Kwa nini Ally Saleh akatazwe kugombea Urais TFF? Ni ubaguzi wa wazi

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Tanzania ni muungano wa nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar. Hilo halina ubishi kabisa. Pia ni kweli Zanzibar tunacho chama cha soka yaani ZFA.

ZFA ni mwanachama wa CECAFA NA CAF lakini wamekataliwa kuwa wanachama wa FIFA KWA SABABU SIO NCHI HURU.

Kwa kuwa FIFA wameamua hivyo kutokana na sheria zao, Mzanzibar moja kwa moja akiwa na vigezo anaruhusiwa kugombea na akishinda anaongoza TFF.

Kama Viongozi wa Bara hawamtaki Ally Saleh au Mzanzibari yoyote TFF hakuna shida. Ishakuwa Zanzibar wana bendera yao,wana wimbonwa Taifa n.k Basi hamna shida.

Serikali kuu ya muungano ipeleke taarifa FIFA kuwa zanzibar ni taifa ndani ya muungano. Mfano united kingdom wanatambulika na fifa na nchi 4. Nazo ni england, scotland, wales, northern ireland.

Nasi TFF baada ya kupata baraka za serikali kuu watuombee, tukipata hakuna mzanzibari kama ally saleh atakaribia ofisi za tff. Tena nawahakikishia zanzibar tunao vijana youngstars wazuri sana lakini hawachaguliwi kwenye timu za taifa za muungano.

Nawachallenge, ushafahamu sio, fifa ikiwakubalia zfa zanzibar itakuwa mbali sana kisoka. Kwa sasa mwacheni ally saleh akitimiza masharti agombee. Mara ngapi zanzibar imewatwanga bara katika challenge cup? Jibu mnalo TFF.
 
Wazanzibari bana 😁, chenu chenu peke yenu. Cha Tanganyika chetu sote. Kubalini ZRFA kuwa chama cha mpira cha mkoa wa Zanzibar kwanza ndipo TFF itakuwa yetu sote.
Yaani imebidi nicheke kwa sauti kubwa 🤣🤣🤣😂😂😂
 
Hilo swala tuwe makini makini nalo, je kuna mtanzania kutoka Tanzania bara anaweza kugombea hata ujumbe wa mtaa huko visiwani? Vipi ZFA, inawezekana?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Hawa wengine hawajui wanaongea nini. TFF kuiwakilisha Tanzania kimataifa na kuizuia Zanzibar na wazanzibari mmoja mmoja kupata haki ya ushiriki no unyonyaji na ubaguzi Wa wazi.

TFF ni Kwa maslahi ya Tanganyika na sio Zanzibar kisiwakilishe Tanzania.

Huyu chawa anawanyonya Wazenji.
 
Wakiruhusu na sie wenye vichogo kugombea Zanzibar ndio nitawaelewa
Hujui unaongea nini wewe. RAIA Wa nchi mshirika Wa muungano ananyimwa kugombea kwenye taasisi inayowakilisha muungano.TFF iitwe Tanganyika Football Federation na sio Tanzania Football Federation.

Ally Saleh anawakilisha kilio cha wazanzibar na Ana hoja nzito.

Wanufaika wanatoka povu
 
Mpira wenyewe mnaujua nyie? Mbona kwenye cecafa hamjawahi hata kubeba ubingwa? Vitimu vyenu vikienda kwenye mashindano ya CAF vinaishia kula vichapo katika preliminary round.

Nyie mnapenda kudeka kama watoto. kwanza nyie wabaguzi sana na nawachukia sana kwa udini udini wenu utafikiri nyie ndo mmeanzisha hiyo dini.
 
Back
Top Bottom