Kwa ninayoyaona ni wazi kuwa Dar es Salaam maisha ni rahisi kuliko mkoa mwingine wowote Tanzania

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,042
10,463
Vijana wanakwenda na Trend kwenye kila kitu kuanzia fashion(mavazi na viatu), vyombo vya usafiri, simu na life style za kinyamwezi na Bata lao halisubiri wikiendi.

Matamasha ya muziki wakati wote huku kumbi zikiwa na nyomi la raia ambao sura zao zinaonyesha wazi kuwa hawana stress na wanakula maisha tu the fullest.

Haya yanathibitisha kuwa Dar es salaam ni sehemu sahihi ya kuishi kwani watu wana pesa za kukidhi mahitaji yao muhimu na pia wana excess ya pesa kwa ajili ya anasa.

Huku nilipo unafanya kazi ngumu kuanzia asubuhi mpaka jioni unapata Tanzania shilingi 5000 hata kama unapenda kwenda na Trend itabidi ukubali tu Trend itangulie wewe utakuwa unaifuata mdogo mdogo.

From northern part of Tanzania.
 
Back
Top Bottom