Kwa nini Afrika ipo nyuma miaka 25 kimaendeleo ikilinganishwa na nchi za magharibi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Afrika ipo nyuma miaka 25 kimaendeleo ikilinganishwa na nchi za magharibi??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Mar 8, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wandugu,

  Nimepokea email kutoka kwa rafiki yangu mmoja inayohusu sababu za Bara la Afrika kuwa nyuma kimaendeleo. Kimsingi, zipo sababu nyingi zinazotufanya waafrika tuwe nyuma kimaendeleo. Tumekuwa tukizijadili mara kwa mara lakini mwandishi wa email hiyo ameibuka na suala ambalo kwangu mimi ni jipya; halikuwepo kabisa kwenye mawazo yangu nalo ni umri wa viongozi wanaoongoza nchi husika. Mwandishi amejaribu kuonyesha takwimu za umri wa viongozi wa kiafrika ambao bado wapo madarakani katika nchi zao na ameonyesha pia umri wa viongozi waliopo madarakani katika nchi za magharibi. Kwa mujibu wa takwimu alizotoa, wastani wa umri wa viongozi wa kiafrika ni miaka 76 wakati wenzao wa nchi za magharibi ni miaka 51 ambapo ni tofauti ya miaka 25. Bahati mbaya thread hii naipost kupitia kwenye simu ya kiganjani lakini nikipata access ya computer nitaweka kwenye thread hii orodha ya viongozi hao, umri wao na nchi wanazoongoza.

  Hitimisho la email hiyo ni kwamba Bara letu la Afrika lipo nyuma kimaendeleo kwa sababu ya kuongozwa na watu ambao umri umesonga mbele mno yaani wazee waliofika mwisho wa kuwaza na kuchambua mambo, wasioweza kupambana na changamoto za sasa. Swali langu ni je, kuna mantiki yoyote katika hoja hii? Nauliza hivi kwa sababu kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, hata Marekani mara nyingi tu imewahi kuongozwa na marais wazee na kamwe haikutetereka. Mfano mmojawapo ni Rais Reagan.
   
Loading...