Dua
JF-Expert Member
- Nov 14, 2006
- 3,236
- 669
Kwa nini Barrick & Pangea wasishitakiwe London?
Ni aibu kwa Tanzania na Africa kwa Ujumla kwa WTZ kufungua kesi ya madai kwa kampuni ya Pangea na Mshiriki wao mkuu Barrick huko Uingereza ambao walikuwa wamepewa Tanganyika kama protectorate hadi hapo watakapoweza kujitawala. Lakini kama serikali ya JK haifanyi chochote kile kuweza kuondoa utata wa swala zima la mikataba ambayo haina kichwa kwa WTZ ni jukumu la wale wote ambao wanaona haki haitendeki kufungua kesi Tanzania na UK kuwashitaki Barrick na Pangea ili walipe fidia muafaka kwa wale wote ambao mali zao wamedhulumiwa na utawala ulioko madarakani. Kilio chao kimekuwa hakisisiski lakini kwa kutumia nguvu za makampuni makubwa ambayo yanadhulumu masikini popote duniani inawezekana kufungua kesi kama hii.
Tukumbuke vile wenzetu wa Botswana (Bushmen) walivyoweza kufanikiwa kuishitaki serikali yao kwa kuwaondoa kule kwenye ardhi za mababu zao ambapo kesi yao walishinda kwa kishindo. Tanzania ni kubwa kuliko kiongozi yoyote yule ama chama chochote kile na dhuluma haiwezi kukubalika katika karne ya 21.
Soma hapa
Soma hapa
Bushmen win land victory
Vile vile tukumbuke kuwa serikali ya Tanzania inaweza kulazimishwa kwa kutumia mahakama za UK kulipa fidia kwa waathirika.