Kwa nini ajali nyingi hutokea pindi watu wanaposafirisha maiti?

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,613
864
WanaJF,
Naomba leo mnisaidie juu ya jambo hili silielewi kabisa?
Natumaini kila mtu atakuwa ameshawahi kufiwa na ndugu yake yoyote katika maisha yake hali inayolazimu kusafirisha maiti.

Takwimu ambazo siyo sahihi lakini zina ukweli ndani yake ni kwamba misafara mingi sana inayosafirisha maiti aidha hukumbwa na vimbwanga vya ajabu ajabu au ajali kabisa na kisababisha tena vifo vya watu wengine!!!!!!

Hii haiishii kwa wanaosafirisha hata ndugu mbali mbali ambao nao huja hujikuta aidha wamepata ajali au kukoswa koswa na ajali mbaya kabisa!!!!

Swali langu kwenu mnisaidie kuna nasaba gani ya maajali yasiyo kuwa ya kawaida na misiba?

Kama kuna mtu itakuwa imemgusa kwa namna moja au nyingine natanguliza samahani kwake sina lengo la kumkumbusha machungu.

Nawakilisha.
 
Kaka ni kweli lkn sijui ni kwa nini. Pengine ni jambo ambalo linahusisha imani, maanake wengi wa wanaokumbwa na mambo hayo huwa wanakuwa na sbb, pengine marehemu alisema azikwe sehemu fulani na wao wanampeleka sehemu nyingine.

Hata mimi mwenyewe nitazua varangati, maana nimewaambia nikifa nizikwe pale kwenye ikulu ya marekani, sasa any attempt kunizika sehemu nyingine itaambatana na radi na mvua ya mawe.
 
Hapo ndipo linapokuja suala la imani za kidini na imani za kijadi. Kuna uhusiano gani wa mtu aliyekufa kama hataki kupelekwa huko kwao na watu kupata maajali wakati keshakufa?
 
ukimsafirisha maiti kichwa kiangalie anakotoka , sio anakoenda "hii ni moja ya sbb kuu".. pia consent sehemu ya kumuhifadhi marehemu izingatiwe endapo aliacha usia wa wapi azikwe. na mwisho hakikisheni hakuna ufisadi utakaofanyika kwa kile alichokiacha hadi hapo atakapohifadhiwa ktkt nyumba yake ya milele!
 
Mkuu nashukuru kwa maelezo ambayo yamekaa kiimani zaidi hasa katika sentensi yako ya kichwa kiangalie alikotoka na si anakokwenda! Hili nilikuwa silijui.

Na hili na wahudhuriaji nao kupata na ajali au kukosakoswa nalo unalisemeaje mkuu?
 
mukisafirisha maiti kwenye gari or ndege inatakiwa mubebe vijiwe 2 vya changarawe.1 kinawekwa miguni 1 kichwani kwa maiti,ampati ajali wara mauzauza
 
kuna jamaa zangu wanasafirisha maiti kutoka Dar kwenda Mwanza, tairi za coaster zimepasuka leo pale Dodoma.
 
kuna jamaa zangu wanasafirisha maiti kutoka Dar kwenda Mwanza, tairi za coaster zimepasuka leo pale Dodoma.
Kunaa jamaa walikuwa wanasafirisha maiti kutoka Dar - Singida kufika Morogoro gari moja iliyokuwa kwenye msafara ikaligonga gari lenzake kwenye msafara kwa nyumba na kulichakaza!!!!!

Kuna jamaa walikuwa wanahudhuria mazishi ya mtangazaji wa TBC1 aliyezikwa leo, hao jamaa walipata ajali na baadhi kufa wakitokea Mbeya!!!!

Yaani sielewi kabisa.
 
Dah naandaa point nitarud...kuna mikasa kama 4 naandaa rejea yake!

Mkuu naisubiri hiyo mikasa, inaweza ikatoa mwangaza zaidi watu wanaposafirisha maiti nini wafanye kiimani z kidini au kitamaduni.
 
jana asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kazini jirani na hapa ninapoishi ulikuwepo msiba na mwili ma marehemu ulikuwa unapakiwa kwenye gari. Dereva na jamaa wa marehemu wakiwa wanapakia mwili wa marehemu kwenye pick up breki za gari zilifyatuka na gari lilianza kuseleleka kwa mwendo mkali(eneo hilo lina mteremko)
Ilikuwa kama sinema fulani hivi,kama dereva asingefanya ujanja wa kupitia dirishani akitokea nyuma na kufunga breki basi jeneza lingesambaratika na watu watano waliokuwa garini maisha yao yangekuwa hatarini....nadhani jambo hili sio la kubeza.
 
[/FONT]QUOTE]Takwimu ambazo siyo sahihi lakini zina ukweli ndani yake ni kwamba misafara mingi sana...
Mfumo wetu wa elimu ndio unazalisha watu kama huyu sasa... "Takwimu ambazo siyo sahihi lakini zina ukweli..." Tunajenga Taifa la vigagula vyenye ma imani yasio na vichwa wala miguu wala uelewa.

Kwa hiyo umekusanya takwimu za kichawi chawi ambazo we mwenyewe unasema sio sahihi lakini zina ukweli!

Hili swali lilifaa alijibu mtoto wa shehe yahaya, ndio alieachiwa urithi wa mambo haya ya kichawichawi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom