ni function ya vitu vingi sana mkuu, siyo transport peke yake! kuna kodi mbalimbali, mkono wa serikali, rushwa, purchasing power ya wateja wako n.k. Hivyo u-compare bei za nchi moja na nyingine utakuwa unakosea sana!
   
 5. Mracho Ngongoti

  Mracho Ngongoti Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 90
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Tanzaniano!? 95% ya raia hawajui kuhusu iyo mada!
   
 6. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Soko huru!! We tazama bei za viwanja ama nyumba/banda watu wakiweka humu!! havina sheria kwamba maximum price kwa eneo hili ni hivi!! utakuta mtu anaweka kiwanja ama shamba kuuza kisha kwenye bei anabofya namba anayojisikia kobofya kisha anaweka kidole kwenye sifuri mpaka asikie sound ya compyuta kwamba sasa imegota!! hio ndio bei!!

  Sasa mkuu huko kwenye cement panataka ufafanuzi wa ndani kwa wale wenye elimu hio wache watumwagie tu humu. cha ajabu cement inapatikana hapa tunazalisha wenyewe ila bei ni ya juu kuliko ile bei tunayowauzia huko nje kwa export!! tazama mfano tu wakati wa South Africa world cup cement ilivyopanda bei kwa wananchi hapa nchini na bei tuliyowauzia makaburu ukiambiwa unaweza kutapika. ngoja ntoke ntarudi
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  jibu ni rahisi sana.
  Kwa sababu CCM wapo madarakani.
   
 8. wade adams

  wade adams Senior Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  dollar kila siku inapanda dhidi ya shilingi yetu na mfumuko wa bei kila siku unapanda kwa sababu wanauchumi wetu waliacha vichwa chuo kikuu. wakamua kuvaa vichwa vingine vya kudanganya yaani siasa. hawazungumzii na kupanga mkakati namna ya kukusanya kodi kutoka kwa hao wanaokufuru badala yake wanawaachia TRA NA SERKALI ZA MITAA watusokote shingo sisi wanyonge. wakubwa wakillipa kodm,i maduka ya fedha za kigeni yakisimamiwa ipasavyo,, madini yetu yakilindwa,, biashara zetu zikilindwa cement badala ya kupanda bei iiashuka au kubaki pale kwa kipindi kirefu
   
Loading...