Kwa nini Ajali hizi tusione kuwa ni zaidi ya nchi kuwa VITANI?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
Kwa Mujibu wa Takwimu za ILO, Vifo vitokanavyo na uzembe kazini na ajali ni Vingi kuliko watu wanaokufa Kwenye VIta na Majanga ya asili. Director General wa ILO Guy Ryder.

Inakadiliwa watu 2.3Mil wanakufa duniani kwa mwaka kutokana na ajali pamoja na uzembe kzn idadi ambayo toka vita vya dunia Hakuna vita vilivyoua watu kama hawa. Ni vita vya wakorea vilivyoua watu 1.2MIl ndio vinashika record hadi sasa.

KWA TAKWIMU HIZO;
Vita vyenye kumbukumbu na kuacha majonzi nchini ni Majimaji na Kagera. Lakini kiukweli watu waliofariki na Gharama taifa lililoingia ni kama Asilimia 5 tu ukilinganisha na hili la ajali ukiliangalia kwa kizio cha tatu. Kuna gharama kubwa sana kuondokewa na Mtanzania mmoja tena kizembe.
Ninashauri Serikali itangaze Taifa lipo katika vita, Vita dhidi ya Vifo vya kizembe vinavyoligharimu Taifa sana.

NINI KIFANYIKE?
Wakati wataalamu wetu na wanasiasa wanapaswa kufikili upya juu ya vita hivi. Dunia ya sasa Technolgia inatatua Matatizo wmegi kwa kutumia Technology, . Kuna system zinazitumia GSM na GPS technologies kutrack na kucontrol speed nyingi. Kwa nini Taifa lisiwe na Vehicle control room inayofanya remote monitoring ya mienendo ya Mabus yetu. Wenye magari makubwa ya mizigo wamefanikiwa ktk hili. Presidents Delivery beaural (PDB) kama mlivyozama kwenye BRN LAB mkaja na hii ya Polisi juzi, hili nalo mliangalie kwa mapana maana Ni aibu kwa Taifa inapanga maendeleo wakati huohuo watekelezaji wa hiyo mipango wanakufa kizembe mabarabarani.

Yangu ni Hayo, Mchana Mwema.
 
Back
Top Bottom