Kwa nini AMREF Isomeshe watoto wa Kilimanjaro nje badala ya Pwani, Lindi, na Mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini AMREF Isomeshe watoto wa Kilimanjaro nje badala ya Pwani, Lindi, na Mtwara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by AridityIndex, Apr 18, 2011.

 1. A

  AridityIndex Senior Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimetafakari kwa kina juu ya suala hili sijapata jibu, naombeni kushare na wana JF wenzangu kulikoni katika hili. Nimepata kusoma katika makala nyingi sana hapa JF na kwingineko zikisisitiza kuwa katika mikoa hii ya pwani ikiwemo Lindi, Pwani na Mtwara ni mikoa ambayo iko nyuma kielimu kuliko mikoa mingine TZ. Tena makala hizo hazikuisha kutaja mikoa ya kanda ya kaskazini ukiwemo Kilimanjaro kuwa ni the best watu wamekula nondoz huko ni balaa na kila penye waTZ 10 wenye kazi nzuri basi 3 hadi 4 wametokea kilimanjaro. Yes wamesoma tena wamesoma vizuri hili halina ubishi, kwa nini wametutangulia watz wengine katika hili nadhani kila mtu anafahamu, na hiyo siyo hoja kwa thread hii.

  Maswali .

  Ni kwanini juhudi za kuelimisha watanzania zinaendelea kuelekezwa huko zaidi ya yale maeneo yaliyopo nyuma kama Lindi, Pwani na Mtwara?.

  Je kuna uhusiano kati ya watoa maamuzi yaani wale walioshika nafasi hivi sasa na uamuzi wanaoufanya wa kuelekeza rasilimali nyingi katika maeneo yao?

  Na je kwa haya maeneo ambayo kila mmoja wetu anakiri kuwa yapo nyuma kielimu yataendelezwaje iwapo wale walioko mbele bado wanaelekeza rasilimali zinazopatikana pamoja na miradi katika maeneo yao?.

  kampuni ya bia ya Afrika Mashariki (EABL)ni mfano mmojawapo tu lakini mambo haya yako sehemu nyingi TZ

  Jamani naomba ushauri wenu, hoja za msingi zitawafikia wabunge wa eneo hilo pia.

  unaweza kupata maelezo kutoka kwa kampuni ya bia ya Afrika Mashariki (EABL) juu ya mradi wa kusomesha nje watoto wa Kilimanjaro kwenye gazete la T/daima ya leo.
  http://http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=29853
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hata AMREF ni kundi la mafisadi
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ukimpa mtoto wa miaka miwili chungwa katikati ya watu, ukamwambia ampe mmoja wapo, kwa vyovyote vile atampa mama yake, au mtu mwingine wa karibu zaidi kuliko wale wengine wote. Ukiwa unatazama mpira ukaona inacheza timu ya nchi yako na nchi nyingine, lazima, mara nyingi utavutiwa kushangilia nchi yako, lakini kama zote ni za nchini mwako, ila moja ni ya wilaya yako utaishangia, kama zote ni za wilaya yako, ila moja ni ya kijiji chako, utajikuta unaishangilia

  Ina maana kuwa ni asili na hulka ya binadamu ya binadamu kupenda na kupendelea zaidi 'kwake', hata kama ni mtoto mdogo (asiyejua majungu wala wivu, wala ufisadi)

  So, kwa mifano yako, ama inaweza kuwa imetokea by chance, au kwa vigezo fulani, au kwa upendeleo. Na kama ni upendeleo, inaweza kuwa imetokea kama asili au hulka ya binadamu.

  Hata hivyo sababu kuwa ninayohisi, ambayo mara nyingi inasababisha baadhi ya maeneo yaliyoendelea kielimu, kupata miradi zaidi ni kwa sababu viongozi wake, na wananchi wake wako makini kutokana na elimu waliokwisha ipata zamani. Ina maana wana uwezo wa kuandika, kufafanua na kutetea miradi yao ya maendeleo kuliko sehemu zilizo duni kielimu...
   
 4. A

  AridityIndex Senior Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa mchango wako mkuu lakini huoni kuwa unahalalisha umakundi mkubwa katika nchi, pia ningeomba ufahamu kuwa kutokana na sababu za usomi kuwa kigezo cha uongozi karibu halmashauri zote za maeneo haya zinaongozwa na watu wasiokuwa wa huko. Tafadhali nini kifanyike sina lengo la kuwapa watu lawama.
   
 5. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Mziki wa kaskazini hutauweza kamwe....ni bora utafute mambo mengine ya kuongelea...Kule kulikucha zamani..sasa kama unataka na huko kwingine kukuche inamaana mitaa ya kaskazini kutakuwa kumeshakuchwa (magharibi) ...mitaa mingine kukikuchwa(magharibi) juu (kaskazini) kunakucha.......hela iliingia mitaa ile ndio ikaanza kusambaa kwingine.......Kiruu kya ndeesi....ndefo ileruya besa!
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani labda ni kutokana na mashirika mengi ya misaada kuona kuwa watu wa Kaskazini wana mwamko zaidi na kwa kuwapelekea opportunities nyingine hawataaribu, labda ni kwa sababu haya mashirika nayo yanategemea kupata fungu kutoka kwa wahisani na kigezo kikuu wanachokitumia wahisani kutoa fungu ni kuona kwanza result ya kilichofanywa mwanzoni, kwa mantiki hiyo, mashirika hayo yanakimbilia Kaskazini kwa sababu watu wa kule wako tayari tayari.

  Chukulia mfano unaenda Lindi kwa lengo la kuwapa watu nafasi za kwenda kusoma, kabla hawajakubali kupokea hizo nafasi wanataka uwashawishi kwanza na kuwaeleza umuhimu wa kwenda kusoma, mpaka wakuelewe labda mwaka umeshakatika, na wewe mradi wako ni wa miaka, say mitatu. Lakini ukienda Kaskazini unakuta watu wako tayari kwenda kusoma kwa sababu umuhimu wa shule wanaujua tayari, unawapatia fungu wanaondoka kwenda darasani, huitaji kuwashawishi.. Labda kwa misingi hiyo Mashirika mengi yanakosa msisimko wa kwenda kuanza moja mikoa mingine wakati ukieda Kaskazini utaanza na mbili au tatu...

  Kila mtu anataka kupata Positive result Ndugu, hata watoa misaada wanataka kuona misaada yao inatoa positive results na siyo kukatisha tamaa.

  Ila kama hizo nafasi zinatolewa kiupendeleo, basi siyo vizuri. Wahusika wajirekebishe...
   
 7. A

  AridityIndex Senior Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani hujakosea TANMO umeeleza vizuri lakini je tufanye nini, hapa tunaomba mchango wako wewe great thinker. Maelezo kama yako yamekuwa yakitolewa na hata viongozi wa serikali wanaolipwa mishahara kwa kutokana na kodi za wananchi. Kila kukicha maneno ndiyo hayo ninyi wajinga masikini na hamjasoma, na mazingira ya fursa yako hivyo tena kwa kukukumbusha tu ni kwamba miradi mingi ya maendeleo ni ya wafadhili na hali ndiyo hiyo je tufanyeje?. Tuendelee kuwa watazamaji tu huku nasi tukijihesabu kuwa ni watanzania?. Naomba mchango wako tena tafadhali
   
 8. A

  AridityIndex Senior Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ipi hoja yako mkuu mbona europe, s.africa, na America tunazungumzia mkuu hatukai kimya na huko tunajua walishaendelea zamani tena na wakatawala wenzao iweje huko north. Anyway hoja ni kutaka mchango wako inaonekana watu wanabana fursa na wameshika mpini sasa je sisi tutatokaje au tutokaje hoja ndiyo hiyo.
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  AMREF ni shirika linalofanya kazi kwenye maeneo ya kijiografia kutokana na vipau mbele vyao kama vilivyo kwenye mikataba ya miradi yao hawezi kufanya vinginevyo labda utambie wanaita Lindi Mtwara kuwa Kilimanjaro
   
 10. A

  AridityIndex Senior Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Froida soma tena mada na pengine michango michache ya wanaJF wengine, kisha uchangie vizuri umeombwa kutoa mchango wa kimawazo /fikra nini kifanyike endapo fursa zenyewe zipo kihivyo? je tubaki watazamaji tu kwenye nchi yetu huru na kwa nini hayo mashirika yaamue hivyo kwani hao wageni walilijua taifa hili kabla yetu?. Tunasubiri mchango zaidi kutoka kwako
   
Loading...