NEW NOEL
JF-Expert Member
- May 21, 2011
- 863
- 407
Nimefikiria sana ila nimekosa majibu kuhusu ili suala la ulipaji kodi kati ya Vodacom na Airtel. Hivi karibuni TCRA wametoa idadi ya wateja kwa kila kampuni ya simu ilionao. Na Vodacom wana wateja Milioni 10 huku Airtel wakiwa na wateja Milioni 5 tu. Lakini ukiangalia orodha aliyotoa Waziri Mkuu wakati kuahirisha Bunge hivi karibuni ilionesha Airtel kama moja ya makapuni kumi yanayoongoza kwa ulipaji kodi nchini na Vodacom haikutajwa kabisa. Na ukitazama idadi ya wateja utaona Vodacom wana wateja wengi kuliko Airtel na Tigo. Jamani kuna suala la uchakachuaji hapa au kuna nini?